Kwahiyo unataka kuoa single mama?

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
10,702
Points
2,000

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
10,702 2,000
Basi fahamu haya:

Mwanamke aliyezaa huhamishia mapenzi kwa mwanaye. Hali huwa hivyo hata ndani ya ndoa, kiasi kwamba ndoa nyingi hupoteza mvuto pale tu mtoto anapozaliwa. Kwako wewe kijana unayetaka kujitwika mabomu uoe single mother.

Mwanamke anatakiwa aolewe katika ubikira wake ili mwanamume kujisikia kwamba kweli amepata mtu mwaminifu. Lakini kama hata hilo halikutosha kukushawishi, usithubutu kuoa mwanamke ambaye ni single mama, labda kama una uvumilivu usiopimika. Yako mambo kadhaa ambayo yanamfanya single mama asiwe sehemu ya mtarajiwa wa ndoa.

1. Single mama wengi ni matokeo ya uzinzi ama uasherati. Binti anapojiingiza kwenye mapenzi kabla ya ndoa kwa kigezo cha kutafuta kuolewa ni dalili mbaya hata kama ataolewa kweli. Hii inaonyesha kuwa ana udhaifu kwenye eneo la ndoa kiasi kwamba yuko tayari kuutumia mwili wake kama rushwa ili kufanikisha ndoa. Hii haitofautiani na mwanamke aliye ndani ama nje ya ndoa kutumia tigo yake kama kishawishi cha kumshika mwanamume. Unapotumia ngono kama sehemu ya ushawishi, ama kama silaha ya kumteka mwanamume ujue kwamba unaondoa thamani yako na kuingia kwenye kundi la makahaba. Ni kweli uchi wa mwanamke ndio silaha yake kwenye mahusiano, lakini si kwa kuigawa hovyo, bali kwa kuwanyima wanaoitamani ili apatikane mwenye nia thabiti ya ndoa.

Inapotokea binti kajiingiza kwenye mapenzi mpaka kupata mimba, tayari keshapata muunganiko mwingine na mwanamume aliyempa mimba hiyo, tayari wameunganishwa na mtoto huyo, ingawa bado mwanamume aliona huyu mwanamke hafai kuwa mke, alikiwa anamtumia tu kukidhi kiu yake mpaka pale atakapompata mtu sahihi. Sasa wewe ni nani hata ukajiingize kuoa mwanamke wa aina hii?

2. Single mama hawezi kukupenda kwa jinsi ulivyo, bali kutakuwa na sharti la mtoto. Kwamba iwapo utamtunza mtoto kama single mama atakavyo basi utapewa mapenzi matamu. Ni ukweli usiopingika kuwa mwanamke apatapo mtoto mapenzi yote huhamia huko, hivyo wewe jiandae kuwa chaguo la pili kwake. Haya sio mapenzi na ujue tu kuwa huwezi kuwa na amani kamwe.

3. Mtoto si wako. Hata kama utampenda na kumhudumia kwa namna yoyote ile, ukweli utabaki kuwa huyo si mwanao, sio damu yako. Ni kwamba umejitwika jukumu la kumhudumia mtoto wa mwanaume mwenzako ambaye ndiye ataendelea kutambulika kama baba mzazi. Siku akikua ataanza kumtafuta aliyechangia mbegu mpaka akaja dunuani, sio aliyechangia ugali. Ikitokea mmeachana na single mama, ujue ndio mwisho wa kuonana na mwanao mpenzi uliyekuwa ukimtunza kwa nguvu zako zote.

4. Utatumia nguvu kubwa kulilinda penzi. Ili ujihakikishie kuwa single mama anatulizana na wewe, utahitaji kuishi maisha ya kumfurahisha yeye, kumpa atakacho ili asije akamkumbuka mume wake wa kwanza. Namna pekee ya kumfurahisha ni kuhakikisha mtoto wa mwanamume mwenzako anapata maatunzo mazuri, nguo nzuri, elimu nzuri n.k. Utalazimika kuwa karibu naye kuliko hata baba mzazi anavyokuwa, yote haya ni kutafuta kumfurahisha single mama. Utaishi maisha ya kujipendekeza, yenye stress nyingi.

