Kwahiyo unataka kuoa single mama?

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
10,637
Points
2,000

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
10,637 2,000
Basi fahamu haya:

Mwanamke aliyezaa huhamishia mapenzi kwa mwanaye. Hali huwa hivyo hata ndani ya ndoa, kiasi kwamba ndoa nyingi hupoteza mvuto pale tu mtoto anapozaliwa. Kwako wewe kijana unayetaka kujitwika mabomu uoe single mother.

Mwanamke anatakiwa aolewe katika ubikira wake ili mwanamume kujisikia kwamba kweli amepata mtu mwaminifu. Lakini kama hata hilo halikutosha kukushawishi, usithubutu kuoa mwanamke ambaye ni single mama, labda kama una uvumilivu usiopimika. Yako mambo kadhaa ambayo yanamfanya single mama asiwe sehemu ya mtarajiwa wa ndoa.

1. Single mama wengi ni matokeo ya uzinzi ama uasherati. Binti anapojiingiza kwenye mapenzi kabla ya ndoa kwa kigezo cha kutafuta kuolewa ni dalili mbaya hata kama ataolewa kweli. Hii inaonyesha kuwa ana udhaifu kwenye eneo la ndoa kiasi kwamba yuko tayari kuutumia mwili wake kama rushwa ili kufanikisha ndoa. Hii haitofautiani na mwanamke aliye ndani ama nje ya ndoa kutumia tigo yake kama kishawishi cha kumshika mwanamume. Unapotumia ngono kama sehemu ya ushawishi, ama kama silaha ya kumteka mwanamume ujue kwamba unaondoa thamani yako na kuingia kwenye kundi la makahaba. Ni kweli uchi wa mwanamke ndio silaha yake kwenye mahusiano, lakini si kwa kuigawa hovyo, bali kwa kuwanyima wanaoitamani ili apatikane mwenye nia thabiti ya ndoa.

Inapotokea binti kajiingiza kwenye mapenzi mpaka kupata mimba, tayari keshapata muunganiko mwingine na mwanamume aliyempa mimba hiyo, tayari wameunganishwa na mtoto huyo, ingawa bado mwanamume aliona huyu mwanamke hafai kuwa mke, alikiwa anamtumia tu kukidhi kiu yake mpaka pale atakapompata mtu sahihi. Sasa wewe ni nani hata ukajiingize kuoa mwanamke wa aina hii?

2. Single mama hawezi kukupenda kwa jinsi ulivyo, bali kutakuwa na sharti la mtoto. Kwamba iwapo utamtunza mtoto kama single mama atakavyo basi utapewa mapenzi matamu. Ni ukweli usiopingika kuwa mwanamke apatapo mtoto mapenzi yote huhamia huko, hivyo wewe jiandae kuwa chaguo la pili kwake. Haya sio mapenzi na ujue tu kuwa huwezi kuwa na amani kamwe.

3. Mtoto si wako. Hata kama utampenda na kumhudumia kwa namna yoyote ile, ukweli utabaki kuwa huyo si mwanao, sio damu yako. Ni kwamba umejitwika jukumu la kumhudumia mtoto wa mwanaume mwenzako ambaye ndiye ataendelea kutambulika kama baba mzazi. Siku akikua ataanza kumtafuta aliyechangia mbegu mpaka akaja dunuani, sio aliyechangia ugali. Ikitokea mmeachana na single mama, ujue ndio mwisho wa kuonana na mwanao mpenzi uliyekuwa ukimtunza kwa nguvu zako zote.

4. Utatumia nguvu kubwa kulilinda penzi. Ili ujihakikishie kuwa single mama anatulizana na wewe, utahitaji kuishi maisha ya kumfurahisha yeye, kumpa atakacho ili asije akamkumbuka mume wake wa kwanza. Namna pekee ya kumfurahisha ni kuhakikisha mtoto wa mwanamume mwenzako anapata maatunzo mazuri, nguo nzuri, elimu nzuri n.k. Utalazimika kuwa karibu naye kuliko hata baba mzazi anavyokuwa, yote haya ni kutafuta kumfurahisha single mama. Utaishi maisha ya kujipendekeza, yenye stress nyingi.

5. Huna sauti juu ya mtoto. Hata kama utataka umchujue mtoto huyu kuwa mwanao kamili, umpe malezi halisi ya mzazi, kuna mahali utakwama tu. Huwezi kumwadabisha kwa mikono miwili, lazima mmoja utakuwa nyuma na mwingine utakuwa mbele. Mara zote utakaa ukijiuliza, labda nikimfanya hivi mama yake atadhani namchukia, jamii nayo itanifikiria vingine. Utajikuta wewe mwenyewe unajiwekea mipaka hata kabla pilato hajakuhukumu kwa kuvuka mstari!! Pigo kubwa zaidi ni pale single mama atakapokutamkia kuwa unamtendea hivyo kwa sababu mtoto sio wako. Hapo utabaki kama mjinga fulani aliyepigwa bumbuwazi asijue aukabili vipi ukweli huu mchungu.

