Kwahiyo unataka kuoa single mama?

Nyenyere

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
10,631
Points
2,000
Nyenyere

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
10,631 2,000
Basi fahamu haya:

Mwanamke aliyezaa huhamishia mapenzi kwa mwanaye. Hali huwa hivyo hata ndani ya ndoa, kiasi kwamba ndoa nyingi hupoteza mvuto pale tu mtoto anapozaliwa. Kwako wewe kijana unayetaka kujitwika mabomu uoe single mother.

Mwanamke anatakiwa aolewe katika ubikira wake ili mwanamume kujisikia kwamba kweli amepata mtu mwaminifu. Lakini kama hata hilo halikutosha kukushawishi, usithubutu kuoa mwanamke ambaye ni single mama, labda kama una uvumilivu usiopimika. Yako mambo kadhaa ambayo yanamfanya single mama asiwe sehemu ya mtarajiwa wa ndoa.

1. Single mama wengi ni matokeo ya uzinzi ama uasherati. Binti anapojiingiza kwenye mapenzi kabla ya ndoa kwa kigezo cha kutafuta kuolewa ni dalili mbaya hata kama ataolewa kweli. Hii inaonyesha kuwa ana udhaifu kwenye eneo la ndoa kiasi kwamba yuko tayari kuutumia mwili wake kama rushwa ili kufanikisha ndoa. Hii haitofautiani na mwanamke aliye ndani ama nje ya ndoa kutumia tigo yake kama kishawishi cha kumshika mwanamume. Unapotumia ngono kama sehemu ya ushawishi, ama kama silaha ya kumteka mwanamume ujue kwamba unaondoa thamani yako na kuingia kwenye kundi la makahaba. Ni kweli uchi wa mwanamke ndio silaha yake kwenye mahusiano, lakini si kwa kuigawa hovyo, bali kwa kuwanyima wanaoitamani ili apatikane mwenye nia thabiti ya ndoa.

Inapotokea binti kajiingiza kwenye mapenzi mpaka kupata mimba, tayari keshapata muunganiko mwingine na mwanamume aliyempa mimba hiyo, tayari wameunganishwa na mtoto huyo, ingawa bado mwanamume aliona huyu mwanamke hafai kuwa mke, alikiwa anamtumia tu kukidhi kiu yake mpaka pale atakapompata mtu sahihi. Sasa wewe ni nani hata ukajiingize kuoa mwanamke wa aina hii?

2. Single mama hawezi kukupenda kwa jinsi ulivyo, bali kutakuwa na sharti la mtoto. Kwamba iwapo utamtunza mtoto kama single mama atakavyo basi utapewa mapenzi matamu. Ni ukweli usiopingika kuwa mwanamke apatapo mtoto mapenzi yote huhamia huko, hivyo wewe jiandae kuwa chaguo la pili kwake. Haya sio mapenzi na ujue tu kuwa huwezi kuwa na amani kamwe.

3. Mtoto si wako. Hata kama utampenda na kumhudumia kwa namna yoyote ile, ukweli utabaki kuwa huyo si mwanao, sio damu yako. Ni kwamba umejitwika jukumu la kumhudumia mtoto wa mwanaume mwenzako ambaye ndiye ataendelea kutambulika kama baba mzazi. Siku akikua ataanza kumtafuta aliyechangia mbegu mpaka akaja dunuani, sio aliyechangia ugali. Ikitokea mmeachana na single mama, ujue ndio mwisho wa kuonana na mwanao mpenzi uliyekuwa ukimtunza kwa nguvu zako zote.

4. Utatumia nguvu kubwa kulilinda penzi. Ili ujihakikishie kuwa single mama anatulizana na wewe, utahitaji kuishi maisha ya kumfurahisha yeye, kumpa atakacho ili asije akamkumbuka mume wake wa kwanza. Namna pekee ya kumfurahisha ni kuhakikisha mtoto wa mwanamume mwenzako anapata maatunzo mazuri, nguo nzuri, elimu nzuri n.k. Utalazimika kuwa karibu naye kuliko hata baba mzazi anavyokuwa, yote haya ni kutafuta kumfurahisha single mama. Utaishi maisha ya kujipendekeza, yenye stress nyingi.

5. Huna sauti juu ya mtoto. Hata kama utataka umchujue mtoto huyu kuwa mwanao kamili, umpe malezi halisi ya mzazi, kuna mahali utakwama tu. Huwezi kumwadabisha kwa mikono miwili, lazima mmoja utakuwa nyuma na mwingine utakuwa mbele. Mara zote utakaa ukijiuliza, labda nikimfanya hivi mama yake atadhani namchukia, jamii nayo itanifikiria vingine. Utajikuta wewe mwenyewe unajiwekea mipaka hata kabla pilato hajakuhukumu kwa kuvuka mstari!! Pigo kubwa zaidi ni pale single mama atakapokutamkia kuwa unamtendea hivyo kwa sababu mtoto sio wako. Hapo utabaki kama mjinga fulani aliyepigwa bumbuwazi asijue aukabili vipi ukweli huu mchungu.

