Kwaheri Zanzibar, utazima moto utaowaka Tanganyika lakini usitusahau endelea kutuombea

Godwine

JF-Expert Member
Jan 15, 2010
1,371
281
ZANZIBAR umekuwa huru na wananchi wako wametulia , lakini Tanganyika inakaliwa kwa mabavu na viongozi wa CCM, wanateka kila haki ya msingi ya wananchi, wametutungia katiba ya Tanganyika na kutuambia ni ya Muungano wa Tanzania. wameamua kujilipa posho za kutuwakilisha bila ya kutuuliza , wamenunua ndege ya rais bila kutuuliza, wamenunua rada ya kuangalia Ukonga na kutuambia itaangalia UK bila kutuuliza.....

Wazanzibar mtapokwenda msisahau kuturushia kamba....na VISA za taifa lenu mtuwekee masharti nafuu kwani watanganyika tunaoteswa ni ndugu zenu na tumeishi vyema muda mwingi
 
GOODWINE: Nimeipeda sana hii. Kwa wale tulio kwenye maombolezo na kumlilia marehemu Tanganyika: huu ni ujumbe wa faraja na wa matumaini katika kipindi hiki tunaposubiri marehemu Tanganyika afufuke.
 
Mkuu si kila kitu kinachofanywa na serikali au watawala,watawaliwa(Wananchi) lazima waulizwe,kama utalatibu huu uatatumika ni referendum ngapi zitafanywa kwa siku,wiki,mwezi na hata kwa mwaka?sina maana nakubaliana na uovu unaofanywa na watawala,nisichokubaliana na wewe ni suala la kuuliza kwa wananchi.Kwa kweli viongozi wetu wanapaswa kulaumiwa kwa kushindwa kufanya maamuzi ya busara ambayo yangeisaidia nchi kupiga hatua za maendeleo kwa haraka!
 
ZANZIBAR umekuwa huru na wananchi wako wametulia , lakini Tanganyika inakaliwa kwa mabavu na viongozi wa CCM, wanateka kila haki ya msingi ya wananchi, wametutungia katiba ya Tanganyika na kutuambia ni ya Muungano wa Tanzania. wameamua kujilipa posho za kutuwakilisha bila ya kutuuliza , wamenunua ndege ya rais bila kutuuliza, wamenunua rada ya kuangalia Ukonga na kutuambia itaangalia UK bila kutuuliza.....

Wazanzibar mtapokwenda msisahau kuturushia kamba....na VISA za taifa lenu mtuwekee masharti nafuu kwani watanganyika tunaoteswa ni ndugu zenu na tumeishi vyema muda mwingi

...
Lakini ole wako ewe marehemu uliyefufuka,Zanzibar!
Unaingia kaburini anakoishi marehemuTANGANYIKA,kinyume cha makubaliano{Katiba} huku ukitumia rasilimali zake kujinufaisha.
Ewe TANGANYIKA,utabaki kubwa jinga hadi lini?
 
Mkuu si kila kitu kinachofanywa na serikali au watawala,watawaliwa(Wananchi) lazima waulizwe,kama utalatibu huu uatatumika ni referendum ngapi zitafanywa kwa siku,wiki,mwezi na hata kwa mwaka?sina maana nakubaliana na uovu unaofanywa na watawala,nisichokubaliana na wewe ni suala la kuuliza kwa wananchi.Kwa kweli viongozi wetu wanapaswa kulaumiwa kwa kushindwa kufanya maamuzi ya busara ambayo yangeisaidia nchi kupiga hatua za maendeleo kwa haraka!

serikali lazima iwaulize wananchi wake, lakini namna ya kuwauliza ndio inategemeana, kuna kuuliza kupitia kwa wawakilishi wetu yaani wabunge, kama wabunge wangekuwa wanatusikiliza na kutetea haki na yale tunayowatuma na sio wanayojituma basi kama serikali ingewauliza wao ingemaanisha imetuuliza sisi lakini kwa mfumo wa wawakilishi wa sasa serikali ikiwauliza basi inakuwa imeuliza vyama vya siasa na si wananchi
 
jamani na maalim anataka bank kuu za zanzibar (BOZ) du kazi kweli kweli zanzibar wamechoka EPA, Dowans, Rizwans, na mabilioni ya JK
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom