Kwahiyo unataka kuoa single mama?

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
10,712
Points
2,000

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
10,712 2,000
Basi fahamu haya:

Mwanamke aliyezaa huhamishia mapenzi kwa mwanaye. Hali huwa hivyo hata ndani ya ndoa, kiasi kwamba ndoa nyingi hupoteza mvuto pale tu mtoto anapozaliwa. Kwako wewe kijana unayetaka kujitwika mabomu uoe single mother.

Mwanamke anatakiwa aolewe katika ubikira wake ili mwanamume kujisikia kwamba kweli amepata mtu mwaminifu. Lakini kama hata hilo halikutosha kukushawishi, usithubutu kuoa mwanamke ambaye ni single mama, labda kama una uvumilivu usiopimika. Yako mambo kadhaa ambayo yanamfanya single mama asiwe sehemu ya mtarajiwa wa ndoa.

1. Single mama wengi ni matokeo ya uzinzi ama uasherati. Binti anapojiingiza kwenye mapenzi kabla ya ndoa kwa kigezo cha kutafuta kuolewa ni dalili mbaya hata kama ataolewa kweli. Hii inaonyesha kuwa ana udhaifu kwenye eneo la ndoa kiasi kwamba yuko tayari kuutumia mwili wake kama rushwa ili kufanikisha ndoa. Hii haitofautiani na mwanamke aliye ndani ama nje ya ndoa kutumia tigo yake kama kishawishi cha kumshika mwanamume. Unapotumia ngono kama sehemu ya ushawishi, ama kama silaha ya kumteka mwanamume ujue kwamba unaondoa thamani yako na kuingia kwenye kundi la makahaba. Ni kweli uchi wa mwanamke ndio silaha yake kwenye mahusiano, lakini si kwa kuigawa hovyo, bali kwa kuwanyima wanaoitamani ili apatikane mwenye nia thabiti ya ndoa.

Inapotokea binti kajiingiza kwenye mapenzi mpaka kupata mimba, tayari keshapata muunganiko mwingine na mwanamume aliyempa mimba hiyo, tayari wameunganishwa na mtoto huyo, ingawa bado mwanamume aliona huyu mwanamke hafai kuwa mke, alikiwa anamtumia tu kukidhi kiu yake mpaka pale atakapompata mtu sahihi. Sasa wewe ni nani hata ukajiingize kuoa mwanamke wa aina hii?

2. Single mama hawezi kukupenda kwa jinsi ulivyo, bali kutakuwa na sharti la mtoto. Kwamba iwapo utamtunza mtoto kama single mama atakavyo basi utapewa mapenzi matamu. Ni ukweli usiopingika kuwa mwanamke apatapo mtoto mapenzi yote huhamia huko, hivyo wewe jiandae kuwa chaguo la pili kwake. Haya sio mapenzi na ujue tu kuwa huwezi kuwa na amani kamwe.

3. Mtoto si wako. Hata kama utampenda na kumhudumia kwa namna yoyote ile, ukweli utabaki kuwa huyo si mwanao, sio damu yako. Ni kwamba umejitwika jukumu la kumhudumia mtoto wa mwanaume mwenzako ambaye ndiye ataendelea kutambulika kama baba mzazi. Siku akikua ataanza kumtafuta aliyechangia mbegu mpaka akaja dunuani, sio aliyechangia ugali. Ikitokea mmeachana na single mama, ujue ndio mwisho wa kuonana na mwanao mpenzi uliyekuwa ukimtunza kwa nguvu zako zote.

4. Utatumia nguvu kubwa kulilinda penzi. Ili ujihakikishie kuwa single mama anatulizana na wewe, utahitaji kuishi maisha ya kumfurahisha yeye, kumpa atakacho ili asije akamkumbuka mume wake wa kwanza. Namna pekee ya kumfurahisha ni kuhakikisha mtoto wa mwanamume mwenzako anapata maatunzo mazuri, nguo nzuri, elimu nzuri n.k. Utalazimika kuwa karibu naye kuliko hata baba mzazi anavyokuwa, yote haya ni kutafuta kumfurahisha single mama. Utaishi maisha ya kujipendekeza, yenye stress nyingi.

5. Huna sauti juu ya mtoto. Hata kama utataka umchujue mtoto huyu kuwa mwanao kamili, umpe malezi halisi ya mzazi, kuna mahali utakwama tu. Huwezi kumwadabisha kwa mikono miwili, lazima mmoja utakuwa nyuma na mwingine utakuwa mbele. Mara zote utakaa ukijiuliza, labda nikimfanya hivi mama yake atadhani namchukia, jamii nayo itanifikiria vingine. Utajikuta wewe mwenyewe unajiwekea mipaka hata kabla pilato hajakuhukumu kwa kuvuka mstari!! Pigo kubwa zaidi ni pale single mama atakapokutamkia kuwa unamtendea hivyo kwa sababu mtoto sio wako. Hapo utabaki kama mjinga fulani aliyepigwa bumbuwazi asijue aukabili vipi ukweli huu mchungu.