6. Chanzo cha vurugu kwenye familia. Hata ikitokea mmezaa watoto wengine, bado mapenzi hayawezi kuwa sawa. Single mama wana kawaida ya kuwaandalia mazingira watoto wa baba wengine tofauti hao wa baba waliye naye wakati huo. Hufanya hivyo kwa hofu kuwa watoto hawa mara nyingi hawana urrithi kwa baba aliyewalea. Hii huleta mgawanyiko mkubwa kwenye familia kiasi cha watoto wenyewe kuchukiana. Hata ndugu wa mwanamume hawawezi kamwe kumhesabu mtoto huyu kama sehemu ya familia kwa sabubu sio damu yao na anao ukoo mwingine kabisa. Hawezi kujitambulisha kwa jina la baba wa kambo kwa sabubu hana muunganiko wowote naye. Hata ikitokea baba mlezi amekufa, ukoo wake hauwezi kumhesabu mtoto huyu kama sehemu ya urithi. Tunajifunza kwa wanyama wengine pia kama simba, ambapo anapoinuka dume mwingine kuongoza majike, huua watoto wote àliowakuta kisha huanza upya kusaka watoto wake. Sasa sisi hatuwezi kuua, bali tunaweza kuepuka taabu hii kwa kutokuoa mwanamke mwenye watoto.

7. Mume wa kwanza ana nafasi ya kuendelea kumtafuna single mama atakavyo. Kwa kawaida mwanamke akishazaa na mwanamume, ule muunganiko huwa haufi. Tayari ni mzazi mwenza na hana cha khmficha tena, hivyo kupasha kiporo ni jambo la kawaida tu. Pia mama atataka mtoto amjue baba yake halisi kwa ajili ya siku zijazo, hivyo hawezi kujiweka mbali na mzazi mwenzake. Sasa mzazi mwenza ni juu yake kuamua kuendelea kumla ama la, kwani hakuna kutongozana tena, ni kupanga miadi tu na kukutana kuserebuka. Kidume wewe utageuzwa baba mlishi huku haki nyingine zote zikielekezwa kwa mwenye mwanaye.

Ukweli ni kuwa single mama anapopata mume, focus yake sio ndoa bali ni malezi ya mwanaye. Anataka uhakika tu kuwa mwanae ataishi na atapata matunzo bora ili siku za usoni aje kumsaidia yeye.

Ewe kijana, usijiingize kwenye mtego utakaoharibu maisha yako. Tafuta bikira atakayefunga kiapo nawe, achana na wanawake waliozaa hovyo kwa kukosa mwelekeo.

Hapa sijazungumza juu ya walioolewa kisha waume zao kufariki, kwani kwao hawa yako mambo mengi pia nyuma ya pazia ya kuchunguza.
 

Rebeca 83

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2016
Messages
9,523
Points
2,000

Rebeca 83

JF-Expert Member
Joined Jun 4, 2016
9,523 2,000
Nikisema ukweli halisi, mara nyingi single mother ni dalili ya mwanamke asiyefaa kuwa mke wa ndoa. Why?

1. Kama kazaa na mwanamume mwenye ndoa unajiuliza iweje mwanamke anayefaa kwa ndoa ajihusishe na mume wa mtu? Ni dalili mbaya kwake

2. Kama kazaa na kijana mwanafunzi unajiuliza akili ya huyu mwanamke kama anaweza kumudu pressure za ndoa

3. Kama kazaa na kijana asiye na mbele wala nyuma ........

4. Kama kazaa na mtoto wa mama ......

5. Kama hana uhakikababa ni yupi.....

6. Kama kazaa na mwanamume single kisha kamkataa maana yake hatoshi kuwa mke...

Na kadhalika
1.Ana upendo ! Kuona alipewa Maisha chance ya kuja duniani, na yeye pia atoe nafasi kwa kiumbe kingine ...anafaa kuwa mke kwa upendo aliouonyesha!

