Kwako Mheshimiwa S. Sitta

Mzee Dogo

JF-Expert Member
Nov 13, 2010
400
140
Kwanza nikupongeze kwa ushindi wa kishindo ulioupata kwa kukalia kiti cha Uenyekiti wa Bunge la Katiba, hii ni ishara kubwa kuwa si tu wabunge bali watanzania wengi wameweka matazamio makubwa kwako kuwa unao uwezo wa kusimamia mchakatoa wa kuwatimizia haja yao ya muda mrefu wa kupata katiba mpya.. Hongera!

Pamoja na pongezi nyingi ambazo umepokea na utakazoendelea kuzipokea kutoka kila kona ya nchi hii naomba nikukumbushe kuwa hili sio la kukuvimbisha kichwa bali tambua kuwa jukumu kubwa sana limewekwa kwako hasa ukizingatia changamoto tulizonazo kama taifa.

Ninatambua kuwa chama chako hawakukutuma wala kukupitisha ukawe mgombea kwa kukurupuka, kuna vitu wanaamini utasimamia maslahi yao ndio maana wakakutuma uende. So wakati unafanya chochote ufanyacho kumbuka kuna watanzania wanakutazama na wanasubiri busara zako ziwafute machozi yao ya muda mrefu.

Niliwahi kusikia eti unataka kuwa rais wa hii nchi, sina uhakika ila kama ni kweli gap hilo, take the lead...!

N.B: Kuna moja lazima litokee kati ya haya mawili, mosi ujiongezee umaarufu na kujisafishia njia ya kuelekea kwenye yale majengo meupe na pili ujipake matope na hata usafi uliokuwa nao kidogo uondoke na ubaki kuwa ni mmoja kati ya wasaliti wakubwa wa Tanzania na wanzania kwa ujumla.

Kazi kwako, tulioko nje ya mjengo yetu macho!
 
we naye unataka tu kuolewa na mheshimiwa!...huna jipya mbebez! Kuna "nyuzi" kibao za sitta humu ndani. Na wewe unataka uonekane umetoa uzi!
 
Back
Top Bottom