Kwako Mama Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania na Waziri TAMISEMI

Chineduchi

Member
Apr 2, 2021
12
5
Kwanza naomba nikupongeze kwakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumteua Waziri mpya TAMISEMI najua uchapaji wake kazi sio wa kitoto.

Naomba mama ikikupendeza tendea haki uhamisho wa watumishi waliokamilisha uhamisho na kusubiri vibali kutoka tamisemi, maana kuna màmbo ambayo sio mazuri yanayo endelea hapo wizarani. Watumishi wanahama kimafungu kwakupitia mlango wa nyuma, sio jambo jema kwaserikali yako.

Naomba haki itendeke kwa wote kulingana na sheria ya utumishi inavyo hitaji.

Kwamama yote mema yanawezeka.
Asante
 
nyie watumishi hasa walimu ndiyo mmetuharibia nchi yetu, karma bado itawaandama wale wote mlohujumu uchaguzi wa 2020.
 
Hayo matokeo ya uchaguzi yalitangazwa na hao walimu! Acha kuwasingizia watu. Mchawi wenu ni Tume mbovu ya uchaguzi, Polisi, Uvccm waliopo Tiss, na nyinyi wenyewe!

Tuliwatahadharisha humu jukwaani kususia huo uchaguzi, lakini hamkutaka! Sisi wengine tulibaki zetu nyumbani siku ya kupiga kura! Nyinyi mkashiriki. Leo hii mnahamishia magoli kwa walimu wasio na nguvu yoyote ile kwenye uchaguzi!

Huu ni wakati muafaka kwenu kujenga mahusiano na huyu mama ili awape Tume Huru ya Uchaguzi, na pia akubali kuurejesha Mchakato wa Katiba Mpya ili tuwe na Uchaguzi huru na wa haki, lakini pia madaraka ya Rais yapunguzwe katika teuzi na mamlaka yake.

Acheni kupoteza muda wenu mwingi kumsifia! Baadae mtakuja mjute. Msisahau huyo ni CCM kama wale wengine! Hivyo atakiangalia chama chake kwanza siku zote badala ya Nchi.
 
Engineer Nyamuhanga amehamishwa tamisemi,sasa kila kitu kitakaa sawa. Yule alikuwa mungu mtu hapa tamisemi
 
nyie watumishi hasa walimu ndiyo mmetuharibia nchi yetu, karma bado itawaandama wale wote mlohujumu uchaguzi wa 2020.
Hapa utawabebesha lawama wasizostahili tu walimu wetu. Hawakupanga matokeo na wala hawakuchakachua ila interahamwe ndo walichakachua pengine kwa kuwatisha na makombeo kuwa kama wangetoa kama yalivyokuwa kwa uhalisia wake basi wangeumia kwa namna moja ama nyingine
 
Ikiwezekana ipangiwe kiasi cha kukusanya(lengo), kama vile matraffic. Kuwe na tozo maalumu inayotambulika kiserikali kama ada ya uhamisho.
 
Hayo matokeo ya uchaguzi yalitangazwa na hao walimu! Acha kuwasingizia watu. Mchawi wenu ni Tume mbovu ya uchaguzi, Polisi, Uvccm waliopo Tiss, na nyinyi wenyewe!

Tuliwatahadharisha humu jukwaani kususia huo uchaguzi, lakini hamkutaka! Sisi wengine tulibaki zetu nyumbani siku ya kupiga kura! Nyinyi mkashiriki. Leo hii mnahamishia magoli kwa walimu wasio na nguvu yoyote ile kwenye uchaguzi!

Huu ni wakati muafaka kwenu kujenga mahusiano na huyu mama ili awape Tume Huru ya Uchaguzi, na pia akubali kuurejesha Mchakato wa Katiba Mpya ili tuwe na Uchaguzi huru na wa haki, lakini pia madaraka ya Rais yapunguzwe katika teuzi na mamlaka yake.

Acheni kupoteza muda wenu mwingi kumsifia! Baadae mtakuja mjute. Msisahau huyo ni CCM kama wale wengine! Hivyo atakiangalia chama chake kwanza siku zote badala ya Nchi.
Nikwel ila hata JK alikuwa CCM lkn tulienjoy maisha, ishu sio chama hata chadema kunanini jipya kule wamejaa wachumia tumbo tu, nawanaharakati
 
Back
Top Bottom