Kwaheri Hayati Dkt. Magufuli, hatimaye mwendo umeumaliza na umetuachia funzo

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Tanzania ilizizima kwa taharuki,simanzi na kila aina ya mtikisiko kwa mapokeo ya hisia juu ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania JPM au John Pombe Magufuli,mara baada ya tanzia iliyotolewa na aliyekuwa makamu wa rais ambaye kwa sasa ndiye rais wetu,hakika inatupa picha kuwa kifo hakina uchaguzi,siku ikifika hata uwe una nini utakwenda tu. Tuombe Allah amuepushie adhabu ya kaburi na amuepushe na Moto wa Jahanam,amen.

Kifo hiki kilizima uvumi na ukanushaji wa baadhi ya viongozi juu ya afya ya kiongozi-mtawala huyo,ambao kupitia tetesi mbalimbali nguvu kubwa ya kidola ilitumika kudhibiti ukweli uliosemwa. Hii ina tupa funzo kwa viongozi/Watawala kutumia busara na weledi katika kuhakikisha Hali Kama hii inapotokea kutafuta suluhisho ambalo halijenga chuki ya wananchi kwa viongozi wao.

Ni kawaida ndugu wanapo hitilafiana suluhisho la migogoro yao humalizwa kwenye matatizo Kama hili lililotokea kwa Taifa hili,maanake nini,msiba huu uwe mwanzo wa kufungua ukurasa mpya wa maridhiano kwa kuondoa mitafaruku iliyo ligawa Taifa kwa misingi ya chuki na utengano.

Tunapo msitiri mzee Magufuli,tutangulize utaifa mbele kwa kuwa yote yaliyofanyika chini ya utawala wake ni katika kuhakikisha tunajenga Taifa moja,hii itatufanya tusahau maumivu tuliyopitia kwa namna moja au nyingine na kuchukulia Kama changamoto kwa tuliobaki safarini,kwa kumtakia pumziko jema katika safari yake ya makao ya kudumu.

Watanzania turudishe utamaduni wetu wa kuheshimiana,kuaminiana,kuoneana huruma na kuombeana kheri. Kushangilia au kubeza msiba ni utamaduni mbaya Sana ambao kwa kutumia nguvu ya dola kuzuia hisia za watu ni zaidi ya kuchochea chuki na kuendeleza utamaduni huu mbovu na mpya kwa Taifa letu,ndo maana nasisitiza Sana kuzika tofauti zetu kwa majadiliano na maridhiano katika meza ya mazungumzo kwa ajili ya mustakabali wa wananchi na serikali yao.

Magufuli atakumbukwa kwa ari yake ya kuhakikisha maendeleo yanapatikana lakini jambo hili lisifanywe la utashi wa kiongozi au Mtawala aliyeko madarakani. Linapaswa kuwekewa mikakati kikatiba ili atayekuja aweze kuendeleza kwa utashi wake,suluhisho pekee ni katiba mpya.

Ni hakika Magufuli hakuwa malaika,aliumbwa na mapungufu yake Kama binadamu wengine,tusichukulie mapungufu yake Kama hukumu kwake,kwa kuwa mwenye dhima hiyo ni Allah (SW) na hatujui aliongea nini na Mungu wake wakati akipambania Maisha yake,ila tuzione Kama changamoto katika kufutana machozi.

Hata Mwalimu Nyerere aliwahi kusema,serikali yake haikuwa ya kimalaika kuna mazuri na mabaya waliyafanya,badala ya watu kuendeleza au kurithi mazuri yao wameamua kuendeleza mabaya . Kwa mantiki hiyo utaona pamoja na maumivu waliyopitia Watanzania kwa utawala wake bado alikuwa muungwana kukemea mabaya ya awamu yake yasirithiwe na awamu zingine.

Tunapo muenzi na kumsitiri mwenzetu,ndugu yetu Magufuli,tukumbuke kuachana na mabaya yake ili mazuri yake yawe na tija kwa Taifa bila kumuumiza mtu. Hapo hakika tutakuwa tumejenga Taifa jipya na kurudisha jina letu la asili, kisiwa cha amani.

Nenda Magufuli,MWENDO UMEUMALIZA unapopanga yako Allah naye amekwisha panga yake,umetuachia dira ya maendeleo lakini tutahakikisha changamoto ya maridhiano iwe chachu ya kufikia maendeleo uliyo kusudia,hakika wewe ni wake na kwake ni marejeo.

Mwanga wa milele akuangazie,upumzike kwa amani,amiin .

N
 
Naona wanafamilia na wageni waalikwa wanaelekea sehemu ya tukio sasa! Muda si mrefu marehemu atahifadhiwa kwenye nyumba yake ya milele.
 
original.gif

Wacha tuendelee na Ulanzi wetu
 
Back
Top Bottom