Kwako Dr Kigwangalla: Sahihi yako hatujaiona

Atakapokuja kwenye hoja yoyote hapa JF lazma tumhoji kuhusu hili la Kamanda Zitto.
Hata kama halihusiani na kilichoko mezani.
 
Binfsi nimem_PM kumualert kuhusu hii thread, na kumpa link ya uzi.
He cannot claim unawaress of the thread.
Simply ignored it.
He is haunted from within.
 
Wanabodi,

Naomba niweke sawa hili Ombi.
Dr Kigwamgalla, wanabodi wamekwazika kutokana na uwepo wa makundi matatu
Kundi 1. Linaamini mambo yanaenda hovyo, kuna ulazima wa kusaini karatasi kulinusuru taifa

Kundi 2. Linaamini hayo ni mambo ya kawaida, utaratibu unaotumika si mzuri, kuna uonevu.
Linaani kuwa ni 'move' ya kisisasa na halipo tayari kukiabisha chama

Kundi 3. Hili ni la 'popo' ambalo ni gumu sana kulijua linasimamia nini
Ni kundi la wabeba vipaza sauti, wakali wa ufisadi n.k

Mhe Dr, wanabodi kwa kutambua ushiriki wako hapa JF na misimamo yako ya nyuma, wanakuomba uwaeleze wewe una maoni gani kuhusu sakata hili linalojulikana kama ' Karatasi ya Zitto'

Ni muhimu ukaja kuweka wazi kwasababu wewe ni miongoni mwa vijana wanotegemewa kuwa mwanga mpya na kupigiwa debe kuwa zama hizi ni za ujana. Ni miongoni mwa wale wanaopigania mabadiliko kwa kumbu kumbu zetu, na wanaotaka kuwakomboa vijana wenzako. Ni miongoni mwa wale wanaokerwa na ufisadi.

Unachaguo la kuja au kutokomea, lakini niamini 'this will damage your credibility significantly and erode your moral authority for long time. It will haunt you with no platform'

'Mwenye neno na asema au akae kimya daima'
 
kigangwala si uje tu ujibu tuhuma,unafki mbaya sana katika maisha haya.nakumbuka siku ile ulipokua na zitto pale mlimani tv nilikukubali sana na kuona kua kumbe ndani ya ccm wapo majembe,kumbe duh!
 
Wanabidi,
Dr Kigwangalla amekuwa mstari Wa mbele katika kupinga ufisadi akianzia kudai mikataba ya Madini, kuwatetea madaktari wenzake. Leo kajificha wapi haonekani kupinga madudu haya ya serikali na wala hatukuona jina lake katika sole saini 70 zilizotakiwa na Zitto. Je ni kweli Ana uchungu na nchi hii au ni dramas?

Tayari wameshampa mgao wake kama Lemberi....
 
:sad: Ulitaka afuate matakwa ya chama gani ambacho hakijamwajiri, tumia akili ya ziada kwa hili :drum:
 
Mshindi wa tatu kura za maoni kuonekana na Chama kama ndiye anayefaa kuliko mshindi wa kwanza Hussein Bashe na mshindi wa pili Lucas Seleli atapata wapi ujasiri wa kupingana na serikali ya chama chake?
 
Mie nilishasema huyu bwana hayuko consistent.

Halafu pia sahihi hizi si kama injili, kwamba utamhubiria mtu mpaka akubali. Kama mtu hakubaliani na hoja hakubaliani nayo, jua hivyo katika vitabu vyako.

Kigs hana jipya ni wale wale tu, mie simshangai. Nawashangaa nyie mnaomshangaa.
 
Acha ubishoo, jibu kwanini hukusign??

Na je hustahili hujumu ya wananchi??

Huenda anajipanga kujibu, ngoja tuvute subira. Mwenzao zainab kawawa hajaweka sahihi yake na siku chache baadae anamwaga machozi kuwa ccm ya sasa sio ile ya enzi za baba yake na Nyerere!
 
.....mwacheni huyu, ana kesi ya jinai ya Uchochezi katika mahakama ya Wilaya ya NZEGA, akithubutu tu anapatikana na hatia kufungwa
 
Amesha nyamazishwa huyo njaa ilikuwa inamsumbua sasa ameshiba kasahau alikotoka kuwa kuna njaa na wananchi waliompeleka hapo mjengoni wana njaa.

Kamanda Lema na kimbunga chako tafadhali usisahau kupita jimboni kwa huyu mnafki dr. kigwangalla anajejifanya kukerwa na mikataba mibovu ila anafurahia serikali mbovu.
 
Ndugu zangu wanabodi,

Nimeamua kuja kujibu kama ambavyo mngependa nifanye. Siyo kwamba nimekimbia JF, la hasha. Siwezi kukimbia na wala sina sababu ya kufanya hivyo. Ni kwamba gadget yangu ninayotumia kwa mawasiliano ilipata mushkeri na nikawa nalazimika kutumia kompyuta na bahati mbaya sana kwa jinsi nilivyokuwa bize na ujenzi wa Taifa nilijikuta nakosa muda wa kukaa kuanza ku-surf. Nisamehewe kwa hilo.

Mimi sijawahi kuwa mnafiki, at least kwa alama tatu za mnafiki kama tunavyofundishwa sisi waislamu. Kwa faida ya mjadala huu, niseme alama zenyewe. Moja ni kuwa akitoa ahadi hatekelezi. Mbili, ni akiaminiwa anahalifu na tatu, akizungumza husema uongo. Namshukuru Mungu sina hata moja ya alama hizi na hivyo kushindwa mtihani wa kuwa 'mnafiki'. Ungeniita mnafiki kama nisingekuwa tayari kutoa maelezo ya maamuzi yangu, ama kama ningewasaliti CCM na kupeleka siri za huku kule, ama kama ningeahidi kuunga mkono hoja hiyo kisha nikakimbia. Leo hii mimi niko chama kimoja tu, CCM, na nitafanya mambo yanayokubalika ndani ya CCM. Siku nikihamia CHADEMA/CUF/NCCR basi nitafanya ya huko bila kusaliti kule na kurudisha CCM ama kupeleka kokote kule kinyume na utaratibu. Huo ndiyo msimamo wa ukweli na siyo unafiki.

Kuna uwezekano wa kuwa na tafsiri tofauti kutokana na pre-conceptions zetu vichwani, siwezi kulizuia hilo hata kidogo. Kwa kuwa ninakalia kiti cha uwakilishi, nina-feel ninawajibika kwenu kutoa maelezo ya msimamo wangu kwenye hili, na wala sintomumunya maneno.

Kwanza, hoja yenyewe siikubali. Kwa sababu ninaamini serikali ya Chama Changu (CCM) haijashindwa kufanya kazi ya watanzania kiasi cha kung'olewa madarakani kwa namna hiyo. Pili, naamini na ninakubali, na kwa hakika ninakerwa na baadhi ya watu waliopewa dhamana za kuongoza baadhi ya ofisi nyeti za umma wametuangusha watanzania, na hivyo naunga mkono hoja ya kutaka kuwatoa hawa. Mhe. Zitto Kabwe (MB) alipokuwa akijumuisha hoja yake, alitaka serikali iwawajibishe baadhi ya mawaziri na watendaji wakuu wa Wizara na Mashirika ya umma, na akasema kama serikali haikufanya hivyo kufikia J3 iliyofuata basi sisi (Bunge) tuna uwezo na WM na kwamba atapitisha karatasi ya kukusanyia saini 70 ili kukidhi matakwa ya kikanuni ya kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na WM; kwa tafsiri yangu ni kwamba Mhe. Mbunge alilenga kuweka presha kwa serikali, kuitaka iwajibike kwa kuwawajibisha mawaziri hao (watano) kama alivyowataja yeye. Kwanza mwanzoni nilielewa hivyo. Baadaye jinsi ilivyopokelewa na wadau mbalimbali nikaona kama hoja inahama sasa na kwamba si mawaziri hao watano wenye tuhuma mbalimbali, ni PM na kwa maana hiyo ni serikali yote Bungeni! Hili mimi siliungi mkono na silikubali. Nasema wazi hivyo kwa sababu, mimi nina imani na WM, nina imani na Rais - aliyemchagua WM, na nina imani na Mawaziri wengine wengi wazuri tu kwenye serikali hii, na msimamo wangu huu uko wazi sana tu.

