Kwaheri Hayati Magufuli (Jeshi), karibu Rais Samia Suluhu (Iron Lady)

Waziri wa madini

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
379
465
KWAHERI HAYATI MAGUFULI (JESHI),KARIBU RAIS SAMIA SULUHU HASSAN(IRON LADY)

Taifa letu teule lipo katika wakati mgumu sana wamaombolezo na majonzi kwa kuondokewa na mpendwa wetu aliyekuwa rais wa tano jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Joseph Magufuli.

Kwa upendo Wa Mungu juu ya nchi yetu na kwa mujibu wa katiba ya Tanzania tumefanikiwa kumpata jemedari shujaa na jasiri Mheshimiwa Samiah suluhu hassan kuwa Rais rasmi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Hatuna shaka na utendaji wake, hatuna shaka na uhodari wake tumeona mengi aliyoyafanya wakati akiwa makamu wa Rais akishirikiana na aliyekuwa raisi hayati Magufuli hakika hakukuwa na dosari hata chembe katika utendaji wake uliotukuka.

Mheshimiwa Rais Samiah Suluhu Hassan akiwa kama Mwanamke jasiri(iron lady) aliyesheheni hekima busara na maono katika utendaji wake hatuna shaka kabisa yeye ni zawadi toka kwa Mungu na tunahakika atatuvusha na tunatarajia kuona makubwa zaidi katika uongozi wake akiwa kama Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania tunaimani naye.

Ushauri wangu kwa wananchi wa Tanzania,najua tumepata pigo kubwa na mioyo yetu imeumia sana kwa sababu tulimpenda sana aliyekuwa raisi wetu alijitoa kwaajili yetu hasa wananchi wanyonge na masikini,alikuwa akitutumikia kama Rais mwenye kutanguliza maslahi ya watu mbele bila kubagua na kuleta upendeleo,alikuwa akitekeleza ahadi zake kwa vitendo na kujituma sana katika majukumu yake, alikuwa mwenye hofu ya Mungu na daima akimtanguliza Mungu mbele, alikuwa mtetezi wa wanyonge na mkombozi wa rasilimali zetu za Tanzania.

Kwa ujumla wake watanzania tutamkumbuka kwa mengi mazuri kama yeye mwenyewe alivyojitabiria ,pamoja kuwa tunauchungu sana na majonzi makubwa ila tusisahau kuwa sisi sote ni wa Mungu na kwake tutarejea na bwana ndiye anayetoa na yeye ndiye anaye twaa jina lake lihimidiwe.

Kifo cha mpendwa wetu ni ahadi ya Mungu kwani siku zote kazi ya Mungu haina makosa ,tunatakiwa tushikamane sana tuondoe tofauti zetu na tusikubali kupokea maneno ya uchonganishi na uchochezi sababu siku zote wanaoanzisha chokochoko lengo lao huwa ni kutugombanisha ili tuharibu amani yetu.

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa yaliyotokea na kusonga Mbele tumepata raisi imara , shupavu ,jasiri na mchapa kazi tusiwe na shaka wala hofu Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan atatuvusha na ataendeleza mazuri yote yaliyoachwa na hayati Magufuli kwani yeye ndiye aliyekuwa msaidizi wake wa karibu zaidi katika Majukumu yote ya Serikali.

Tumuombee Rais wetu ,tupuuze habari za uzushi na uchochezi zenye lengo la kutugawa ,tufanye kazi kwa jitihada kwani ndio njia sahihi ya kumuenzi hayati Magufuli ,tulinde amani yetu na mshikamano ili tuweze kutimiza ndoto ya Tanzania tuitakayo.

Ushauri kwa wanasiasa huu si wakati wa kutafuta umaarufu wa kisiasa , kukuza majina wala kulipa visasi ,huu si wakati wa kuendeleza chuki na majungu ,huu si wakati wa kupigania vyeo na madaraka,huu ni wakati wa kuchapa kazi, kuwa waadilifu na kuwatumikia watanzania ambao wanamatumaini makubwa na Serikali yao ,huu ni wakati wa kumsaidia Mheshimiwa Raisi kujenga Tanzania iliyoimara ,huu ni wakati wakutanguliza uzalendo ili tuweze kufikia malengo makubwa tuliyojiwekea kama nchi inayopiga hatua katika maendeleo.

Wito kwa viongozi wa dini tumuombee Rais wetu mpendwa Mama samiah suluhu hassan ili aweze kutekeleza majukumu yake kama raisi akiwa na baraka za Mungu, tuiombee nchi yetu ambayo ipo salama usalimini amani na upendo uzidi kutawala,tuwahimize wananchi ambao wao ndio waumini wa dini mnazoziongoza wajue thamani ya nchi yao wadumishe amani na upendo ili nchi yetu izidi kubarikiwa.

Nchi yetu inathamani sana umoja wetu ndiyo mafanikio yetu. Mungu ibariki Afrika Mungu ibariki Tanzania Mungu mbarikiwa raisi wetu mpendwa na hodari shujaa Mama Samia Suluhu Hassan.
 
Umbali toka DAR, DODOMA hadi kyela nimbali.

Tupeni taarifa tunasikia majina meengi

Majaliwa, bashiru, cdf, jk, mwinyi, ssh ndo wakina nan TZ hii.
 
Hakika Mama Samia ni Iron Lady, tuna historia yake nzuri toka alipopata umaarufu kutokana na umakini wake wakati wa bunge la Katiba pendekezwa. Sasa ni Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na Usalama tutaRajie kasi mpya.
 
Back
Top Bottom