Kwako Dr. Slaa mwanasiasa makini unayeamini kutokutetereka

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
10,742
2,000
Siku moja jioni mwaka 2015 mwezi wa tisa nikiwa na "frustrations zangu" ambazo wewe ndiye uliyezisababisha siku tatu kabla kwa hotuba matata uliyotoa pale Serena hotel niliwasha tv baada ya kutoka kazini.Kumbe familia walikuwa wametoka kuangalia Star tv hapo kabla nadhani kuna kipindi walikiita sijui "Lerato" Sina kumbukumbu vizuri! Kwa hakika kama siyo wao basi nisingekutana na star tv maana nilikuwa nikiichukia sana kutokana na propaganda zake chafu.

Hatimaye ile kuwasha tu tv nakutana na mwanasiasa makini asiyetetereka balozi Dr. Wilbrod Slaa. Mwanasiasa anayeamini kutokushirikiana na walaghai katika siasa. Ulikuwa ukimpamba kweli yule mtangazaji aliyekuwa akikuhoji kwa kumwambia kuwa anauliza maswali yenye mitego! Pale alipokuuliza swali kuhusu Lowassa kutaka kuwaachia Uamsho na Babu Seya unakumbuka ulijibu nini? Unakumbuka ulimpamba vipi Magufuli kuhusu hili? Kisha baadaye kuhusu jambo hilihili unakumbuka ulihitimisha vipi?

Ukishakumbuka hayo basi naomba uamue moja! Ama kuachana tena na wanasiasa walaghai ( Hapa naona ulishashindwa kwani ungeweza kufanya hivyo kitambo kidogo kutokana na mambo yanayoendelea) Au basi nakuomba uchutame maana u mtupu kwa sasa!

Wasalaam balozi Dr Wilbrod Slaa.
 
leiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
619
1,000
Sio balozi Slaa pekee aliyeachwa solemba na uamuzi wa jemedari Magufuli bali wachumia tumbo wengi tu wa chama cha mafisi wanahaha watazisafisha vipi kauli zao. Kweli yatupasa kuwa na akiba ya maneno.
Katika kipindi hiki cha jeshi la mtu mmoja, hauwezi kubashiri ni kipi kitatokea kesho.........
Wapi comrade Shaka!!
 
lokomu

JF-Expert Member
Apr 25, 2013
4,933

naomba uibold hii
 
Masanja

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
4,149
2,000
The only thing predictable about JPM is his unpredictability.

I will be the last person to bet on anything when it comes to this man. Yeye mwenyewe alishasema bora sheria zivunjwe ilmradi mambo yaende. Yanaenda vipi? Ni kitendawili.

Kitu ambacho JPM (na hata Nyerere, aliyekuwa na good will ya wananchi), kimewashinda ni kutumia good will waliyokuwa nayo kwa wananchi kuunda na kusimamia mifumo bora na thabiti ambayo ingeweza kutuvusha popote pale (mf. katiba makini). Lakini sitashangaa JPM akiondoka tukarudi kule kule na hawa hawa wanaoshangilia leo ndo watakuwa mstari wa mbele kumponda huyu huyu JPM. Ofcourse mwisho wa siku kila mtu anataka mkono uende kinywani na watoto waende shule.

Kama wasemavyo wahenga. Mda ni mwamuzi mzuri sana!
 
GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,283
2,000
Nimecheka sana sana, Akiba ya maneno muhimu, Leo nimeamini ule mstari wa bibilia kuwa hakuna ajuae kesho, Watu hasa vijana wa lumumba waliropoka sana kuhusu ubakaji leo wamevuliwa nguo,
 
The Valiant

JF-Expert Member
Aug 16, 2017
2,829
2,000
Mimi kinachoniuma ni kwanini Mungu ametupa watanzania akili ndogo kiasi hiki
Ivi kweli in the midst of very serious national issues tunapoteza muda wetu mwingi kujadili events...kweli?
Ivi watanzania mbona akili zetu ndogo hivi? Kweli tunapoteza muda kujadili dr shika..sijui babu seya?

Mungu aisaidie sana nchi hii.

Kizazi kilichopo sasa ni cha ajabu sana..akili mb 8..hakitunzi kumbukumbu

Na watawala tunawapata walio reflection ya sisi..kwa hio na wao wataendelea kututengenezea matukio tu kila siku.

Mwishoni kama taifa tunasahau kujadili issues.

