Kwako Magreth Samwel Sita

Masanilo

Platinum Member
Oct 2, 2007
22,286
4,493
Kwako Magreth Sita

Mimi sina kipaji cha kuandika mengi, ila nina ujumbe mfupi tu naomba umfikishie mheshimiwa spika wa bunge la muungano, Samweli Sita, ninafahamu huwa anakusikiliza kuliko mtu yeyote. Maana bila wewe kumkumbatia na kumkanya asingeweza kuwa hapo alipo. Kumbuka yale maisha ya kule Tabora ukifundisha kabla hujaingia kwenye siasa. Ujumbe wangu nakuomba mama mwambie Sita afuate sheria za Bunge awe mkali na mwenye akili, atumie elimu yake ya sheria kuwaita wale wote wanaikandia kamati ya bunge iliyoongozwa na Mh Mwakyembe, nitawaja wachache Mbunge wa Monduli yule mwenye hisa Richmondi (Lowassa), Karamagi, Ole Naiko, Yona waje bungeni wahojiwe kwanini wanadhalilisha na kulidhalau bunge? na watanzania kwa jumla....Mwambie kabisa mzee Sita sasa tunataka kuona zile speed na standard asijaribu kukimbia vita avipigane tupo nyuma yake na mama upo! Asizushe safari ya marekani wakati tunamhitaji, mkumbushe kama angeenda na mjadala wa Richmondi ukasitishwa Lowassa angeendelea kuwepo kama PM aibu fisadi huyo. Pamoja tunajua ni shabiki wa CCM aweke utaifa mbele na Mungu atamtangulia....

Mwisho mama Magreth karibu jimboni wakati wowote usitutupe, tunakukubali, tunakuandali asali na maboga najua huwa bado unapenda,

Wasalaam

MwanaMtama
 
Back
Top Bottom