Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Basi fahamu haya:
Mwanamke aliyezaa huhamishia mapenzi kwa mwanaye. Hali huwa hivyo hata ndani ya ndoa, kiasi kwamba ndoa nyingi hupoteza mvuto pale tu mtoto anapozaliwa. Kwako wewe kijana unayetaka kujitwika mabomu uoe single mother.
Mwanamke anatakiwa aolewe katika ubikira wake ili mwanamume kujisikia kwamba kweli amepata mtu mwaminifu. Lakini kama hata hilo halikutosha kukushawishi, usithubutu kuoa mwanamke ambaye ni single mama, labda kama una uvumilivu usiopimika. Yako mambo kadhaa ambayo yanamfanya single mama asiwe sehemu ya mtarajiwa wa ndoa.
1. Single mama wengi ni matokeo ya uzinzi ama uasherati. Binti anapojiingiza kwenye mapenzi kabla ya ndoa kwa kigezo cha kutafuta kuolewa ni dalili mbaya hata kama ataolewa kweli. Hii inaonyesha kuwa ana udhaifu kwenye eneo la ndoa kiasi kwamba yuko tayari kuutumia mwili wake kama rushwa ili kufanikisha ndoa. Hii haitofautiani na mwanamke aliye ndani ama nje ya ndoa kutumia tigo yake kama kishawishi cha kumshika mwanamume. Unapotumia ngono kama sehemu ya ushawishi, ama kama silaha ya kumteka mwanamume ujue kwamba unaondoa thamani yako na kuingia kwenye kundi la makahaba. Ni kweli uchi wa mwanamke ndio silaha yake kwenye mahusiano, lakini si kwa kuigawa hovyo, bali kwa kuwanyima wanaoitamani ili apatikane mwenye nia thabiti ya ndoa.
Inapotokea binti kajiingiza kwenye mapenzi mpaka kupata mimba, tayari keshapata muunganiko mwingine na mwanamume aliyempa mimba hiyo, tayari wameunganishwa na mtoto huyo, ingawa bado mwanamume aliona huyu mwanamke hafai kuwa mke, alikiwa anamtumia tu kukidhi kiu yake mpaka pale atakapompata mtu sahihi. Sasa wewe ni nani hata ukajiingize kuoa mwanamke wa aina hii?
2. Single mama hawezi kukupenda kwa jinsi ulivyo, bali kutakuwa na sharti la mtoto. Kwamba iwapo utamtunza mtoto kama single mama atakavyo basi utapewa mapenzi matamu. Ni ukweli usiopingika kuwa mwanamke apatapo mtoto mapenzi yote huhamia huko, hivyo wewe jiandae kuwa chaguo la pili kwake. Haya sio mapenzi na ujue tu kuwa huwezi kuwa na amani kamwe.
3. Mtoto si wako. Hata kama utampenda na kumhudumia kwa namna yoyote ile, ukweli utabaki kuwa huyo si mwanao, sio damu yako. Ni kwamba umejitwika jukumu la kumhudumia mtoto wa mwanaume mwenzako ambaye ndiye ataendelea kutambulika kama baba mzazi. Siku akikua ataanza kumtafuta aliyechangia mbegu mpaka akaja dunuani, sio aliyechangia ugali. Ikitokea mmeachana na single mama, ujue ndio mwisho wa kuonana na mwanao mpenzi uliyekuwa ukimtunza kwa nguvu zako zote.
4. Utatumia nguvu kubwa kulilinda penzi. Ili ujihakikishie kuwa single mama anatulizana na wewe, utahitaji kuishi maisha ya kumfurahisha yeye, kumpa atakacho ili asije akamkumbuka mume wake wa kwanza. Namna pekee ya kumfurahisha ni kuhakikisha mtoto wa mwanamume mwenzako anapata maatunzo mazuri, nguo nzuri, elimu nzuri n.k. Utalazimika kuwa karibu naye kuliko hata baba mzazi anavyokuwa, yote haya ni kutafuta kumfurahisha single mama. Utaishi maisha ya kujipendekeza, yenye stress nyingi.
5. Huna sauti juu ya mtoto. Hata kama utataka umchujue mtoto huyu kuwa mwanao kamili, umpe malezi halisi ya mzazi, kuna mahali utakwama tu. Huwezi kumwadabisha kwa mikono miwili, lazima mmoja utakuwa nyuma na mwingine utakuwa mbele. Mara zote utakaa ukijiuliza, labda nikimfanya hivi mama yake atadhani namchukia, jamii nayo itanifikiria vingine. Utajikuta wewe mwenyewe unajiwekea mipaka hata kabla pilato hajakuhukumu kwa kuvuka mstari!! Pigo kubwa zaidi ni pale single mama atakapokutamkia kuwa unamtendea hivyo kwa sababu mtoto sio wako. Hapo utabaki kama mjinga fulani aliyepigwa bumbuwazi asijue aukabili vipi ukweli huu mchungu.
6. Chanzo cha vurugu kwenye familia. Hata ikitokea mmezaa watoto wengine, bado mapenzi hayawezi kuwa sawa. Single mama wana kawaida ya kuwaandalia mazingira watoto wa baba wengine tofauti hao wa baba waliye naye wakati huo. Hufanya hivyo kwa hofu kuwa watoto hawa mara nyingi hawana urrithi kwa baba aliyewalea. Hii huleta mgawanyiko mkubwa kwenye familia kiasi cha watoto wenyewe kuchukiana. Hata ndugu wa mwanamume hawawezi kamwe kumhesabu mtoto huyu kama sehemu ya familia kwa sabubu sio damu yao na anao ukoo mwingine kabisa. Hawezi kujitambulisha kwa jina la baba wa kambo kwa sabubu hana muunganiko wowote naye. Hata ikitokea baba mlezi amekufa, ukoo wake hauwezi kumhesabu mtoto huyu kama sehemu ya urithi. Tunajifunza kwa wanyama wengine pia kama simba, ambapo anapoinuka dume mwingine kuongoza majike, huua watoto wote àliowakuta kisha huanza upya kusaka watoto wake. Sasa sisi hatuwezi kuua, bali tunaweza kuepuka taabu hii kwa kutokuoa mwanamke mwenye watoto.
7. Mume wa kwanza ana nafasi ya kuendelea kumtafuna single mama atakavyo. Kwa kawaida mwanamke akishazaa na mwanamume, ule muunganiko huwa haufi. Tayari ni mzazi mwenza na hana cha khmficha tena, hivyo kupasha kiporo ni jambo la kawaida tu. Pia mama atataka mtoto amjue baba yake halisi kwa ajili ya siku zijazo, hivyo hawezi kujiweka mbali na mzazi mwenzake. Sasa mzazi mwenza ni juu yake kuamua kuendelea kumla ama la, kwani hakuna kutongozana tena, ni kupanga miadi tu na kukutana kuserebuka. Kidume wewe utageuzwa baba mlishi huku haki nyingine zote zikielekezwa kwa mwenye mwanaye.
Ukweli ni kuwa single mama anapopata mume, focus yake sio ndoa bali ni malezi ya mwanaye. Anataka uhakika tu kuwa mwanae ataishi na atapata matunzo bora ili siku za usoni aje kumsaidia yeye.
Ewe kijana, usijiingize kwenye mtego utakaoharibu maisha yako. Tafuta bikira atakayefunga kiapo nawe, achana na wanawake waliozaa hovyo kwa kukosa mwelekeo.
Hapa sijazungumza juu ya walioolewa kisha waume zao kufariki, kwani kwao hawa yako mambo mengi pia nyuma ya pazia ya kuchunguza.
Najua hii ni ngumu kumeza na ukweli unauma sana lakini hii ni kweli tupu ila hapo kwenye kumpata bikra ni adimu siku hizi bora ungesema yeyote yule ambaye bado hajawahi kupata mimba kabisa na utamjua tu ipo namna.....
 