6. Chanzo cha vurugu kwenye familia. Hata ikitokea mmezaa watoto wengine, bado mapenzi hayawezi kuwa sawa. Single mama wana kawaida ya kuwaandalia mazingira watoto wa baba wengine tofauti hao wa baba waliye naye wakati huo. Hufanya hivyo kwa hofu kuwa watoto hawa mara nyingi hawana urrithi kwa baba aliyewalea. Hii huleta mgawanyiko mkubwa kwenye familia kiasi cha watoto wenyewe kuchukiana. Hata ndugu wa mwanamume hawawezi kamwe kumhesabu mtoto huyu kama sehemu ya familia kwa sabubu sio damu yao na anao ukoo mwingine kabisa. Hawezi kujitambulisha kwa jina la baba wa kambo kwa sabubu hana muunganiko wowote naye. Hata ikitokea baba mlezi amekufa, ukoo wake hauwezi kumhesabu mtoto huyu kama sehemu ya urithi. Tunajifunza kwa wanyama wengine pia kama simba, ambapo anapoinuka dume mwingine kuongoza majike, huua watoto wote àliowakuta kisha huanza upya kusaka watoto wake. Sasa sisi hatuwezi kuua, bali tunaweza kuepuka taabu hii kwa kutokuoa mwanamke mwenye watoto.

7. Mume wa kwanza ana nafasi ya kuendelea kumtafuna single mama atakavyo. Kwa kawaida mwanamke akishazaa na mwanamume, ule muunganiko huwa haufi. Tayari ni mzazi mwenza na hana cha khmficha tena, hivyo kupasha kiporo ni jambo la kawaida tu. Pia mama atataka mtoto amjue baba yake halisi kwa ajili ya siku zijazo, hivyo hawezi kujiweka mbali na mzazi mwenzake. Sasa mzazi mwenza ni juu yake kuamua kuendelea kumla ama la, kwani hakuna kutongozana tena, ni kupanga miadi tu na kukutana kuserebuka. Kidume wewe utageuzwa baba mlishi huku haki nyingine zote zikielekezwa kwa mwenye mwanaye.

Ukweli ni kuwa single mama anapopata mume, focus yake sio ndoa bali ni malezi ya mwanaye. Anataka uhakika tu kuwa mwanae ataishi na atapata matunzo bora ili siku za usoni aje kumsaidia yeye.

Ewe kijana, usijiingize kwenye mtego utakaoharibu maisha yako. Tafuta bikira atakayefunga kiapo nawe, achana na wanawake waliozaa hovyo kwa kukosa mwelekeo.

Hapa sijazungumza juu ya walioolewa kisha waume zao kufariki, kwani kwao hawa yako mambo mengi pia nyuma ya pazia ya kuchunguza.
 
Karma

Karma

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Messages
8,967
Points
2,000
Karma

Karma

JF-Expert Member
Joined May 20, 2019
8,967 2,000
Umekazania hapo kwenye bikira haya hebu niambie mwanamke na mwanaume wakifanya uzinzi au uasherati halafu wakaamua kutubu wakasamehewa na kumrudia muumba hiyo bikira aliyoipoteza mwanamke isiporudi anapata madhara gani??

Halafu kwahiyo mwanaume kuwa juu ya mwanamke maana yake anatakiwa kumkandamiza na kumdharau?? Kwamba ili mwanaume uonekane uko juu na mwanamke aonekana yuko chini unatakiwa kumkandamiza na kumdharau?? Yaani sisi kupinga kukandamizwa na kudharauliwa na ninyi ndiyo maana yake tunataka usawa??
 
Karma

Karma

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Messages
8,967
Points
2,000
Karma

Karma

JF-Expert Member
Joined May 20, 2019
8,967 2,000
Sasa ni wanaume wangapi wanafanya hivyo kwa dunia ya sasa??
Kwa hiyo akitoa uchi ndio haachwi? Mwanamume mwenye nia ya kuoa hata akinyimwa papuchi atapoigana kumpata huyo binti kwa gharama yoyote! Hiyo gharama inapaswa kuwa ndoa
 
Nyenyere

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
10,631
Points
2,000
Nyenyere

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
10,631 2,000
tatizo unaongea theory
Tatizo wewe ni kizazi cha kisasa. Hujui historia na sababu ya mabadiliko ya sasa. Lakini tangu zamani ilikuwa hivyo. Basi sasa nimeelewa kumbe wewe natetea unachokiona sasa na si ilivyokuwa tangu mwanzo.
 