2.Anayatambua majukumu yake na kuyakabili (responsibilities ) hivyo anafaa kuwa mke

3. Mvumivilivu despite kuonwa na kusemwa vibaya Na baadhi ya watu juu ya Maisha yake na mwanae anavumilia yote hivyo anafaa kuwa mke

Sacrifice wanazotoa single mothers ni sign ya u self-less atakupenda wewe na ndugu zako,, single mothers oyeee lols
 

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
10,637
Points
2,000

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
10,637 2,000
Sawa mkuu

Ila hakuna mstari kwenye biblia umesema mwanamke aliyekwisha zaa asiolewe imetoa hata muongozo kwenye hilo
Na bikra zipo madukani siku hizi nyingi tuu kila mwanamke anaweza kuwa nayo

Cha maana mwombe Mungu akupe mwanamke sahihi
1. Biblia inasema mwanamke asiye bikira apewe talaka
2. Bikra za madukani ni utapeli usio mashiko. Tabia itaumbua
3. Mwanamke sahihi atoka kwa Bwana, sasa Mungu hawezi kukupa kahaba
 

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
10,637
Points
2,000

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
10,637 2,000
Eti uhai wa ndoa unakua determined na bikira hahaaa ingekua it is that important wanawake woote wangeziacha zibaki mpaka waolewe ili wadumu ndoani, acha kuishi ulimwengu wa kufikirika ndugu! ,,, ni kwa vile tu hatuna alama usoni km huyu ni bikira ama not ila ingekua una alama usoni ukiwa bikira sijui ungefanyaje baada ya kugundua labda dada zako wote hawanazo , bado ungepreach hapa JF ubikira??

Single mothers wako veeery strong eti social media sijui zimefanyaje...uhalisia upi unaoongea?? Si tunaona mitaani wakipambana kuhakikisha wao na watoto wao wanapata chakula.. kuwa strong ni ku FACE RESPONSIBILITIES,,,,

Kisha ukahaba upo sababu jinsia zote mbili zimeridhia unacholalamikiwa in this topic ni kuwalaumu wanawake tu ndio wako responsible, ukweli km wanaume wangebaki bikra then wanawake nao wangebaki bikra end of!

Mwisho research jiongeze mwenyewe kuna watu wanafanya research wakiwa biased,,,anyway I also found this research have a look lol https://www.google.co.uk/amp/s/www.independent.co.uk/life-style/love-sex/ideal-number-sexual-partners-before-settling-down-sex-man-woman-marriage-study-a7717571.html?amp
Kwa nini unalilia u single mother? Hao walio strong wangeandamana kwa RC? Nitakuwekea takwimu mbalimbali za uhalifu, uvutaji bangi, ukahaba n.k. uone souce kubwa ni nini
 

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
10,637
Points
2,000

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
10,637 2,000
Mkuu Nyenyere I hope wewe ni bikira ndio maana unasisitiza kuoa bikira.... it's a good thinking

Biblia imetoa miongozo mingi katika maisha ya wanadamu nikukumbushe tuu signature yangu hapo chini muongozo wa biblia. Acha kuwasemea vibaya wanawake waliozaa
Kuzaa nje ya ndoa ni dhambi. Pia kushaui not to marry aliyezaa ni biblical!! Labda nikuulize madam, unaelewa nini pale bibloa inapoongelea kuwa mwili mmoja? Halafu Mungu ni lini anakuwa shuhuda wa mke wa ujana?

Yako mengi uanze na hayo
 

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
10,637
Points
2,000

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
10,637 2,000
1.Ana upendo ! Kuona alipewa Maisha chance ya kuja duniani, na yeye pia atoe nafasi kwa kiumbe kingine ...anafaa kuwa mke kwa upendo aliouonyesha!

2.Anayatambua majukumu yake na kuyakabili (responsibilities ) hivyo anafaa kuwa mke

3. Mvumivilivu despite kuonwa na kusemwa vibaya Na baadhi ya watu juu ya Maisha yake na mwanae anavumilia yote hivyo anafaa kuwa mke

Sacrifice wanazotoa single mothers ni sign ya u self-less atakupenda wewe na ndugu zako,, single mothers oyeee lols
Ooh, basi sawa
 

Rebeca 83

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2016
Messages
9,523
Points
2,000

Rebeca 83

JF-Expert Member
Joined Jun 4, 2016
9,523 2,000
Kwa nini unalilia u single mother? Hao walio strong wangeandamana kwa RC? Nitakuwekea takwimu mbalimbali za uhalifu, uvutaji bangi, ukahaba n.k. uone souce kubwa ni nini
Siulilii usingle mother, na nishakuambia sio kila tafiti ni ya kuiamini I..there are a lot of garbage out there,,,antisocial behaviour sio usingle mother ndio source, antisocial behaviour is to do with harsh and inconsistent parenting style..watoto wanakua na anger issues na sometimes inequality and deprivation ndio ina play .. watoto wa certain area are more likely to misbehave
 

mama D

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Messages
1,788
Points
1,225

mama D

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2010
1,788 1,225
Kuzaa nje ya ndoa ni dhambi. Pia kushaui not to marry aliyezaa ni biblical!! Labda nikuulize madam, unaelewa nini pale bibloa inapoongelea kuwa mwili mmoja? Halafu Mungu ni lini anakuwa shuhuda wa mke wa ujana?

