Kwaheri 2011 na machungu yake karibu 2012 na baraka zake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwaheri 2011 na machungu yake karibu 2012 na baraka zake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ndachuwa, Dec 30, 2011.

 1. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Eeh Mungu mwenyezi mwingi wa rehema na baraka, nashukuru kwa baraka ya uhai hata kufika siku ya leo ninapoelekea kuaga mwaka 2011 na kuupokea mwaka 2012 kwa moyo mkunjufu.

  • Nashukuru Eeh Mungu Baba kwa mapito yote niliyokumbana nayo mwaka huu na wakati wote nilijipa moyo nikiamini hutanitupa Baba, na kweli kwa neema zako niliyashinda yote.
  • Nashukuru hata siku ile ya tarehe 16/10/2011 nilipokuwa natoka matembezi ya jioni, nikiwa katika mwendo wa taratibu kabisa ghafla nilianguka na kuvunjika kwenye kiwiko cha mkono wa kazi mkono wa kulia, nashuruku uliwatuma wapita njia wengine ambao waliniinua na kunipeleka hadi nyumbani; kwa tukio lile maswali yamekuwa mengi bila majibu, nami sina majibu zaidi ya kushukuru kwa kila jambo.
  • Nashukuru Mungu baba kwa msaada wako madaktari wa mifupi walifanikisha kazi upasuaji mkono wangu tarehe 22/10/2011 na kuunga mfupa uliokatika kwenye kiwiko kwa waya; nashukuru pamoja na maumivu ya upasuaji na waya ulio mwilini mwangu niliweza kukamilisha na kutuma "course work for MSc Finance - Financial Reporting and Analysis" tarehe 04/11/2011 somo la kwanza kabisa katika hiyo kozi. Nashukuru Eeh Mungu Baba kwani ilipofika 11/11/2011 pamoja na maumivu makali niliweza kufanya mtihani wa FRA ingawaje majibu bado kwa Imani na baraka zako utakuwa umenivusha.
  • Nashukuru Eeh Mungu Baba nikiwa naendelea kuhudhuria mazoezi ya kukunja na kunyoosha mkono uliopasuliwa, tarehe 5/12/2011 ukamchukua Dada yangu mpendwa katika pumziko la milele; Eeh Baba naomba umlaze mahali pema peponi Amina.

  Pamoja na mapito yote hayo, Nashukuru Mungu Mwenyezi kwani kuanzia mwanzo wa mwaka 1/1/2011 hadi leo umeendelea kubariki kazi za mikono yangu; familia yangu haikuwahi kupungukiwa mahitaji muhimu; sikuwahi kuvuka Ijumaa ya mwisho wa mwezi bila kuwalipa wasaidizi wangu stahili zao. Nasema Ahsante Baba kwa yote mazuri na yaliyokuwa machungu kwa mwaka 2011; naomba Baba Mungu Mwenyezi unipunguzie yale machungu na kuzidisha yale mazuri kwa mwaka 2012. AMINA
   
 2. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  duh! Mungu ni mwema.hutupa tuombayo na tusiyoomba.baraka zake zitimie
   
Loading...