Kwako Heri James, mwenyekiti wa UVCCM Taifa

Umerudi shule au bado unahangaika na mitaa? Unajiponza bureee! Maliza shule ndo uhangaike na siasa. Utakuwa kama akina Mnyika na Mbowe na soon tutaweka mahitaji ya digrii kuwa Mbunge.

Uliyoandika yote yameshaelezwa magazetu ya leo, yakieleza msimamo wa K/mkuu wa CCm juu ya hilo. Dogo unaleta tena mitandaoni, ili iweje?

Katibu Mkuu wa CCM kalipeleka hilo SUALA Polisi?

Waliotumia lugha za Kijinai wamehojiwa?
 
Mtoto Wa Dada hakuwa na sifa ya ushindi bali alilazimishwa ashinde kwa nguvu ya maagizo,chama ni Mali binafsi ya familia
 
Natumai unaendelea vyema na majukumu yako kama mwenyekiti. Naomba nitumie nafasi hii kutoa maoni yangu juu ya kauli zako na za viongozi wa chini yako wa UVCCM. Hii ni kama njia ya kuelimishana sababu sisi sote ni vijana mbali na tofauti za itikadi ya vyama vyetu.Wewe ni mwanachama wa CCM, mimi ni mwanachama wa ACT wazalendo ila tunaweza kuelimishana na kuelekezana kama vijana.

Ndugu Heri James, imekuwa ni kawida kwako mara zote kutoa kauli za kutisha,kukashifu,kutukana viongozi wa vyama pinzani ,pia na wenye mitizamo tofauti na chama chenu cha CCM.

Ndugu Heri James, aina ya siasa zenu za matusi na kashfa zimezidi kuigwa na viongozi wengi wa UVCCM walio chini yako mara nyingi wamekuwa na kauli za vitisho na chuki dhidi ya wote ambao wanakinzana mitazamo na chama chenu.

Ndugu Heri James, kwa haraka sana nimegundua changamoto kadha kama sio udhaifu kutoka kwako na viongozi wenzako wa UVCCM.

Udhaifu wa kwanza hamsomi na kutii katiba ya chama chenu ya 1977 toleo la 2017 wala hamsomi muongozo wenu wa UVCCM na kuutii.

Mbili ,hamuheshimu wala kutii mawazo ya viongozi waandamizi wastaafu wa chama chenu na taifa letu.

Naomba ufungue akili ili upate kuelimika kidogo sababu ni moja ya wajibu wako kama mwanachama wa CCM kujielimisha kadiri uwezavyo imelezewa ibara ya 15 ibara ndogo ya 6 ya katiba ya chama chenu cha CCM.

Ndugu,Heri James kauli yako uliyoitoa dhidi ya viongozi wa upinzani kwamba mmewadekeza sana bila kuwaonesha vurugu ,kwamba wanaenda hotelini ,kwamba mnakaa nao siti moja katika ndege bila kuwaonesha vurugu na kuagiza vijana wawafanyie vurugu ni kauli ya chuki,yenye kuchochea vurugu na uvunjifu wa amani katika nchi yetu.

Ndugu Heri James,kauli zako hizo za kutusi,kukashifu zinakufanya kabisa kutokuwa na sifa ya kuwa hata mjumbe wa nyumba 10,wewe ni kiongozi usio soma wala kuelewa katiba ya chama na muongozo wenu wa UVCCM.

Tafadhali,ebu soma hii,ukisoma katiba yenu ya CCM ibara ya 8 ,inazungumzia juu ya sifa au masharti ya uwanachama katika ibara ndogo ya (1) mtu anayeheshimu watu ,ibara ndogo ya ( 6) mtu mwenye tabia nzuri kwa vitendo vyake na kauli zake.

Pia ukisoma Muongozo au kanuni za UVCCM toleo la 2017 ,ibara ya 10 ,juu masharti ya uwanachama wa UVCCM ,ibara ndogo ya (4) mwanachama wa UVCCM awe kijana anayeshimu watu ,mwenye tabia nzuri,muaminifu,mwenye kauli na vitendo vizuri mbele ya jamii.

