Kwako ephrahim kibonde katika jahazi radio- clouds fm

......KIBONDE ANATUKANA WATU HOVYO REDIONI, HATARI ILIYO MBELENI WALA HAONI, HANA AKILI KICHWANI, AU ANAVYOSAMBAZA NGOMA MAKUSUDI MITAANI ANADHANI HATUMUONI.....by JOSEPH MBILINYI.
 
kivalley ni janga la taifa, ni vizuri kumtetea anaekulipa lkn shurti utumie akili, yeye anatumia kisigino.
 
Mimi ni msikilizaji mzuri wa kipindi cha Jahazi na kama mfuatiliaji wa masuala naitegemea hii redio kwa taarifa na maarifa.
Nafanya kile waingereza wanasema "selective exposure" maana hakuna madhara kufanya hivyo kwa kuwa nina uwezo wa kupima masuala. Kama kuna miongoni mwetu hawaoioni Clouds kama chanzo cha taarifa na maarifa, na hawapendi kusikia wasiyoyapenda, waache kulalamika na wafanye kile kiitwacho "selective avoidance".
Kwa kuwa,daima, haiwezekani kuwa na mitazamo na fikra zinazoshabihiana, ni vema tujenge na tuimarishe utamaduni wa kuheshimu mawazo ya wananchi wenzetu.
 
Sasa hayapiti masaa mawili bila threads zinazomhusu Kobonde kuletwa hapa, Mods, nadhani mnapaswa kuunganisha nyuzi zote zinazomhusu huyu bwana!!!!! Badala ya kumshusha, mkizidi kumwongelea eleweni kuwa mnampaisha!
 
ingekuwa ni Baraza la wawakilishi wangetoka nje kama boti ingekuwa imezama ziwa nyasa/ ziwa Tanganyika? mbona JK aliendelea na Ziara yake mpaka Arusha na Rais wa Laiberia? Ni kweli Kibonde ni MSEMA CHOCHOTE (MC) na mtu asietumia akili kwenye mambo mengi but ktk hili no!
 
Wana JF,
Napenda Kumweleza kibonde mambo machache tuuu esp katika sakata la wabunge wa zanzibar kutoka nje ya Bunge. kwa maoni yake kibonde alivyo kuwa akijadiri baada ya wabunge kupata habari ya kuwa Meri Imezama.
Kibonde ulisema ati kuwa wabunge walio toka Bungeni walikuwa na "UTOVU WA NIDHAMU"
Kibonde ulipaswa kutambua kwanza wabunge wale sio wajinga au mambumbumbu. Mi ntakueleza hoja zangu. Kuzama kwa meri kulisikika kwa vyanzo vya habari vingini kuanzia saa 7 mchana, Nchi yetu hiii ina wizara kwanza moja ni nyeti sana Wizara ya mambo ya ndani (na inavitengo vyake vingi tuuuu police, JKT, Usalama nakadharika) pia kuna wizara ya uchukuzi na mawasiliano. na hizi wizara zina kazi zake muhimu za kuwajibika sana katika kulihudumia taifa hili.
Juzi Meri imezama mchana Taarifa za kwanza kabisa zapaswa kutoka wapi katika serikali hiiii? kama sio wizara hizi mbili mambo ya ndani na uchukuzi?

Point yangu ni nini:- Bungeni wabunge wamezipata taarifa mapema kama tetesi mwanzo ila kwa namna flani wao wakawa wameisha pata full details kuwa tukio ni harisi na sio tetesi tena. Na kumbuka hizi wizara mbili zenyewe zilikuwa kimya either makusudi au hazikuwa na taarifa kabisaaaaaa yaani kwangu nasema wana poor communication 100%, wizara ya mambo ya ndani means (ULINZI NA USALAMA) ni wizara nyeti sana katika kila Taifa duniani. sasa kama wabunge walipata taarifa na waziri husika yupo ndani ya bunge hajui au amekaidi tuu huoni hapo ni uzembe mkubwa ndani ya nchi hata ndani ya bunge? Au ni mpaka wabunge watoke nje ndio serikali ishtukeeeee kweli??? Hapo ni nani ana utovu wa nidhamu? Wabunge walio toka Nje? Wizara husika? Ni Muda gani ulipaswa hizi wizara mbili kujua kuwa chombo kimezama baharini?? na Taifa kujulishwa kuwa tume patwa na tatizo hiliii na lina fanyiwa kazi. Na hiyo hali ya kuwepo mawasiliano mabovu hadi wabunge wanaingia bungeni ile Jioni wengine hawajui kilichokuwa kimetokea hiyo ni aibu kubwa sana. Karibuni kwa kuchangia hoja wana JF

My Take:
Watangazaji mkiwapo hewani jaribuni sana kuchambua POSITIVE and NEGATIVE kwa topic husika msilalie upande mmoja tuuu, Bunge kama muhumili mkuu wa nchi ulipaswa kupata taarifa mapema sana at least 2hrs after the terrible incidence.
Na hakuna kitu kama Chain of Command ndani ya serikali hiiiii utaratibu huo watauwezea wapi waache kupiga siasa na ma deal yao ya kuwarubuni watanzania. Hizi life jackets zinauzwa bei juu kweli wakati zilipaswa uzwa bei rahisi sana ili watu wasiwe na tamaa ya kuziiba, wakuta zafungiwa kwa makufuli makubwa ya ajabu na minyororo khaaaaaa.

ulioeleza hapo juu ni mtazamo wako, na aliosema kibonde ni mtazamo wake kwa haki ileile. Cha msingi hapa ni wewe kuacha kusikiliza "Jahazi kama uliyyoacha kusikiliza vipindi vya watoto.
 
Majira ya jioni, mbali na waleti, huwa napenda kutembea na simu & headphones ili niwasikilize jamaa wa Jahazi.
Kwa mtazamo wangu, katika redio za Tanzania, sijaona kipindi kizuri kama Jahazi.
Nikiwa na stress na frustrations za kazini, nikiwasikiliza hawa ndugu zangu, huwa narejea katika hali yangu ya kawaida.
These guys ni wabunifu sana.
Hakuna haja ya kuwakatisha tamaa , tuwatie moyo.
 
Hivi ule mpango wao wa kuchangisha life jackets baada ya spice islanders uliishia wapi? Au ndo ilikuwa agenda ya cheap popularity. Tanzania kweli kuna mabo na vijimambo nilitegemea kampeni hiyo iwe kama ya vyandarua labda itasaidia. Wapi ruge?
 
Back
Top Bottom