Kwaheri "viroba", buriani "viroba", mbele yako,nyuma yetu.Tutakukumbuka sana

Mdakuzi mkuu

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
212
719
Salam wakuu,ndugu zangu hapa JF!

Tusijisahaulishe na tukio zito la tarehe 01 March , 2017, ambapo katazo la viroba linaanza kufanya kazi. Kwa wazalishaji, wasambazaji, wauzaji na wanywaji a.k.a walengwa.

Kuna aina nyingi sana za viroba mfano Konyagi, Valuer, Jogoo, Zanzi, nk...vyote hivyo vimekumbwa na hilo katazo, katazo toka kwa Mh Waziri Mkuu Kassim Majaliwa!

Ni pombe ambazo kwa kweli zimekuwa rafiki sana kwa mazingira yetu, hali ya hewa, vipato vyetu na pia "spirit" ambayo imekuwa ikitengenezea vinywajo hivyo, inazalishwa hapa Tanzania. Siku zote Konyagi imekuwa ikionesha uzalendo, hasa unapoichanganya na kipande cha limao au barafu.

Viroba vimekuwa vikiuzwa kwa TZS 500, 1000 mpk 1,500 kutegemeana na mfuko wako. Kwakweli zimekuwa rafiki sana. Ukiwa na buku 3, unakaa kwenye momentum safi kabisaaa sawa na aliyekunywa bia za elfu 30 mpk 40. Sina la kusema kwakweli.

"Buriani viroba, mbele yako , nyuma yetu.Tutakukumbuka sana"
 
Alie kwambia vitaadimika nani! Vipodozi tfdi kila siku wanapiga marufuku,wanakagua na matangazo ya madhara kwenye media lakini ndo kwanza vimejaa madukani......sembuse virobo...bado sana.........unataka kunambia T.i.d baada ya kujitangaza juzi kuacha unga ndo kaacha na baada ya kamata kamata ya wahusika wa unga ndo unga umeadimika?...makatazo ya hapa kwetu ni mbio za sakafuni ndugu yangu
 
Sijui chadema kama wana hela ya kuwanywesha walevi wao jack daniels.
 
Kirobaaaaaa awe Kirobaaaaaa weeeee [HASHTAG]#niko[/HASHTAG] kwa mangi nimemwambia anikopeshe tu maana baada ya tarehe moja ni haramu hahahahhaa
 
kwa hili la viroba aisee watatukamata wengi, ila uzuri tumekuja na plan B ya kuvinywa hatutafyonza bali tuta....... watashangaa tunayumba tu, sifa ni kulewa sio kunywa, bia moja sawa na viroba 4 lazima vienziwe.
 
na ndipo pombe za karatasi za nchi za jiran zitajaa mfano malawi kuna vipombe vya ajabu ajabu vipo mbeya ambavyo ukiwa na buku lazima ukae sasa ndo zitaenea nchi nzima
 
Back
Top Bottom