Kwaheri 2008 karibu 2009 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwaheri 2008 karibu 2009

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Baba Mkubwa, Dec 31, 2008.

 1. B

  Baba Mkubwa JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 770
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nikiwa kama mwana-member, ninapenda kuwatakia wote mafanikio mema katika mwaka huu unaoanza, mwaka 2009. Ninaamini mwaka unaoisha una mafanikio na hasara pia, all in all "May The Year 2009 Bring for You Happiness,Success and filled with Peace,Hope & Togetherness of your Family & Friends....

  Wishing You a...*HAPPY NEW YEAR*" 2009
   
 2. M

  Mama JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  sydney bridge.jpg
  New year fireworks in Sydney Habour bridge
   
 3. M

  Mama JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Hivi Tanzania bado hawaruhusu fataki wakati wa mkesha wa mwaka mpya ?

  Kutoka BBC: Pamoja na sehemu nyingine duniani Auckland na Sydney wameshauona 2009 katika link hii.
   
 4. Suki

  Suki JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2008
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 373
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Last I checked,one required a written permission to do so.
   
 5. B

  Baba Mkubwa JF-Expert Member

  #5
  Dec 31, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 770
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kumependeza, tutumie ma-link mengine, tuenjoy. Thanks Mama
   
 6. M

  Mama JF-Expert Member

  #6
  Dec 31, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Naples sex strike over fireworks


  [​IMG]

  New Year's Eve could go off without a bang for some Neapolitan men

  New Year's Eve could prove to be something of a damp squib for some men in the Italian city of Naples.
  Hundreds of Neapolitan women have pledged to go without sex unless their men promise to refrain from setting off dangerous illegal fireworks.
  Local authorities are backing the women and have sent out text messages urging the men to "make love, not explosions".
  The women say it is the only way to persuade their partners that they are serious about their concerns.

  kwa habari zaidi
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Jan 1, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,182
  Trophy Points: 280
  Ni maamuzi ya mwaka 47 ambayo yameshapitwa na wakati. Ni kuweka ulinzi wa kutosha tu na kuchagua sehemu kubwa Dar na mikoa mingine ambayo inaweza kuhimili umati wa watu na kuamua hapo ndipo sherehe za Mwaka mpya zitafanyika na fataki kupigwa kusherehekea mwaka mpya. Pamoja na kuwa haziruhusiwi lakini bado zinapigwa kinyemela, lakini ukikamatwa ole wako cha moto utakiona.
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Jan 1, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,182
  Trophy Points: 280
  [media]http://www.youtube.com/watch?v=v7UbL4nfeJE[/media]
   
 9. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #9
  Jan 1, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Heri ya mwaka mpya kwa wakulu wote mliokwishauona!
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Jan 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,182
  Trophy Points: 280
  Polisi yalipua mabomu kutuliza upigaji fataki

  na Sitta Tumma, Mwanza
  Tanzania Daima~Sauti ya Watu

  JESHI la Polisi mkoani Mwanza, juzi usiku lililazimika kufyatua mabomu ya machozi kwa baadhi ya maeneo jijini hapa kwa ajili ya kuwatawanya watu waliokuwa wakisherehekea mwaka mpya 2009 kwa kupiga fataki na baruti.

  Sanjari na hayo, jeshi hilo kupitia askari wake lililazimika pia kuwatia mbaroni baadhi ya vijana ambao walionekana kukaidi amri ya jeshi hilo ya kutokulipua baruti wakati wakisherehekea kuuaga na kuupokea mwaka mpya.

  Katika kudhibiti hali hiyo juzi usiku, hususan maeneo ya Igoma, Kirumba, Kitangiri, Kilimahewa, Mabatini, Nyakato na maeneo mengine kadhaa ya jiji la Mwanza, askari polisi waliokuwa doria walipata wakati mgumu kutokana na wananchi kuendelea kulipua baruti hewani.

  Juzi, jeshi hilo kupitia Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Khamis Bhai, ilitoa onyo dhidi ya watu wanaolipua fataki na baruti nyakati za usiku, na kusema ni marufuku kufanya vitendo hivyo.

  Kauli hiyo ya polisi ilionekana kutotekelezwa vema na baadhi ya wakazi wa jiji hilo, kwani watu wengi vijana na wanawake walionekana kuzagaa na kutanda barabarani hususan maeneo ya Igoma hali ambayo iliwalazimu askari polisi hao kufyatua mabomu ya kutoa machozi.

  Kizaazaa hicho kilichukuwa takriban saa mbili kutoka saa 6:00 usiku hadi saa 8 usiku, ambapo polisi walifanikiwa kutuliza hali kama hiyo ya ulipuaji wa fataki kabla ya watu waliokuwa wakihusika na ulipuaji huo wa baruti kuanza kukimbia kukwepa mabomu hayo ya machozi.

  Ofisa mmoja wa polisi mkoani Mwanza aliyeshiriki katika doria hiyo, aliiambia Tanzania Daima kuwa walilazimika kufyatua mabomu hayo ili kudhibiti na kuleta utulivu kwa wananchi wa maeneo husika.

  “Imetubidi kutumia mabomu ya kutoa machozi ili kuwadhibiti watu waliokuwa wakifyatua baruti…..pia tumefanya hivyo kwa kuleta utulivu na kuondoa hofu kwa wananchi waliokuwa majumbani,” alisema.

  Hata hivyo, Tanzania Daima ilishuhudia baadhi ya watu katika maeneo ya Mabatini, Igoma na Nyakato wakiwa wametanda barabarani wakishangilia kuupokea mwaka mpya huku wakiwa na matawi ya miti na wengine wakipiga madebe pasipo kujali onyo la Jeshi la Polisi lililotolewa na jeshi hilo mkoani hapa.
   
Loading...