Yako mengi uanze na hayo
Mkuu Nyenyere usisahau hiyohiyo biblia inasema kwa Mungu hakuna kuoa wala kuolewa🤣🤣🤣
 

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
10,637
Points
2,000

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
10,637 2,000
Mkuu Nyenyere usisahau hiyohiyo biblia inasema kwa Mungu hakuna kuoa wala kuolewa
Sio kwa Mungu mkuu, inasema kwenye kiama. Kumbuka ni pale walipoulizwa mke aliyeolewa na wanaume saba kwenye kiama atakuwa wa nani.

[Marko 12
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁹ Mwalimu, Musa alituandikia ya kwamba ndugu ya mtu akifa, akamwacha mkewe wala hana mtoto, ndugu yake amtwae yule mkewe akampatie ndugu yake mzao.
²⁰ Basi kulikuwa na ndugu saba, wa kwanza akatwaa mke, akafa, asiache mzao.
²¹ Wa pili naye akamtwaa akafa, wala yeye hakuacha mzao. Na wa tatu kadhalika;
²² hata na wote saba, wasiache mzao. Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye.
²³ Basi, katika kiyama atakuwa mke wa yupi katika hao? Maana wote saba walikuwa naye.
²⁴ Yesu akajibu, akawaambia, Je! Hampotei kwa sababu hii, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu?
²⁵ Kwa maana watakapofufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika walioko mbinguni.
 

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
10,637
Points
2,000

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
10,637 2,000
Siulilii usingle mother, na nishakuambia sio kila tafiti ni ya kuiamini I..there are a lot of garbage out there,,,antisocial behaviour sio usingle mother ndio source, antisocial behaviour is to do with harsh and inconsistent parenting style..watoto wanakua na anger issues na sometimes inequality and deprivation ndio ina play .. watoto wa certain area are more likely to misbehave
Suala la kuzaa hovyo wala halina mjadala, pia halina namna unaweza kulihalalisha. Ni tabia isiyofaa katika jamii na ni kuwanyima watoto malezi bora. Garbage ni pamoja na kujaribu kuaminisha ouwa hilo ni jambo la kawaida, ni kinyume na noms za jamii isipokuwa kuna kizazi kimekuwa programmed kuamini ni natural. Hata wanyama hawazai bila utaratibu. Mind programming ni jambo la hatari sana
 

Rebeca 83

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2016
Messages
9,523
Points
2,000

Rebeca 83

JF-Expert Member
Joined Jun 4, 2016
9,523 2,000
Suala la kuzaa hovyo wala halina mjadala, pia halina namna unaweza kulihalalisha. Ni tabia isiyofaa katika jamii na ni kuwanyima watoto malezi bora. Garbage ni pamoja na kujaribu kuaminisha ouwa hilo ni jambo la kawaida, ni kinyume na noms za jamii isipokuwa kuna kizazi kimekuwa programmed kuamini ni natural. Hata wanyama hawazai bila utaratibu. Mind programming ni jambo la hatari sana
mnhhhh..

hakuna kizazi kilichokua programmed kuamini ni natural kuzaa hovyo,chochote unachokiona leo jua kilikua in the past generations na kimersuvive kikawa passed on to this generation,this is evolutionary Psychology..this means kuzaa hovyo kulikuwepo na its 'natural' to happen....namaanisha ni jambo la kawaida,sasa wewe unapita na fagio lako kutaka kufagia vitu ambavyo ni natural ku happen, you are wasting your time mkuu....

i understand watoto wanahitaji malezi ya baba na mama..lakini hii isikufanye kuwapa death penality single mothers..wapo wanao work hard watoto wao wasi feel hilo Gap...
 

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
10,637
Points
2,000

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
10,637 2,000
mnhhhh..

hakuna kizazi kilichokua programmed kuamini ni natural kuzaa hovyo,chochote unachokiona leo jua kilikua in the past generations na kimersuvive kikawa passed on to this generation,this is revolutionary Psychology..this means kuzaa hovyo kulikuwepo na its 'natural' to happen....namaanisha ni jambo la kawaida,sasa wewe unapita na fagio lako kutaka kufagia vitu ambavyo ni natural ku happen, you are wasting your time mkuu....

i understand watoto wanahitaji malezi ya baba na mama..lakini hii isikufanye kuwapa death penality single mothers..wapo wanao work hard watoto wao wasi feel hilo Gap...
Ok, tuseme basi suala la uzazi halihitaji kuwa jinsia mbili, hata mwanamke peke yake aweza kujenga familia. Basi hhakuna haja ya malalamiko ya single mothers kutelekezwa, it is natural. Single mothers mmeshinda, zaeni for as much as you wish
 

Forum statistics

Threads 1,343,539
Members 515,077
Posts 32,788,091
Top