5. Huna sauti juu ya mtoto. Hata kama utataka umchujue mtoto huyu kuwa mwanao kamili, umpe malezi halisi ya mzazi, kuna mahali utakwama tu. Huwezi kumwadabisha kwa mikono miwili, lazima mmoja utakuwa nyuma na mwingine utakuwa mbele. Mara zote utakaa ukijiuliza, labda nikimfanya hivi mama yake atadhani namchukia, jamii nayo itanifikiria vingine. Utajikuta wewe mwenyewe unajiwekea mipaka hata kabla pilato hajakuhukumu kwa kuvuka mstari!! Pigo kubwa zaidi ni pale single mama atakapokutamkia kuwa unamtendea hivyo kwa sababu mtoto sio wako. Hapo utabaki kama mjinga fulani aliyepigwa bumbuwazi asijue aukabili vipi ukweli huu mchungu.

6. Chanzo cha vurugu kwenye familia. Hata ikitokea mmezaa watoto wengine, bado mapenzi hayawezi kuwa sawa. Single mama wana kawaida ya kuwaandalia mazingira watoto wa baba wengine tofauti hao wa baba waliye naye wakati huo. Hufanya hivyo kwa hofu kuwa watoto hawa mara nyingi hawana urrithi kwa baba aliyewalea. Hii huleta mgawanyiko mkubwa kwenye familia kiasi cha watoto wenyewe kuchukiana. Hata ndugu wa mwanamume hawawezi kamwe kumhesabu mtoto huyu kama sehemu ya familia kwa sabubu sio damu yao na anao ukoo mwingine kabisa. Hawezi kujitambulisha kwa jina la baba wa kambo kwa sabubu hana muunganiko wowote naye. Hata ikitokea baba mlezi amekufa, ukoo wake hauwezi kumhesabu mtoto huyu kama sehemu ya urithi. Tunajifunza kwa wanyama wengine pia kama simba, ambapo anapoinuka dume mwingine kuongoza majike, huua watoto wote àliowakuta kisha huanza upya kusaka watoto wake. Sasa sisi hatuwezi kuua, bali tunaweza kuepuka taabu hii kwa kutokuoa mwanamke mwenye watoto.

7. Mume wa kwanza ana nafasi ya kuendelea kumtafuna single mama atakavyo. Kwa kawaida mwanamke akishazaa na mwanamume, ule muunganiko huwa haufi. Tayari ni mzazi mwenza na hana cha khmficha tena, hivyo kupasha kiporo ni jambo la kawaida tu. Pia mama atataka mtoto amjue baba yake halisi kwa ajili ya siku zijazo, hivyo hawezi kujiweka mbali na mzazi mwenzake. Sasa mzazi mwenza ni juu yake kuamua kuendelea kumla ama la, kwani hakuna kutongozana tena, ni kupanga miadi tu na kukutana kuserebuka. Kidume wewe utageuzwa baba mlishi huku haki nyingine zote zikielekezwa kwa mwenye mwanaye.

Ukweli ni kuwa single mama anapopata mume, focus yake sio ndoa bali ni malezi ya mwanaye. Anataka uhakika tu kuwa mwanae ataishi na atapata matunzo bora ili siku za usoni aje kumsaidia yeye.

Ewe kijana, usijiingize kwenye mtego utakaoharibu maisha yako. Tafuta bikira atakayefunga kiapo nawe, achana na wanawake waliozaa hovyo kwa kukosa mwelekeo.

Hapa sijazungumza juu ya walioolewa kisha waume zao kufariki, kwani kwao hawa yako mambo mengi pia nyuma ya pazia ya kuchunguza.
 

Karma

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Messages
9,165
Points
2,000

Karma

JF-Expert Member
Joined May 20, 2019
9,165 2,000
Huo ni mtazamo wa jamii lakini mtazamo wa Mungu ni kwamba mwanaume anayezalisha nje ya ndoa na mwanamke anayezalishwa nje ya ndoa wote ni wazinzi na waasherati hauwezi kusema eti mwanamke tu ndiyo ana makosa maana hata mwanaume naye anahusika na ni kwanini jamii iwe na mtazamo huo wa kumhukumu mwanamke tu??
Kitendo cha mwanamke kuzaa nje ya ndoa tena bila utaratibu au mpango maalumu unaoeleweka anahesabika kuwa ni mwanamke asiyekuwa anajitunza.Mwanamke huyo anahesabika kuwa ni mzinzi, asiye NA msimamo, dira wala mwelekeo, hajui kutunza unyumba ndio maana ameweza kutapeliwa kimapenzi kirahisi, hivyo upo uwezekano mkubwa wa kuweza kutapeliwa tena zaidi NA zaidi ktk maisha yake yote, ni mwanamke asiyefaa, n.k., n.k.

Suluhisho pekee ni KUJITUNZA, USIZAE NJE YA NDOA
 

Karma

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Messages
9,165
Points
2,000

Karma

JF-Expert Member
Joined May 20, 2019
9,165 2,000
Kwahiyo mwanaume anayeomba ngono hana makosa ila mwanamke anayekubali ngono ndiyo ana makosa siyo??
KWA nini ukubali kushawishiwa kizembe?Kudanganywa au kurubumiwa kirahisi tena kizembe kabisa kama mtoto mdogo wa umri wa miaka mitano???
Mwanamke kukubali kudanganywa kizembe ni udhaifu mkubwa NA tena inaonyesha wazi kuwa hauna msimamo ktk maisha yako, mama huduma NA matokeo yake ni kuzalishwa nje ya ndoa na hatimaye kudhalilishwa KWA kuitwa majina mabaya yasiyofaa ktk jamii.

Shikeni msimamo, hakuna ndoa hakuna kuzaa mtoto!
Mkiwa NA msimamo huu, mkijitunza NA kujiheshimu lazima wanaume tutawaoeni, NA mtazaa watoto mkiwa ktk ndoa.
 

Karma

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Messages
9,165
Points
2,000

Karma

JF-Expert Member
Joined May 20, 2019
9,165 2,000
Ukikubali utazoea tu,mbona mitume walio oa wake wengi,baba wa imani pia alikuwa na wake wawili.
Usinilazimishe nifuate imani yako nafuata imani yangu ambayo haitambui ndoa ya wake wengi wala waume wengi inatambua ndoa ya mke mmoja na mume mmoja tu
 

Karma

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Messages
9,165
Points
2,000

Karma

JF-Expert Member
Joined May 20, 2019
9,165 2,000
Elewa hoja nimesema wote mwanaume na mwanamke wanatakiwa kulaumiwa kwa dhambi ya uzinzi na uasherati

Halafu nimekwambia mimi sifuati mitazamo ya jamii iliyojaa maovu ambayo imezoea kumhukumu mwanamke kwa kila kitu mimi nafuata maandiko ya Mungu yanayohukumu kwa haki na yanayotambua kuwa dhambi ni dhambi tu haijalishi imetendwa na mwanaume au mwanamke
Naona umeamua kujitukana mwenyewe na kuwatukana wenzako.

Kwahiyo lawama zinakuja kwetu sio ? Sisi waombaji au ?
 

Zurri

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Messages
10,542
Points
2,000

Zurri

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2018
10,542 2,000
Elewa hoja nimesema wote mwanaume na mwanamke wanatakiwa kulaumiwa kwa dhambi ya uzinzi na uasherati

Halafu nimekwambia mimi sifuati mitazamo ya jamii iliyojaa maovu ambayo imezoea kumhukumu mwanamke kwa kila kitu mimi nafuata maandiko ya Mungu yanayohukumu kwa haki na yanayotambua kuwa dhambi ni dhambi tu haijalishi imetendwa na mwanaume au mwanamke
Sawa.

Ila nakuita,lakini huitikii.
 

Forum statistics

Threads 1,344,662
Members 515,970
Posts 32,831,251
Top