6. Chanzo cha vurugu kwenye familia. Hata ikitokea mmezaa watoto wengine, bado mapenzi hayawezi kuwa sawa. Single mama wana kawaida ya kuwaandalia mazingira watoto wa baba wengine tofauti hao wa baba waliye naye wakati huo. Hufanya hivyo kwa hofu kuwa watoto hawa mara nyingi hawana urrithi kwa baba aliyewalea. Hii huleta mgawanyiko mkubwa kwenye familia kiasi cha watoto wenyewe kuchukiana. Hata ndugu wa mwanamume hawawezi kamwe kumhesabu mtoto huyu kama sehemu ya familia kwa sabubu sio damu yao na anao ukoo mwingine kabisa. Hawezi kujitambulisha kwa jina la baba wa kambo kwa sabubu hana muunganiko wowote naye. Hata ikitokea baba mlezi amekufa, ukoo wake hauwezi kumhesabu mtoto huyu kama sehemu ya urithi. Tunajifunza kwa wanyama wengine pia kama simba, ambapo anapoinuka dume mwingine kuongoza majike, huua watoto wote àliowakuta kisha huanza upya kusaka watoto wake. Sasa sisi hatuwezi kuua, bali tunaweza kuepuka taabu hii kwa kutokuoa mwanamke mwenye watoto.

7. Mume wa kwanza ana nafasi ya kuendelea kumtafuna single mama atakavyo. Kwa kawaida mwanamke akishazaa na mwanamume, ule muunganiko huwa haufi. Tayari ni mzazi mwenza na hana cha khmficha tena, hivyo kupasha kiporo ni jambo la kawaida tu. Pia mama atataka mtoto amjue baba yake halisi kwa ajili ya siku zijazo, hivyo hawezi kujiweka mbali na mzazi mwenzake. Sasa mzazi mwenza ni juu yake kuamua kuendelea kumla ama la, kwani hakuna kutongozana tena, ni kupanga miadi tu na kukutana kuserebuka. Kidume wewe utageuzwa baba mlishi huku haki nyingine zote zikielekezwa kwa mwenye mwanaye.

Ukweli ni kuwa single mama anapopata mume, focus yake sio ndoa bali ni malezi ya mwanaye. Anataka uhakika tu kuwa mwanae ataishi na atapata matunzo bora ili siku za usoni aje kumsaidia yeye.

Ewe kijana, usijiingize kwenye mtego utakaoharibu maisha yako. Tafuta bikira atakayefunga kiapo nawe, achana na wanawake waliozaa hovyo kwa kukosa mwelekeo.

Hapa sijazungumza juu ya walioolewa kisha waume zao kufariki, kwani kwao hawa yako mambo mengi pia nyuma ya pazia ya kuchunguza.
 

Mgg3

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2018
Messages
464
Points
1,000

Mgg3

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2018
464 1,000
Ngoja niongelee mtazamo wangu kuhusu single father kuoa single mother. Mwanamume kwa kawaida huwa na mapenzi ya kweli kwa mkewe. Hata kama atazaliwa mtoto mwanamume ataendelea kumpenda mwanamke kwa kiwango kile kile bila kuhamishia mapenzi kwa mtoto.
Mwanamke kwa upande mwingine mapenzi yake hupungua pale tu anapojifungua. Mtoto huwa ndio kila kitu kwake na mume huwa ni chaguo la pili (kama anampenda kweli, vinginevyo atakuwa hata chaguo la 4). Hii inahuasianaje na single mother?
Mwanamume aliye na mtoto akioa mwanamke mwingine mwenye mtoto ni nadra sana kumpata ambaye atampenda mwanaye kikweli na kumlea vema. Mtoto huyo ambaye atahesabika wa kambo kwa mama atanyanyasika kwa kiwango kikubwa sana kiasi kwamba ni wanaume wachache wanaoweza kukabili hili. Hata kama majirani watamuonya kuhusu manyanyaso hayo, bado wengi wa wanaume wanakuwa nhawana sauti kukemea.
Mtoto wa kambo wa mwanamke kwa upande wake atapata mapenzi full tokan kwa baba bila chemne ya ubaguzi, sababu kubwa mlezi ni mama. Mama hulea watoto nyumbani na ni jukumu la kiasili, mwanamume yeye anajali mbunye tu. Hivyo, kuoa SINGLE MOTHER kwa sababu nawe ni SINGLE FATHER sio jibu. Tatizo litakuwa kubwa zaidi.
Umeeleza ukweli mtupu na kama ni mtihani umepata 100%. Hichi ulichoandika kinatokea sana tena sana kwenye jamii zetu. Thumb UP
Mtu ambaye ni single father unamshauri vipi?
 

