Kwaheri Diana, tutaonana Mungu akipenda...

Habari za ajali nimezipata kutoka kwa vyanzo sahihi. Dereva (Ibra ambaye ni mtoto wa dada yake Diana) aliyenusurika na ajali hiyo anasema: Mbele yao kulikuwa na magari makubwa mawili yaliyoharibika njiani upande wa kulia eneo la kona lenye mwinuko Machimboni Igawa. Hao madereva w magari yaliyoharibika hawakuchukua tahadhari yoyote. Wahanga walikuwa upande sahihi, lakini katikati ya magari mawili hayo yaliyoharibika Fuso ilikuwa inakuja kwa kasi upande wao. Ibra alijaribu kuingia kwa Ghafla katikati ya Magari mawili kulikwepa Fuso lililokuwa liwagonge uso kwa uso; lakini alichelewa na kubamizwa upande wa nyuma ambao ndio walikaa wahanga.
 
Ilikuwa alfajiri yenye simu ya mshtuko sana, kwamba P amka..'Diana hatunae tena' nilishindwa kuelewa, sikuweza kuamini.

Kiukweli ni alfajiri ya huzuni kubwa sana.

Diana alikuwa ameanza safari yake ya kufunga ndoa takatifu ambapo alienda Mbeya kwa ajili ya kuagwa na wazazi 'Send off' ili baadae send off kubwa ya ndugu, marafiki na jamaa ifanyike Jijini Dar es Salaam tarehe 27 June 2019.

Means Next Thursday, just to know that a week before her day Diana amefupishwa maisha yake na ajali iliyotokea maeneo ya Igawa mbeya.

Ajali ambayo imemchukua Diana, pamoja na ndugu zake wengine wa kuzaliwa watatu !!

Ilikuwa ni usiku wa kikatili sana kwa kweli.

Mungu azilaze roho za marehemu mahala Pema peponi.

Nitakukumbuka sana Diana kwa ucheshi na uchangamfu wako. Mungu akupokee wewe na ndugu zako.


Kwaheri ya kuonana Kipenzi!


View attachment 1131646

Diana Akiwa na Mumewe mtarajiwa enzi za uhai wake...











.
R. I. P
 
Back
Top Bottom