Kwaheri Hayati Dkt. John Pombe Magufuli

Pole na Hongera sana Mkuu, hivi ndivyo binadamu tunatakiwa kuwa usimbebe mtu moyoni na kifuani kwako siku zote.

Mungu akusimamie katika kazi zako na akupe nguvu.

Pumzika kwa amani JPM.
 
Hatimaye Leo Ndiyo Kilele Cha Siku 21 Za Maombolezi Bila Shaka Sasa Hatutaweza Tena
Kuwaza Nyuma Isipokuwa Msemo Wako!!
Tuchape Kazi


Leo Vyombo Vya Habari Vimefunguliwa Huku
Wengine Siyo Waandishi Wa Habari Utawasikia Vigogo Wafa!!😃😂😁😀
 
Mkuu Wangari, the man, i.e. Magufuli alikuwa controversial sana. Sana tu. Mungu nisamehe kama nakosea lakini mimi naona ni kama Mungu ameamua kumwondoa ili watanzania wasiangamie tena. Hebu fikiria watu waliofariki tangu covid iingie na ambao wangeweza kupona kama angetuongoza vizuri. Ni kwa sababu watanzania tuko kama nyumbu na hatujihangaishi kufuatilia mambo lakini wamekufa watu wengi sana, tena vifo vya mateso kwa covid. Fungakazi ni pale walipokufa mapandri na watawa (of course na watu wengine wengi) na uongozi wa kanisa ulipoamua kuingilia kati kuwaeleza ukweli waumini wake, marehemu akawasema sana na kubeza. Hivi unataka kuniambia hakuwa anaona hivyo vifo? Ni kwanini hakujali na hakutaka uongozi wa kanisa ujali? Anafaidika nini kwa watu kufa? Unakumbuka mara ya mwisho kanisani alivyombeza uongozi wa kanisa kwa kusema watu wavae mask? Kutoka hapa ndiyo alianza kuugua na kifo. Mungu hadhihakiwi!

Neno”controversial” linampa kasifa ya “ujanja” fulani hivi. Lakini ukweli Hayati alikuwa na tatizo kubwa sana. Kwa uwazi kabisa, alikuwa kazidiwa na sifa za kiburi, jeuri na ujinga (ignorance). Na kwa hayo alikuwa “an open book” - what you see is what you get. Mtu anayediriki kuwatishia maDED hadharani wasithubutu kutangaza ushindi wa wapinzani. Hakuna mwanasiasa anayefanya ujinga aina hiyo.

Kwa jeuri tu ya kutaka kuthibitisha yeye ni zaidi kuliko wapinzani, “mabeberu”, viongozi wa dini na wataalamu wa afya, aliamua kucheza kamari na virusi vya corona hadi vikampata na kumshughulikia. Mambo aliyokuwa akifanya wala hayahitaji mjadala mgumu. Matokeo yake yako wazi. It’s just a matter of time.

Mwenzake, Trump, naye alikuwa akiwapumbaza wafuasi wake hivyo hivyo, LAKINI yeye na familia yake walipata chanjo kimyakimya Januari wakiwa ikulu. Huo “ujinga” ulikuwa ni wa kujifanya tu. Baadaye akajifanya kupromote chanjo eti “it’s safe, it works) baada ya baadhi ya wafuasi kuwa wametishia kuwaua akina Dr. Fauci, Bill Gates, nk.
 
Katika maisha ya mwanadamu, mambo mawili: mwanzo na mwisho, ni hakika.

Japo ni Mungu pekee ajuaye, kwa upendeleo, sisi tumeuona mwanzo na mwisho wako.

Tumejifunza mengi kupitia maisha na kifo chako – Ee Mungu tujaalie mwisho mzuri.

Kwaheri Mhe. JPM.
Tunakukumbuka Chuma
 
Back
Top Bottom