Rebeca 83

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2016
Messages
9,562
Points
2,000

Rebeca 83

JF-Expert Member
Joined Jun 4, 2016
9,562 2,000
Mimi ambaye siyo single father nakutaka na wewe hiyo ndoa si itakuwa ndoani kweli kwa haya mawazo yako? Mtoa uzi kaandika ukweli lakini ndiyo hivyo anatupiwa mawe. Kuna jamaa yangu ameoa single mother ila mambo anayokutana nayo yanaogopesha sana ndiyo maana nimekataa kuoa single mother hata kwa mtutu wa bunduki. Mwanamke anajali watoto wake na kazi. Kama mwanaume unakuwa namba 3 si bora uwe bachelor milele
SINGLE MOTHER + SINGLE FATHER = NDOA
Just one woman???sample size is too small to make generalization sir!
 

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
10,712
Points
2,000

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
10,712 2,000
Unataka nikujibu kutokana na uhalisia?? Wapo wanawake wengi tu wanaolewa na waume zaidi ya mmoja na ndoa zinadumu ndiyo maana nakwambia wewe unahitaji exposure zaidi ili uendelee kujifunza mambo mengine kuhusu maisha au hata kama hauna exposure basi jaribu hata kuwa mfuatiliaji mzuri wa haya mambo ili siku nyingine usije na nyuzi kama hizi zenye porojo nyingi kuliko uhalisia!!
Amen
 

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
10,712
Points
2,000

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
10,712 2,000
Umeeleza ukweli mtupu na kama ni mtihani umepata 100%. Hichi ulichoandika kinatokea sana tena sana kwenye jamii zetu. Thumb UP
Mtu ambaye ni single father unamshauri vipi?
Ni ngumu sana mkuu, lakini ni bora akaoa binti ambaye hajazaa bado ili aanze kujifunza kumjali mtoto. Sababu kubwa asiye na mtoto akiolewa na single father atajielekeza kumjali mtoto pia akiamini ndipo ulipo moyo wa mumewe, akitafutwa kupendwa zaidi. Kabla ya kuzaa ataamini kuwa kudumu kwake kwenye ndoa kuna husiana moja kwa moja na kumlea vema mtoto wa kambo.
 

Karma

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Messages
9,184
Points
2,000

Karma

JF-Expert Member
Joined May 20, 2019
9,184 2,000
Usitake nikutukane vibaya sana boya wewe, nimekwambia mvulana ni baba yako aliyekuzaa sasa endelea
Hahahaha yaani unanitishia matusi?? Tukana ili tuone kati ya mimi na wewe nani ni mpumbavu sasa na hapo najua hauna tusi jipya zaidi ya yale yale matusi ya nguoni na yale yanayohusisha viungo vya mwili na kuwaingiza wazazi ambayo hayanishitui hata kidogo kwahiyo kama una mapya ambayo sijawahi kuyasikia kabisa yalete!!
 

Khaligraph Jordan

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2017
Messages
4,810
Points
2,000

Khaligraph Jordan

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2017
4,810 2,000
Hahahaha yaani unanitishia matusi?? Tukana ili tuone kati ya mimi na wewe nani ni mpumbavu sasa na hapo najua hauna tusi jipya zaidi ya yale yale matusi ya nguoni na yale yanayohusisha viungo vya mwili na kuwaingiza wazazi ambayo hayanishitui hata kidogo kwahiyo kama una mapya ambayo sijawahi kuyasikia kabisa yalete!!
Kiamba mkumba wewe uliyetolewa ubikira shule ya msingi, ajuza mkubwa.
.
Usinizoee zoee mimi kamzoee baba yako dagaa wewe
 

Ralph Tyler

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2015
Messages
1,609
Points
2,000

Ralph Tyler

JF-Expert Member
Joined Jul 31, 2015
1,609 2,000
Mkuu, nasikitika ulichoandika ni kujaribu kubalance gender. Ukweli hauko hivyo hata kidogo. Nikuulize swali dogo tu, kwa nini inawezekana kwa mwanamume kuoa wanawake zaidi ya mmoja na isiwezekane kwa mwanamke kuolewa na wanaume zaidi ya mmoja?

Sipingi kwamba mwanamume awe na make mmoja kwa sababu za kiimani lakini,, hoja hapa ni binti asiolewe na mwanamume aliyezaa this is wrong in all accounts. Labda kama ni kwa mtazamo was equality na sio uhalisia na asili.

