Kwaheri 2012, nini kilikuumiza na nini kilikufarahisha, funguka. Kwa mfano mimi

kwamtoro

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
4,922
3,234
Kitu kilicho nisononesha na kuniumiza 2012 ni hiki hapa.

UFAFANUZI KUHUSU FAO LA KUJITOA KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII.


Ufuatao ni ufafanuzi mfupi kuhusu marekebisho ya Sheria za Mifuko hasa kuhusu fao la kujitoa.
20 JULAI, 2012

Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.

Na kilichonifurahisha 2102 ni kupata watoto mapacha wa kike na kiume.
 
Kitu kilinisononesha mwaka 2012 ni kusikia ufisadi mwingine wa mabilioni ya dola yaliyofichwa nchini Uswisi, ina maana watanzania bado hatujapata dawa ya mafisadi tu!!!.
 
Mimi kilicho niboa kupoteza mtoto wangu kwenye ajali ya Skagit pamoja na Chadema kupoteza umeya jiji la Mwanza

na kilicho nifurahisha kupata watoto mapacha
 
Siwezi kusema maana sijaumaliza je nikifa leo nitarudi tr 31/12/12 saa 23oohrs nitachangia hii sired
 
Kilichoniumiza zaidi ni kutekwa na kuteswa kwa mtetezi wa sector ya afya, Dr Ulimboka. Pia kifo cha Mwandishi wa habari Daudi Mwangosi. Ni matukio yanayoniuma hadi leo. Kilichonifurahisha zaidi ni CHADEMA kushinda ubunge Arumeru mashariki.
 
Niliumizwa na jinsi BARAZA LA MITIHANI lilivyobainika kuwafelisha
wanafunzi wa kiislamu na pale lilipoguswa tu Shekh Ponda akawekwa
ndani kwa kisingizio cha kuvamia kiwanja lakini kumbe tatizo ni kugusa
makaomakuu ya Mfumo nanihii.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom