Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Kila la heri kamanda. Kama ni mwanamke anayejielewa utakuwa umeokota lulu na mtaishi maisha mema sana. Single mother akiwa amekata dhamira kabisa ya kutulia, kulinda na kuendeleza familia yake huwa hawatetereki. Wanajua walikopitia. Dharau walizozipata. Na hawataki kurudi huko tena.
Kila la heri !!!
 
Kila la heri kamanda. Kama ni mwanamke anayejielewa utakuwa umeokota lulu na mtaishi maisha mema sana. Single mother akiwa amekata dhamira kabisa ya kutulia, kulinda na kuendeleza familia yake huwa hawatetereki. Wanajua walikopitia. Dharau walizozipata. Na hawataki kurudi huko tena.
Kila la heri !!!
shukrani
 
nimeanguka kwa single mother, nimejiandaa kukabiliana na changmaoto zote zinazosemwa humu. kwakuwa la kuambiwa changanya na akili yako, nimeamua kuendelea.....maneno yapo humu, vitendo mtaani. wengi humu, tena wengine ni wapostaji wa kila siku wa threads zinazoponda single mothers, wanadeal nao vizuri tu; ni eidha wake zao au wapenzi wao. nikiwa muislam, najua ndoa hainibani sana.....asipotia akili, sioni tabu kuivunja hata kesho.

nimemzidi kipato maana hana kazi wakati mimi ni muajiriwa. yeye amenizidi, kwa mbali tu, akili ya ujasiriamali....amenizidi sana. mipango yake inaonekana na ipo dhahiri (wakati yangu ninapoilinganisha kimyakimya ipo dhaifu kweli dhidi yake).....nataka kuvuna hiki kipaji, km sio mimi basi mtoto wangu (tukijaaliwa kuzaa), km ambavyo nae najua anataka kufaidika nami. aliolewa lkn mume ukicheche ulimsumbua baada ya kupata mtoto wao huyo....akamtelekeza na harakati za kudaiana talaka zikafanyika.

nimepeleka barua, wananijibu kuwa wanataka laki nne. PUMBAVU!!! nimewaambia wapunguze hadi nusu km hawataki basi. natoka na nipo maeneo ya pwani, huku ndoa ni ibada zaidi kuliko fursa....ukizingatia na umama wake, naona km nataka kupigwa. nimewapa hadi kesho kuamua hilo.

nilileta thread ya kukimbiwa na binti na kwenda kuolewa na tajiri flani,...ameolewa kwa laki mbili na nusu tu!

karibuni.....
Hao wanao kejeliwa kuwa hawafai yaani ni wanawake Safi tu Kama wanawake wengine.Huo unaoitwa u single mother sijui nini ni kejeli tu zinazo lenga kuwadhalilisha,lakini hazina uhusiano wowote na uhalisia.Wapo waliopo kwenye mahusiano na mahusiano yao Yana afya ya kutosha kuliko hata hao ambao sio ma single mother.
 
Pole sana... ila laki nne siyo mbaya sababu...

She is a single mom and you are a single further... wote mna watoto tayari...

Kila la kheri...


Cc: mahondaw
 
Basi fahamu haya:

Mwanamke aliyezaa huhamishia mapenzi kwa mwanaye. Hali huwa hivyo hata ndani ya ndoa, kiasi kwamba ndoa nyingi hupoteza mvuto pale tu mtoto anapozaliwa. Kwako wewe kijana unayetaka kujitwika mabomu uoe single mother.

Mwanamke anatakiwa aolewe katika ubikira wake ili mwanamume kujisikia kwamba kweli amepata mtu mwaminifu. Lakini kama hata hilo halikutosha kukushawishi, usithubutu kuoa mwanamke ambaye ni single mama, labda kama una uvumilivu usiopimika. Yako mambo kadhaa ambayo yanamfanya single mama asiwe sehemu ya mtarajiwa wa ndoa.

1. Single mama wengi ni matokeo ya uzinzi ama uasherati. Binti anapojiingiza kwenye mapenzi kabla ya ndoa kwa kigezo cha kutafuta kuolewa ni dalili mbaya hata kama ataolewa kweli. Hii inaonyesha kuwa ana udhaifu kwenye eneo la ndoa kiasi kwamba yuko tayari kuutumia mwili wake kama rushwa ili kufanikisha ndoa. Hii haitofautiani na mwanamke aliye ndani ama nje ya ndoa kutumia tigo yake kama kishawishi cha kumshika mwanamume. Unapotumia ngono kama sehemu ya ushawishi, ama kama silaha ya kumteka mwanamume ujue kwamba unaondoa thamani yako na kuingia kwenye kundi la makahaba. Ni kweli uchi wa mwanamke ndio silaha yake kwenye mahusiano, lakini si kwa kuigawa hovyo, bali kwa kuwanyima wanaoitamani ili apatikane mwenye nia thabiti ya ndoa.

Inapotokea binti kajiingiza kwenye mapenzi mpaka kupata mimba, tayari keshapata muunganiko mwingine na mwanamume aliyempa mimba hiyo, tayari wameunganishwa na mtoto huyo, ingawa bado mwanamume aliona huyu mwanamke hafai kuwa mke, alikiwa anamtumia tu kukidhi kiu yake mpaka pale atakapompata mtu sahihi. Sasa wewe ni nani hata ukajiingize kuoa mwanamke wa aina hii?

2. Single mama hawezi kukupenda kwa jinsi ulivyo, bali kutakuwa na sharti la mtoto. Kwamba iwapo utamtunza mtoto kama single mama atakavyo basi utapewa mapenzi matamu. Ni ukweli usiopingika kuwa mwanamke apatapo mtoto mapenzi yote huhamia huko, hivyo wewe jiandae kuwa chaguo la pili kwake. Haya sio mapenzi na ujue tu kuwa huwezi kuwa na amani kamwe.

3. Mtoto si wako. Hata kama utampenda na kumhudumia kwa namna yoyote ile, ukweli utabaki kuwa huyo si mwanao, sio damu yako. Ni kwamba umejitwika jukumu la kumhudumia mtoto wa mwanaume mwenzako ambaye ndiye ataendelea kutambulika kama baba mzazi. Siku akikua ataanza kumtafuta aliyechangia mbegu mpaka akaja dunuani, sio aliyechangia ugali. Ikitokea mmeachana na single mama, ujue ndio mwisho wa kuonana na mwanao mpenzi uliyekuwa ukimtunza kwa nguvu zako zote.

4. Utatumia nguvu kubwa kulilinda penzi. Ili ujihakikishie kuwa single mama anatulizana na wewe, utahitaji kuishi maisha ya kumfurahisha yeye, kumpa atakacho ili asije akamkumbuka mume wake wa kwanza. Namna pekee ya kumfurahisha ni kuhakikisha mtoto wa mwanamume mwenzako anapata maatunzo mazuri, nguo nzuri, elimu nzuri n.k. Utalazimika kuwa karibu naye kuliko hata baba mzazi anavyokuwa, yote haya ni kutafuta kumfurahisha single mama. Utaishi maisha ya kujipendekeza, yenye stress nyingi.

5. Huna sauti juu ya mtoto. Hata kama utataka umchujue mtoto huyu kuwa mwanao kamili, umpe malezi halisi ya mzazi, kuna mahali utakwama tu. Huwezi kumwadabisha kwa mikono miwili, lazima mmoja utakuwa nyuma na mwingine utakuwa mbele. Mara zote utakaa ukijiuliza, labda nikimfanya hivi mama yake atadhani namchukia, jamii nayo itanifikiria vingine. Utajikuta wewe mwenyewe unajiwekea mipaka hata kabla pilato hajakuhukumu kwa kuvuka mstari!! Pigo kubwa zaidi ni pale single mama atakapokutamkia kuwa unamtendea hivyo kwa sababu mtoto sio wako. Hapo utabaki kama mjinga fulani aliyepigwa bumbuwazi asijue aukabili vipi ukweli huu mchungu.

