Kinoamiguu
JF-Expert Member
- Nov 29, 2018
- 10,526
- 13,013
Bwana David Silinde popote ulipo.
Hongera kwa kuula. Umeula uwaziri. Mpe Salaam ndugu waitara. Mwambie wanawaukonga na wapenda mabadiliko wote wanakumbuka michango na kujitolea kwai hata akawa mbunge. Kumbe leo amerejea nyumbani nae sasa ni Waziri ameulamba.
Bwana silinde asubuhi nilikusikia ukidanganya bungeni. Sijui kwa faida ya nani? Uliulizwa swali juu ya upungufu wa wataalamu wa afya na dawa. Hilo ni tatizo sugu kwenye hospitali za umma. Ukajibu kwa mbwembwe kwamba "Luna watumishi wasio waaminifu wanaiba dawa" sijui kwamba huwa mnafanya Tafiti au majibu ya kisiasa tu.
Ukweli ni kwamba hakuna dawa zinaibiwa ila dawa hazipelekwi za kutosha huo ndio ukweli. Serikali ya ccm imeshindwa kutenga bajeti ya kutosha ya kununulia dawa na vitendanishi badala yake wanajisifia kujenga Majengo wanayoyaita Vito vya " afya" kituo cha afya bila dawa. Katika kukabiliana na wizi huu wa dawa kama upo. Walikuja na mpango wa kuzipiga nembo za MSD dawa zote za serikali!
Je ile nembo haisaidii kuendelea kuwaita?