Nakusikiliza
Ndiyo, binti asiolewe na mwanaume aliyezaa, akitaka yakamfika avumilie tu. Ukichanganya ulanzi wa leo na mkangafu unapata kitu tofauti kabisa, msichanganyane mtaumizana bure.
Binti kuolewa na mwanaume aliyezaa ni sawa na kuolewa mke wa pili, unless huyo mzazi mwenza alishafariki. Kama mzazi mwenza yupo, na hata kama ameolewa, na hapo nakujibia swali lako, ni mke mwenza mwenye waume wawili.
Hii nilishuhudia mwaka juzi kwenye harusi, bibi harusi alikuwa na baba wawili pale high-table, mmoja ni baba mzazi na mwingine ni mume wa mama yake, kiuhalisia wote wawili walikuwa waume za mama yake kwa sababu kuna wakati walikuwa wanamhudumia mwanamke huyohuyo at the same time. Mwanaume A anatoa matunzo ya mwanae na mwanaume B anatoa matunzo ya familia lakini yote yanapokelewa na mwanamke C na yanatumiwa na familia ileile!
Acheni watu waoane fresher kwa fresher, mkangafu kwa mkangafu. Tofauti na hapo ni duhuluma na kuumizana roho!
 

Ralph Tyler

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2015
Messages
1,609
Points
2,000

Ralph Tyler

JF-Expert Member
Joined Jul 31, 2015
1,609 2,000
Na kweli tumuulize mtoa mada hili swali mbona wanaume wakitongozwa na wanawake hawakatai??
Hakuna mwanaume mwenye uwezo wa kukataa anapotongozwa na mwanamke, isipokuwa tu kama huyo mwanamke mvuto ziro. Otherwise sumu haijaribiwi kwa kuionja. Ukibipu unapigiwa. Ukiacha goli wazi kitu kinatinga, na matokeo yake yanakuhusu mwenyewe mwanakulitaka mwanakulipata, unakuwa singo maza unahangaika nalo na hata aliyekupelekea moto atakuwa miongoni mwa watakaokucheka!
 

Ulweso

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2016
Messages
12,474
Points
2,000

Ulweso

JF-Expert Member
Joined May 24, 2016
12,474 2,000
Hakuna mwanaume mwenye uwezo wa kukataa anapotongozwa na mwanamke, isipokuwa tu kama huyo mwanamke mvuto ziro. Otherwise sumu haijaribiwi kwa kuionja. Ukibipu unapigiwa. Ukiacha goli wazi kitu kinatinga, na matokeo yake yanakuhusu mwenyewe mwanakulitaka mwanakulipata, unakuwa singo maza unahangaika nalo na hata aliyekupelekea moto atakuwa miongoni mwa watakaokucheka!
Pia mawanawake wasilaumie kuwa ni maharagwe ya mbeya, maana mwanamke awaweza tongozwa na me 10 na akawakataa wote, lakini mwanaume akitongozwa na k 10 atakubali 7
 

uungwana classic

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2014
Messages
1,956
Points
2,000

uungwana classic

JF-Expert Member
Joined Jun 9, 2014
1,956 2,000
Tuache kuishi maisha nyuma ya wakati kwa wakati kama huu ni tofauti na zamani kiukweli kujilinda mpaka uwe na miaka 30+ ni ngumu sana so kwa sasa tuishi hivyohivyo tu angalia mazingira na mtu ambaye unawaza kuwa naye kabla hujacheki usingle mama wake otherwise unaweza poteza mke mwema kisa umekuta ni single mum et ni mke wa mtu
 

Karma

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Messages
9,184
Points
2,000

Karma

JF-Expert Member
Joined May 20, 2019
9,184 2,000
Hakuna mwanaume mwenye uwezo wa kukataa anapotongozwa na mwanamke, isipokuwa tu kama huyo mwanamke mvuto ziro. Otherwise sumu haijaribiwi kwa kuionja. Ukibipu unapigiwa. Ukiacha goli wazi kitu kinatinga, na matokeo yake yanakuhusu mwenyewe mwanakulitaka mwanakulipata, unakuwa singo maza unahangaika nalo na hata aliyekupelekea moto atakuwa miongoni mwa watakaokucheka!
Sasa kama wanaume hamuwezi kuchomoa mnapotongozwa na wanawake mnadhani ndiyo itakuwa rahisi kwa wanawake kuchomoa wanapotongozwa na wanaume??
 

Karma

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Messages
9,184
Points
2,000

Karma

JF-Expert Member
Joined May 20, 2019
9,184 2,000
Tuache kuishi maisha nyuma ya wakati kwa wakati kama huu ni tofauti na zamani kiukweli kujilinda mpaka uwe na miaka 30+ ni ngumu sana so kwa sasa tuishi hivyohivyo tu angalia mazingira na mtu ambaye unawaza kuwa naye kabla hujacheki usingle mama wake otherwise unaweza poteza mke mwema kisa umekuta ni single mum et ni mke wa mtu
Umenena vyema sana mkuu
 

Forum statistics

Threads 1,344,956
Members 516,083
Posts 32,840,962
Top