Mbili, sioni sababu ya kuiingiza nchi kwenye wasiwasi wa kiutawala kiasi hiki. Na kwa kuwa wabunge wa CCM kwenye party caucus tulikuwa tayari tumeishaambiwa kwamba kuna mawaziri wameamua kujiuzulu wenyewe (tena siyo wale watano, ni wanane kabisa) kutokana na tuhuma hizo na presha kutoka kwa wabunge wa CCM na wengine, sikuona sababu ya mimi kusaini hoja ya Zitto (ambayo kikanuni ilikuwa imekosewa - kitendo kilichonidhihirishia wazi kwamba hakuwa na u-seriousness wa kutaka kweli kumuondoa WM bali ni baadhi ya mawaziri, sema alichomeka tu hiyo kauli ili kutia presha zaidi!). Zaidi ya hapo, ninaamini hoja hiyo ni nzito na kimsingi, kwa sasa, imegeuka kuwa ni mchezo wa kisiasa na media na haitofika popote! Kama Mhe. Mbunge Zitto alikuwa na nia ya dhati ya kumuondoa WM asingekurupuka kiasi kile, angewashirikisha watu wengi zaidi, hususani wabunge wa CCM, na kimkakati zaidi angewapa wabunge wa CCM walioibua hoja hizo za kuwataka mawaziri wang'olewe na hapo angefanikisha malengo ya kumuondoa WM na serikali yake Bungeni. Kwa namna ilivyo hawezi kupata support ya wabunge wa CCM na kwa kuwa sisi ndiyo majority, hoja hiyo haitopita - na hii itaturudisha kule kule kwenye nilichokisema kule twitter kwamba hoja hii ni ......politically right but technically flawed!

Jamani, hoja ya kumuondoa WM madarakani siyo kitu kidogo, siyo kitu cha mchezo, ni lazima ujipange. Ukweli ni kwamba rafiki yangu Mhe. Zitto hakujipanga kuifanikisha (bila shaka yeye mwenyewe analielewa hili vizuri - he is smarter than this, I know him!)

Tatu, msisahau kitu kimoja cha muhimu kabisa. Kwamba, mimi ni Mbunge kutokea CCM na kama walivyo wengi wenzangu hatukusaini kwa sababu hatuwezi kuiangusha serikali ya CCM kwa hoja inayoletwa na Mbunge wa Kambi ya Upinzani! Mbunge wa Chama Tawala kuamua kuiangusha serikali ya chama chako ni sawa na kuamua kukata tawi la mti uliokalia, kwa vyovyote vile utaanguka nalo! Simple logic! Mfumo wa Bunge letu ni wa Westminster, na hivyo kuna kambi ya Upinzani (yenye interest ya kutaka kuiangusha serikali inayotawala) na Kambi ya Serikali (ambayo ina interest ya kutaka kuilinda serikali yake). Kwa maana hiyo sisi wabunge wa CCM tuna jukumu la kuilinda Serikali inayopatikana kutokana na sisi kuwa majority. Serikali ni lazima i-enjoy majority status ndani ya Bunge ili nchi itawalike kwa amani na utulivu, japokuwa haimaanishi kuruhusu ubadhirifu na ndiyo maana kwenye Party Caucus wabunge wana nguvu na fursa ya kusema chochote dhidi ya serikali ya Chama Chao. Kuna wengine wanataka Bunge liwe Bunge huru (ama 'An Indipendent Power House') disregarding political opinions/inclinations/affiliations na serikali iwe serikali, hii haiwezekani kwa katiba tuliyonayo leo. Tubadilishieni kwanza katiba na mfumo wa kufanya kazi ndipo mtutake tufanye hayo mnayoyatamani.

Nadhani nimejiweka wazi bila unafiki, sasa tujadili kwa hoja siyo kwa hisia na matusi kama hatukwenda shule vile.

Wakatabahu,
HK.
 
Wewe kweli ni msukule!!

Kwa hiyo kila kinachosemwa na viongozi wako ni sahihi...

Nimeamini wewe ni zaidi ya kunguru!!

hapa ndipo huwa naona umuhimu wa Bashe kuwa mbunge wa Nzega,2015!
 
Back
Top Bottom