Elections 2010 Kwako Mheshimiwa Raisi

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
7,022
9,285
Pole sana na hekaheka za uchaguzi na majukumu mazito ya kuliongoza Taifa letu.
Ni dhahiri kwamba kwa sasa utakuwa unaipanga serikali utakayofanya nayo kazi kwa miaka mitano ijayo.

Na hili ni ombi langu kwako.
(1): Mpe profesa Lipumba kazi ya Uchumi, mfanye hata mshauri wako: hiki kichwa ni hazina kubwa sana kwa Taifa. maana kwa kuwa tunajenga nyumba moja, kila mwenye kuweza kubeba fito na azibebe.

(2)Ili kutekeleza vilivyo azma ya Kilimo Kwanza, toa incentive kwa vijana wetu wachukue masomo ya kilimo katika ngazi za vyuo vikuu: kwa sababu ninaamini pasipo na wataalamu wa kutosha, Kilimo kwanza itasuasua, pia na scholarship kwa vijana watakaosomea kilimo ni bora pia zikaongezwa.

(3) Kuhusiana na National service, ni dhahiri kwamba ile national service ya kwenda kupiga kwata na kuimba nyimbo za kuwasifu viongozi imepitwa na wakati, napendekeza uunde national service ambayo itaweza kuwafanya watu watumie vipaji vyao kiukweli ukweli kulisaidia taifa, mathalani kwa vijana wanaomaliza kidato cha sita, ambao wana rekodi ya kufanya vizuri sana katika masomo yao, wanaweza kujitolea kwenda kufundisha katika shule hizi mpya tunazozijenga maarufu kwa jina la shule za kata, wakati huo wakisubiri muda wao wa kwenda vyuo vikuu, hii inaweza kuwa modelled na ile peace corps ya wamarekani.
 
Mkuu si Jk anayepanga baraza lake. He is highly remotely controlled na wenye urais nao ushauri wako huu (mzuri) ni sumu kwao.
 
Pia namshauri Rais JK amuamuru Chenge asigombee u-spika wa bunge, nia ainu na kashfa kwa Taifa letu na nje pia
 
Mm niatamani Mh Rais angetumia zile nafasi zake 10 za kuteua wabunge angewapa Profesa Lipumba na Dr Slaa. hapo ndipo wananchi tutajua kuwa viongozi wetu wanajali mustabali mzuri wa taifa letu, ndani na nje ya nchi.
 
JK na CCM kwa ujumla wao hawako kwa maslahi ya Taifa wako kwa maslahi binafsi zaidi, kuna watendaji wzuri tu ndani ya CCM lakini hawapewi nafasi kwa sababu watatenda haki na watapendwa na watu, ni vigumu sana kwa JK kumpa Lipumba ama Mpinzani yoyote nafasi ya uongozi, labda wanaoweza kupewa ni Zitto na Mrema
 
c.c:Rostam Aziz
Edward Lowasa
Endrew Chenge

then your request will be absolute considered in deep concern with the road to success
 
kwanza lilikuwa ni tusi kubwa aliposema ccm huwa wanajenga nyumba moja na hawatumi fito.

maana yak ni kwamba kamwe watatumia ilani yao kutekeleza ahadi zao na sio kuchanganya na ilan ya cuf.

pili kikwete alivyo hawezi kumtumia lipumba maana na yeye anaongozwa na watu wake.
 
Back
Top Bottom