Ukisoma pia ibara ya 8 ya Muongozo au kanuni za UVCCM inazungumzia juu ya kazi ya UVCCM ,ibara ndogo ya,
(iv) kutetea na kudumisha haki na maslahi ya vijana katika fani mbali mbali .

Pia ibara ndogo ya,
ii)Kuongoza shughuli zote zinazohusu maendeleo na ustawi wa vijana.

Ibara ndogo ya
(viii), kukuza uhusiano na ushirikiano baina ya umoja wa vijana wa CCM na vyama vingine vya ndani na nje, taasisi za ndani na nje zinazojishughulisha na maslahi ya vijana. Husomi wala hutii hata sheria zenu.

Miongozo ,kanuni ya UVCCM na katiba yenu ya CCM hutofautiana na matendo na mienendo yenu kabisa .Sasa hatuelewi mnaongozwa na sheria zipi za chama chenu ,kama hamuheshimu wala kutii hata Sheria zenu mnaweza kuheshumu watu kweli?.

Kila siku mnawakusanya vijana wa UVCCM mnaishia kutukana watu tuu badala ya kuwasemea vijana juu ya maslahi yao ,ajira ,mikopo na mambo mengine hata nyie vijana mjiongeze someni mjue kazi ya UVCCM na sio kudanganywa danganywa.

Uliwahi kutoa kauli mbaya kuhusu watu ambao wanakosoa matendo ya viongozi wa chama chenu na sera zenu ukasema hadi mlale na wake zao ndio waelewe mazuri yanayofanywa na Rais,unakumbuka kauli ya mwenyekiti wa UVCCM Dar alisema wabunge wapimwe marind* ,umesikia kauli ya mwenyekiti wa UVCCM Iringa juzi ,ulisikia kauli ya Kiongozi aliyetamka wazi na kuimba "apigwe Tundulisu apigwe" Kuna kauli nyingi wote hawa wewe kama mwenyekiti ndio kinara wao wa matusi na kashfa hamtaki kukosolewa ikiwa Katiba yenu ya CCM ya 1977 toleo la 2017 ,ibara ya 15 ,ibara ndogo ya 7, "Mwanachama wa CCM anapaswa kuwa tayari kukosolewa ili kuwa na msimamo sahihi.

Sina muda ningekuonesha kauli na nia njema ya viongozi wastaafu wa CCM na serikali ambao ndoto yao kubwa ilikuwa ni kuboresha demokrasia ya vyama vingi nchini , tafadhali usome gazeti la Tanzania Daima(Nondo za Nondo) J.tano .Nadhani utaelewa vizuri .

UVCCM chini yako imekuwa UVCCM ya matusi ,vurugu,kashfa.Jifunzeni siasa za ushawishi sio za mabavu,kashfa na chuki.Hata sisi siasa za ubabe na chuki tunaziweza ila tunataka mjifunze kutoka kwetu vijana wa vyama pinzani.

Heri James wewe na vijana wenzako wa UVCCM mnapaswa mshtakiwe sababu mmevunja sheria ya kanuni za makosa ya jinai kifungu cha 390,"Mtu yeyote ambaye anamshawishi au anamchochea mtu
mwingine kutenda kosa, atakuwa anatenda kosa bila kujali kwamba ushawishi au uchochezi huo hauna madhara"I390. "Any person who solicits or incites another to commit an offence
is guilty of a misdemeanour notwithstanding that the solicitation or
incitement has no effect."


Abdul Nondo.

abdulnondo10@gmail.com

Sent using Jamii Forums mobile app
Alijivunia Mjomba wake. Alidhani ataishi milele
 
Umerudi shule au bado unahangaika na mitaa? Unajiponza bureee! Maliza shule ndo uhangaike na siasa. Utakuwa kama akina Mnyika na Mbowe na soon tutaweka mahitaji ya digrii kuwa Mbunge.

Uliyoandika yote yameshaelezwa magazetu ya leo, yakieleza msimamo wa K/mkuu wa CCm juu ya hilo. Dogo unaleta tena mitandaoni, ili iweje?
Mkuu habari za siku nyingi Nadhani sasa umepata akili. Jiwe hayupo. 7baya yuko Jela
 
Back
Top Bottom