G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Siku moja jioni mwaka 2015 mwezi wa tisa nikiwa na "frustrations zangu" ambazo wewe ndiye uliyezisababisha siku tatu kabla kwa hotuba matata uliyotoa pale Serena hotel niliwasha tv baada ya kutoka kazini.Kumbe familia walikuwa wametoka kuangalia Star tv hapo kabla nadhani kuna kipindi walikiita sijui "Lerato" Sina kumbukumbu vizuri! Kwa hakika kama siyo wao basi nisingekutana na star tv maana nilikuwa nikiichukia sana kutokana na propaganda zake chafu.
Hatimaye ile kuwasha tu tv nakutana na mwanasiasa makini asiyetetereka balozi Dr. Wilbrod Slaa. Mwanasiasa anayeamini kutokushirikiana na walaghai katika siasa. Ulikuwa ukimpamba kweli yule mtangazaji aliyekuwa akikuhoji kwa kumwambia kuwa anauliza maswali yenye mitego! Pale alipokuuliza swali kuhusu Lowassa kutaka kuwaachia Uamsho na Babu Seya unakumbuka ulijibu nini? Unakumbuka ulimpamba vipi Magufuli kuhusu hili? Kisha baadaye kuhusu jambo hilihili unakumbuka ulihitimisha vipi?
Ukishakumbuka hayo basi naomba uamue moja! Ama kuachana tena na wanasiasa walaghai ( Hapa naona ulishashindwa kwani ungeweza kufanya hivyo kitambo kidogo kutokana na mambo yanayoendelea) Au basi nakuomba uchutame maana u mtupu kwa sasa!
Wasalaam balozi Dr Wilbrod Slaa.