lyasi

lyasi

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2015
Messages
303
Points
500
lyasi

lyasi

JF-Expert Member
Joined Sep 23, 2015
303 500
Ungesoma mpaka mwisho usingeandika hivi. Ndoa sio taasisi ya huruma, ila suala la wajane soma mwishoni utaona.
Mkuu umenena kweli Tena ukweli mchungu ambao kwa vijana wa era hii inayoongoza kwa mivunjiko ya ndoa Kila kukichwa vigumu kukuelewa. Umenikumbusha wosia niliopewa wakati nipo kwenye mchakato wa kuoa "Ndoa siyo taasisi ya huruma Wala si sehemu ya kufanyiana hisani, ikiwa unaona kasoro zisizoendana na wewe usizipuuze, achana nae hata Kama alikutolea Figo wakati was kupigania uhai wako"
 
rikiboy

rikiboy

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Messages
11,419
Points
2,000
rikiboy

rikiboy

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2017
11,419 2,000
Tatizo wewe ni kizazi cha kisasa. Hujui historia na sababu ya mabadiliko ya sasa. Lakini tangu zamani ilikuwa hivyo. Basi sasa nimeelewa kumbe wewe natetea unachokiona sasa na si ilivyokuwa tangu mwanzo.
Sasa wewe unaongea miaka ya 80 huko??? Hata pono hazikuwepoo... vishawishi vya kingono hakuna kabisaa.. Siku hizi haya mavazi na mavyakula ya ovyoo ukichanganya na Technology ya simu si ndo balaa... Mihemkoo juu muda wotee zama hizi sio zile mkuu...
 
Karma

Karma

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Messages
8,967
Points
2,000
Karma

Karma

JF-Expert Member
Joined May 20, 2019
8,967 2,000
kipi kinaingiza mimba,kukataa au kukubali??
Kwahiyo anayeomba ngono hana makosa ila anayekubali ngono ndiyo ana makosa??

Maandiko yanasema uzinzi na uasherati ni dhambi kwa jinsia ZOTE MBILI sasa inakuwaje anayeomba uzinzi na uasherati asiwe na makosa ila anayekubali uzinzi na uasherati ndiyo awe na makosa??
 
Nyenyere

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
10,631
Points
2,000
Nyenyere

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
10,631 2,000
Na mimi ndiyo nashangaa hapo...
Huwa anaandika mada nzuri ila ya leo amechemsha!
Ninaposema ndoa sio taasisi ya huruma ninamaasha hivi: huwezi kusema mtu aonewe huruma yaani aolewe kwa kumhurumia kwa madhara aliyojisababishia mwenyewe. Achana na single mothers, wapo waliopata maradhi kwa mfano, huwezi kusema waonewe huruma waolewe. Ndoa ni taasisi yenye vigezo, na kimojawapo mke awe bikira ingawa
wanaume siku hizi wameamua kuvaa miwani. Lakini matokeo yake tunayaona sasa, ndoa zimegeuka kaa la moto.

Kwa hiyo msitafute huruma bali mjiweke kwenye mazingira ya kustahili. Ni neno gumu lakini ndio ukweli wenyewe.

Kuhusu kuchemsha ni mtazamo wako tu, hebu pitia thread yote uone ni wangapi wanapinga ujishangae.
 
lyasi

lyasi

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2015
Messages
303
Points
500
lyasi

lyasi

JF-Expert Member
Joined Sep 23, 2015
303 500
Nina mbwa wangu ambaye umemzidi umri ila ana busara na akili kukuzidi wewe. Rudia bandiko lako mstari kwa mstari kisha mpe mtu unayedhani umemzidi maarifa asipokuambia ulichoandika ni kampeni ya kutaka wanawake ambao wana watoto wasiolewe tena. Imagine mtu ni single mother simply kwa kuwa alibakwa ama mimba za utotoni then akutane na kampeni yako hii mshuuuu...pambaffff
Huna hoja na Kama unayo basi unatatizo katika uwasolishaji wako na Kama vyote hivyo viko sawa basi mazingira na malezi yamekuharibu na kukufanya usiwe na staha Wala heshima juu ya mawazo ya wengine isipokuwa kukashifu kwa lugha zinye ukakasi.
 
Nyenyere

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
10,631
Points
2,000
Nyenyere

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
10,631 2,000
Ta

Tatizo wanaoingia jf wengi ni above20yrs,wadogo ndiyo mnawadanganya hasa kwa ubichi wao wakipata mimba zenu mnawalalamikia huku....

Suala la kujitunza ni muhimu ila litasaidiwa na wazazi na walezi kuwapa watoto elimu ya jinsia waweze kujitambua....

Kuna wasichana hawajui bikira ni nini na inafaida gani zaidi ya kujua ukifanya unapata mimba,so atajitahidi asipate mimba tu,hapo bado hajajitunza anatumika kama kawaida...
Kosa ni letu wazazi. Ndio maana tunaleta humu tukumbushane wajibu wetu kwa watoto
 
rikiboy

rikiboy

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Messages
11,419
Points
2,000
rikiboy

rikiboy

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2017
11,419 2,000
Ninaposema ndoa sio taasisi ya huruma ninamaasha hivi: huwezi kusema mtu aonewe huruma yaani aolewe kwa kumhurumia kwa madhara aliyojisababishia mwenyewe. Achana na single mothers, wapo waliopata maradhi kwa mfano, huwezi kusema waonewe huruma waolewe. Ndoa ni taasisi yenye vigezo, na kimojawapo mke awe bikira ingawa
wanaume siku hizi wameamua kuvaa miwani. Lakini matokeo yake tunayaona sasa, ndoa zimegeuka kaa la moto.

Kwa hiyo msitafute huruma bali mjiweke kwenye mazingira ya kustahili. Ni neno gumu lakini ndio ukweli wenyewe.

Kuhusu kuchemsha ni mtazamo wako tu, hebu pitia thread yote uone ni wangapi wanapinga ujishangae.
Pambana na kutafuta Bikra mkuu wapo wengi lakini NDOA sio lelemamaa...!! Oa bikra alafu mdomoo hautuliii...Oa bikra kichwani kweupee... Ndoa sio suala la Ubikra ni more than that
 
Karma

Karma

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Messages
8,967
Points
2,000
Karma

Karma

JF-Expert Member
Joined May 20, 2019
8,967 2,000
Haya je wanawake wakijitunza wanaume mtaweza kuvumilia kutokufanya ngono hadi mtakapofikia umri wa kuoa na kutaka kuoa??
Ninaposema ndoa sio taasisi ya huruma ninamaasha hivi: huwezi kusema mtu aonewe huruma yaani aolewe kwa kumhurumia kwa madhara aliyojisababishia mwenyewe. Achana na single mothers, wapo waliopata maradhi kwa mfano, huwezi kusema waonewe huruma waolewe. Ndoa ni taasisi yenye vigezo, na kimojawapo mke awe bikira ingawa
wanaume siku hizi wameamua kuvaa miwani. Lakini matokeo yake tunayaona sasa, ndoa zimegeuka kaa la moto.

Kwa hiyo msitafute huruma bali mjiweke kwenye mazingira ya kustahili. Ni neno gumu lakini ndio ukweli wenyewe.

Kuhusu kuchemsha ni mtazamo wako tu, hebu pitia thread yote uone ni wangapi wanapinga ujishangae.
 
K

Koriee

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2018
Messages
319
Points
500
K

Koriee

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2018
319 500

Leo umeteleza! Huwa napenda mada zako sana...
Sina cha kujishangaa la sivyo tutaanza kubishana,ukweli ni kwamba siyo kila siku utakuwa sahihi!
 
Karma

Karma

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Messages
8,967
Points
2,000
Karma

Karma

JF-Expert Member
Joined May 20, 2019
8,967 2,000
Kwahiyo wazazi wanatakiwa wawachunge watoto wao kike tu ila wa kiume wawalee kuja kuwa wahuni kwa sababu tu wao hawapati madhara??
Kosa ni letu wazazi. Ndio maana tunaleta humu tukumbushane wajibu wetu kwa watoto
 
Nyenyere

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
10,631
Points
2,000
Nyenyere

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
10,631 2,000
Umekazania hapo kwenye bikira haya hebu niambie mwanamke na mwanaume wakifanya uzinzi au uasherati halafu wakaamua kutubu wakasamehewa na kumrudia muumba hiyo bikira aliyoipoteza mwanamke isiporudi anapata madhara gani??

Halafu kwahiyo mwanaume kuwa juu ya mwanamke maana yake anatakiwa kumkandamiza na kumdharau?? Kwamba ili mwanaume uonekane uko juu na mwanamke aonekana yuko chini unatakiwa kumkandamiza na kumdharau?? Yaani sisi kupinga kukandamizwa na kudharauliwa na ninyi ndiyo maana yake tunataka usawa??
1. Bikira ni kiungo muhimu kwenye agano LA ndoa. Kwenye mila za nyuma binti alitakiwa kuwa bikira ndio aolewe, damu ya ubikra wake ndio ilikuwa ushahidi. Hata Biblia imeagiza hivyo, hicho kiwambo hakikuwekwa kama show tu.

2. Elezea kuhusu kumkandamiza na kumdharau. Ni wapi nimesema hayo? Kwa mwanamke aliyepea katika tamaduni za kigeni mamlaka ya mume kwake ni unyanyasaji. Nasikitika kusema wewe ni mmoja was wanawske was aina hiyo.
 
Forum statistics

Threads 1,342,618
Members 514,728
Posts 32,757,659
Top