6. Chanzo cha vurugu kwenye familia. Hata ikitokea mmezaa watoto wengine, bado mapenzi hayawezi kuwa sawa. Single mama wana kawaida ya kuwaandalia mazingira watoto wa baba wengine tofauti hao wa baba waliye naye wakati huo. Hufanya hivyo kwa hofu kuwa watoto hawa mara nyingi hawana urrithi kwa baba aliyewalea. Hii huleta mgawanyiko mkubwa kwenye familia kiasi cha watoto wenyewe kuchukiana. Hata ndugu wa mwanamume hawawezi kamwe kumhesabu mtoto huyu kama sehemu ya familia kwa sabubu sio damu yao na anao ukoo mwingine kabisa. Hawezi kujitambulisha kwa jina la baba wa kambo kwa sabubu hana muunganiko wowote naye. Hata ikitokea baba mlezi amekufa, ukoo wake hauwezi kumhesabu mtoto huyu kama sehemu ya urithi. Tunajifunza kwa wanyama wengine pia kama simba, ambapo anapoinuka dume mwingine kuongoza majike, huua watoto wote àliowakuta kisha huanza upya kusaka watoto wake. Sasa sisi hatuwezi kuua, bali tunaweza kuepuka taabu hii kwa kutokuoa mwanamke mwenye watoto.

7. Mume wa kwanza ana nafasi ya kuendelea kumtafuna single mama atakavyo. Kwa kawaida mwanamke akishazaa na mwanamume, ule muunganiko huwa haufi. Tayari ni mzazi mwenza na hana cha khmficha tena, hivyo kupasha kiporo ni jambo la kawaida tu. Pia mama atataka mtoto amjue baba yake halisi kwa ajili ya siku zijazo, hivyo hawezi kujiweka mbali na mzazi mwenzake. Sasa mzazi mwenza ni juu yake kuamua kuendelea kumla ama la, kwani hakuna kutongozana tena, ni kupanga miadi tu na kukutana kuserebuka. Kidume wewe utageuzwa baba mlishi huku haki nyingine zote zikielekezwa kwa mwenye mwanaye.

Ukweli ni kuwa single mama anapopata mume, focus yake sio ndoa bali ni malezi ya mwanaye. Anataka uhakika tu kuwa mwanae ataishi na atapata matunzo bora ili siku za usoni aje kumsaidia yeye.

Ewe kijana, usijiingize kwenye mtego utakaoharibu maisha yako. Tafuta bikira atakayefunga kiapo nawe, achana na wanawake waliozaa hovyo kwa kukosa mwelekeo.

Hapa sijazungumza juu ya walioolewa kisha waume zao kufariki, kwani kwao hawa yako mambo mengi pia nyuma ya pazia ya kuchunguza.
 
Naunga mkono hoja
Screenshot_20190906-165503.jpeg
 
Kwani huwa wanazini na miti ama na wanaume? Una hakika gani kwamba baba yako alimuoa mama yako akiwa bikra? Muwe na staha basi wakati mwingine maana kuna leo na kesho binti yako anadungwa mimba na utageuka mshenga ili aolewe kulinda heshima ya familia!
 
Singo maza masikini. Wanaandamwa kila siku. Mimi nadhani, kama ilivyo hata kwetu wanaume, ni suala la tabia ya mtu na mtu na siyo haki kuwarundika wote kwenye kundi moja. Nafahamu ndugu na jamaa ambao wameoa singo mazas na ndoa zao zina unafuu sana kuliko hata zile za wale waliooa "watakatifu".

Japo baadhi ya hoja zako zinakubalika katika ujumla wa kimajumuisho na zina misingi ya kisayansi (mf. Akina mama kuhamishia mapenzi kwa watoto wao), katika kiwango cha mtu mmoja mmoja zinapwaya. Binadamu ni kiumbe tata mno na tabia zake huwezi kuziundia fomyula. Kama kuna mapenzi ya kweli, amani, maelewano na hofu ya Mungu sioni sababu ya maana ya kutooa singo maza.

Na hao mabikra wa kuoa siku hizi utawapata wapi?
 
Single mother anapaswa kuolewa na single father au Mgane au mwanaume wa makamo au mzee. Kamwe kijana usijaribu kuchukua single mother, utakuwa unabahatisha mnoo, na huenda ukateseka sana.

Single mother hawana shida, shida ni vijana wanaokimbilia kuwaoa single mother wakati vigezo na masharti hawawezi kuvizingatia.
 
Back
Top Bottom