Najua hii ni ngumu kumeza na ukweli unauma sana lakini hii ni kweli tupu ila hapo kwenye kumpata bikra ni adimu siku hizi bora ungesema yeyote yule ambaye bado hajawahi kupata mimba kabisa na utamjua tu ipo namna.....
Nakuelewa mkuu, tatizo la ambaye hajapata mimba ni kuwa atakuwa na attachment nyingine pia. Kwanza kuna aliyemtoa bikira, pili wako waliomsugua vizuri. Itakuwa mkipishana kidogo tu, anakwenda kutafuta faraja kwa washika dau. Utachapiwa mapaka basi, kwani atajiona hana cha kuwaficha kwani walishamfunua uchi wake.

Unataka kuwa salama? Tafuta bikira, ni dalili njema kwamba anajiheshimu na ana nafasi kubwa kukuheshimu oia
 
Pambafff kwani huwa wanazini na miti ama na wanaume? Una hakika gani kwamba baba yako alimuoa mama yako akiwa bikra? Muwe na staha basi wakati mwingine maana kuna leo na kesho binti yako anadungwa mimba na utageuka mshenga ili aolewe kulinda heshima ya familia!
Hoja ya kijinga kabisa hii. Kuwa na mtoto anayetumia madawa ya kulevya sio sababu ya kukaa kimya kulinda staha. Ni ujinga uliopitiloza. Habari ya baba yangu kuiingiza humu ni dalili ya wewe kuwa uliyeharibika akili, hufai hata kuwa baba wa familia.

Hapa hatupaki mafuta kwa mgongo wa chupa, ni ukweli mtimilifu, no matter what! Kama umeumia kaa kimya, nina uhakika wako vijana wawili ama watatu watajifunza neno hapa.
 
Singo maza masikini. Wanaandamwa kila siku. Mimi nadhani, kama ilivyo hata kwetu wanaume, ni suala la tabia ya mtu na mtu na siyo haki kuwarundika wote kwenye kundi moja. Nafahamu ndugu na jamaa ambao wameoa singo mazas na ndoa zao zina unafuu sana kuliko hata zile za wale waliooa "watakatifu".

Japo baadhi ya hoja zako zinakubalika katika ujumla wa kimajumuisho na zina misingi ya kisayansi (mf. Akina mama kuhamishia mapenzi kwa watoto wao), katika kiwango cha mtu mmoja mmoja zinapwaya. Binadamu ni kiumbe tata mno na tabia zake huwezi kuziundia fomyula. Kama kuna mapenzi ya kweli, amani, maelewano na hofu ya Mungu sioni sababu ya maana ya kutooa singo maza.
Nakuelewa mkuu, exception cases zipo kwa kila kitu. Ila kwa ujumla wake ukweli ni huo, huwezi khniambia kuwa ni suala la tabia kwani kuzaa nje ya ndoa tayari ni kiashiria cha aina ya tabia. Sasa wako waliojifunza kwa MOTO, yaani baada ya kupitia msoto kufuatia kosa hilo, hizo ndio exception cases, lakini wengi ndio hao hata leo tunawasikia wakitaka mpaka kuanzisha UMOJA wao. By the way hao watakatifu unaowasema hivyo sidhani kama unajua maana. Binti anmepaswa kuolewa akiwa bikra, thats all.
 
Fine, ni mtazamo wako. Pia waweza kuwa ni ushamba wako, hao wengi umewafanyia assessment lini? Narudia,
FACT: kuoa single mama ni kuoa mke wa mwanaume mwenzio
Mbona uko mkali hivi kamanda? Mada ni yako. Waache watu watoe mawazo yao kwa uhuru. Sasa tena inakuwa kama vile ni ugomvi. Kwa nini tusisemeshane na kujadiliana kwa staha?
 
Single mother anapaswa kuolewa na single father au Mgane au mwanaume wa makamo au mzee. Kamwe kijana usijaribu kuchukua single mother, utakuwa unabahatisha mnoo, na huenda ukateseka sana.

Single mother hawana shida, shida ni vijana wanaokimbilia kuwaoa single mother wakati vigezo na masharti hawawezi kuvizingatia.
Ndio kusema single mother huolewa kwa kutimiziwa masharti yao
 
Ukisoma kwa makini hizo sababu ziko kwa pande zote mbili!

Wimbi la hawa singo mama/baba ni kubwa sana! Sababu ni nini haswa?! Kubali kataa chanzo ni malezi, vijana hawana hofu tenaa zamani ilikuwa ukizaa bila kuolewa ni aibu kwa mzazi kijiji kizima kinanyoosha kidole kwenye hiyo familia!

Mtoto wa kiume ajitambue, na mtoto wa kike ajithamini! Hawa tunaowaita singo mama ni binadamu pia, wana mapungufu yao ila kitendo cha wao kuamua kuzaa na sio kutoa mimba ni ujasiri!

Tumebaki tukiwanyooshea vidole singo mama na kusahau kuwaasa watoto wetu wa kiume!!
Kila mzazi asimamie nafasi yake kwenye malezi!
 
Hoja ya kijinga kabisa hii. Kuwa na mtoto anayetumia madawa ya kulevya sio sababu ya kukaa kimya kulinda staha. Ni ujinga uliopitiloza. Habari ya baba yangu kuiingiza humu ni dalili ya wewe kuwa uliyeharibika akili, hufai hata kuwa baba wa familia.

Hapa hatupaki mafuta kwa mgongo wa chupa, ni ukweli mtimilifu, no matter what! Kama umeumia kaa kimya, nina uhakika wako vijana wawili ama watatu watajifunza neno hapa.
Nina mbwa wangu ambaye umemzidi umri ila ana busara na akili kukuzidi wewe. Rudia bandiko lako mstari kwa mstari kisha mpe mtu unayedhani umemzidi maarifa asipokuambia ulichoandika ni kampeni ya kutaka wanawake ambao wana watoto wasiolewe tena. Imagine mtu ni single mother simply kwa kuwa alibakwa ama mimba za utotoni then akutane na kampeni yako hii mshuuuu...pambaffff
 
Hata usemeje. Aliekuzalisha ndio akuoe. Kama baba wa mtoto yupo hai huyo single maza ni wa kukaa nae mbali sana. Hata salam usimpe
Nina mbwa wangu ambaye umemzidi umri ila ana busara na akili kukuzidi wewe. Rudia bandiko lako mstari kwa mstari kisha mpe mtu unayedhani umemzidi maarifa asipokuambia ulichoandika ni kampeni ya kutaka wanawake ambao wana watoto wasiolewe tena. Imagine mtu ni single mother simply kwa kuwa alibakwa ama mimba za utotoni then akutane na kampeni yako hii mshuuuu...pambaffff
 
Back
Top Bottom