KWAKO JK a.k.a MJOMBA! SOMA USHAIRI HUU ILI TUONE UTAAMUA NINI!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KWAKO JK a.k.a MJOMBA! SOMA USHAIRI HUU ILI TUONE UTAAMUA NINI!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyakarungu, Jul 10, 2011.

 1. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Nami nashika kalamu, namuandikia mjomba,
  Kusema tena sina hamu, sasa nataka kuimba,
  Nayosema ni muhimu, sio kwamba mimi natamba,
  MJOMBA JAMANI MJOMBA, SIKIA HAYA MJOMBA..!X 2

  Mpoto kaianza zamu, kakuimbia mjomba,
  Imefika yangu zamu, wa kijiji sasa ninalumba,
  Tunapinga udhalimu, mafisadi kutamba,
  MJOMBA EWE MJOMBA, SIKIA HAYA MJOMBAA..X 2

  Kwa hilo ninakulaumu, usichukie mjomba,
  Kidogo tunakushutumu, naimba sasa kama komba,
  Hoja zangu sio ngumu, ninakuasa kama kolimba,
  MJOMBA EWE MJOMBA, SIKIA HAYA MJOMBAAA...X 2

  Hasa hao mabinamu, waliokuzunguka mjomba,
  Na wao ninawashutumu, kwa kutufanya sisi manamba,
  Wamenogewa na utamu,hata kidogo wanakomba,
  MJOMBA EWE MJOMBA, SIKIA HAYA MJOMBAA...X 2

  Loliondo mmeshaiuza, mkauza nayo Buhemba,
  Masaki Beach mwaiuza,imekuwaje tena mjomba,
  Na kila tunapowauliza, mwaunguruma kama simba,
  MJOMBA EWE MJOMBA, SIKIA HAYA MJOMBAA...X 2

  Mmemkubalia Nduru, imekuaje tena mjomba,
  Wamejenga kwa kufuru , sio nyumba haya ni majumba,
  Kaja juu kama faru, eti anastahili mjombaa,
  MJOMBA EWE MJOMBA SIKIA HAYA MJOMBAA...X 2

  Wawekezaji watunyanyasa, mbona u kimya mjomba,
  Machozi tunayapangusa, twabak kulia au kuchemba,
  Tatizo ni nini hasa, nakuuliza mjomba,
  MJOMBA EWE MJOMBA, SIKIA HAYA MJOMBAA...X 2

  BADO BILILLA HOTEL YA SERENGETI NITAIWEKA BAADE!!!
   
 2. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kumbe na kwenye hi fani umo?
   
 3. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Nyimbo yako nzuri sana inaweza kukutoa
   
 4. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  huku ndiko nilikoanzia mkuu.
   
 5. m

  mndeme JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2011
  Joined: Sep 2, 2008
  Messages: 322
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  naona na ww unataka upewe fedha kama mpoto ili utulie, endelea atakutafuta
   
 6. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  hahahaaaa itanitoa kama mjomba atajibu kwa vitendo kaka.
   
 7. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Haahahahaaaa, looo haya mkuu!!siwezi kukuzuia na harakati za fikra zako ndio hizo go go on.
   
 8. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #8
  Jul 10, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  endelea na huku ndipo panakufaa
   
 9. J

  JikeDume Member

  #9
  Jul 10, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  du!!!!! nyakarungu umenifanya niamini unaakili sana haya kaka endelea na harakati zako, ila samahani naweza kujua uko wapi sasa?
   
 10. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #10
  Jul 10, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  yaani una maana niache fani ya taaluma niliyoisomea au niachane na siasa nibaki mwanamuziki?
  kuhusu sanaa naifanya bado.
   
 11. N

  Nyakarungu JF-Expert Member

  #11
  Jul 10, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  ninaku PM.
   
 12. M

  Mbwazoba Member

  #12
  Jul 10, 2011
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bonge la shairi nakupa thanks la kutosha mkuu, usalama wa taifa wataiprint na kumpelekea usihofu ujumbe utampata
   
 13. P

  Peter bedson Member

  #13
  Jul 10, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuwasiliane mzee ww ni msanii ili utoke
   
 14. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #14
  Jul 10, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  vyote viwili mkuu
   
 15. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #15
  Jul 10, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,826
  Likes Received: 553
  Trophy Points: 280
  Nzuri sana hii mkuu...Tunapaswa kutumia kila njia kufanikisha ukombozi wa Taifa letu.Kairekodi basi!
   
 16. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #16
  Jul 10, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  endelea kuimba uhenda mjomba atakusikia
   
 17. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #17
  Jul 10, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  hongera kaka! thou kalala iko siku atasikia
   
 18. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #18
  Jul 10, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
 19. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #19
  Jul 10, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  kajifunze tena lugha. Ujue kutofautisha wingi na umoja
   
 20. Kikarara78

  Kikarara78 JF-Expert Member

  #20
  Jul 10, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,160
  Likes Received: 513
  Trophy Points: 280
  Nyakarungu, Mistari imetulia na Ujumbe nafikiri umefika, Kumbe Watanzania tunaweza
   
Loading...