Naionea huruma sana nchi yangu
 
mzado

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
933
1,000
The only thing predictable about JPM is his unpredictability.

I will be the last person to bet on anything when it comes to this man. Yeye mwenyewe alishasema bora sheria zivunjwe ilmradi mambo yaende. Yanaenda vipi? Ni kitendawili.

Kitu ambacho JPM (na hata Nyerere, aliyekuwa na good will ya wananchi), kimewashinda ni kutumia good will waliyokuwa nayo kwa wananchi kuunda na kusimamia mifumo bora na thabiti ambayo ingeweza kutuvusha popote pale (mf. katiba makini). Lakini sitashangaa JPM akiondoka tukarudi kule kule na hawa hawa wanaoshangilia leo ndo watakuwa mstari wa mbele kumponda huyu huyu JPM. Ofcourse mwisho wa siku kila mtu anataka mkono uende kinywani na watoto waende shule.

Kama wasemavyo wahenga. Mda ni mwamuzi mzuri sana!
Hakika umenena mkuu
 
barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
29,770
2,000
Mimi kinachoniuma ni kwanini Mungu ametupa watanzania akili ndogo kiasi hiki
Ivi kweli in the midst of very serious national issues tunapoteza muda wetu mwingi kujadili events...kweli?
Ivi watanzania mbona akili zetu ndogo hivi? Kweli tunapoteza muda kujadili dr shika..sijui babu seya?

Mungu aisaidie sana nchi hii.

Kizazi kilichopo sasa ni cha ajabu sana..akili mb 8..hakitunzi kumbukumbu

Na watawala tunawapata walio reflection ya sisi..kwa hio na wao wataendelea kututengenezea matukio tu kila siku.

Mwishoni kama taifa tunasahau kujadili issues.

Naionea huruma sana nchi yangu
Na wewe unajadili hicho hicho ila hujui kama unajadili hicho, wee ni mmoja wa hao watanzania wajinga.
 
Ngushi

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
9,082
2,000
Akiba ya maneno ni muhimu mno kuliko kitu chochote!
Teknolojia na Mungu ni vitu vya kuogopwa sana!
 
mliberali

JF-Expert Member
Jul 13, 2012
8,392
2,000
Siku moja jioni mwaka 2015 mwezi wa tisa nikiwa na "frustrations zangu" ambazo wewe ndiye uliyezisababisha siku tatu kabla kwa hotuba matata uliyotoa pale Serena hotel niliwasha tv baada ya kutoka kazini.Kumbe familia walikuwa wametoka kuangalia Star tv hapo kabla nadhani kuna kipindi walikiita sijui "Lerato" Sina kumbukumbu vizuri! Kwa hakika kama siyo wao basi nisingekutana na star tv maana nilikuwa nikiichukia sana kutokana na propaganda zake chafu.

Hatimaye ile kuwasha tu tv nakutana na mwanasiasa makini asiyetetereka balozi Dr. Wilbrod Slaa. Mwanasiasa anayeamini kutokushirikiana na walaghai katika siasa. Ulikuwa ukimpamba kweli yule mtangazaji aliyekuwa akikuhoji kwa kumwambia kuwa anauliza maswali yenye mitego! Pale alipokuuliza swali kuhusu Lowassa kutaka kuwaachia Uamsho na Babu Seya unakumbuka ulijibu nini? Unakumbuka ulimpamba vipi Magufuli kuhusu hili? Kisha baadaye kuhusu jambo hilihili unakumbuka ulihitimisha vipi?

Ukishakumbuka hayo basi naomba uamue moja! Ama kuachana tena na wanasiasa walaghai ( Hapa naona ulishashindwa kwani ungeweza kufanya hivyo kitambo kidogo kutokana na mambo yanayoendelea) Au basi nakuomba uchutame maana u mtupu kwa sasa!

Wasalaam balozi Dr Wilbrod Slaa.
amelazimishwa avae kijani LA sivyo hakuna kuapishwa
 
mliberali

JF-Expert Member
Jul 13, 2012
8,392
2,000
Wapinzani bhana, leo imewauma tena JPM kuwasamehe hawa?? Si kamuiga lowassa.
dogo watu wenye akili tupo mbali na huu upuuzi siju babu Seya, siju takataka gani?, hayo ni mambo ya kipuuzi hata kama yashabikiwa na Ccm / Chadema
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom