Kwacha ya Zambia inaipiku shilingi ya Tanzania kwa mbali

Jackal

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
9,539
12,654
Mwaka 2012 nilikuwa Zambia. Shilingi 1 ya Tanzania ilikuwa sawa na Kwacha za Zambia 3.Sasa nipo Zambia Kwacha Moja ni sawa na shilingi 217. Kwa muda wa miaka 4 kumetokea mabadiliko makubwa kabisa dhidi ya Kwacha kuipita pesa yetu. Kuna mtu wa BOT humu atuelezee nini kinaendelea?
 
Mh!ngoja waje ila shilingi yetu nahisi itakuwa imeshuka sana kipindi hiki cha baba j e ssyyyCER!!
 
Unaongelea kwacha ya zambia au malawi? Mmh kweli wamepiga hatua nakumbuka mwaka 2011 nilikwenda kutumia kwacha unabeba nyiingi unapata vitu kidogo. Kumbe pesa imeimarika ghafla hivyo? Hongera zao
 
Unaongelea kwacha ya zambia au malawi? Mmh kweli wamepiga hatua nakumbuka mwaka 2011 nilikwenda kutumia kwacha unabeba nyiingi unapata vitu kidogo. Kumbe pesa imeimarika ghafla hivyo? Hongera zao
Sio yao kuimarika. Ni yetu kushuka..
 
Unaongelea kwacha ya zambia au malawi? Mmh kweli wamepiga hatua nakumbuka mwaka 2011 nilikwenda kutumia kwacha unabeba nyiingi unapata vitu kidogo. Kumbe pesa imeimarika ghafla hivyo? Hongera zao
Kwacha ya Zambia Mkuu
 
Tatizo la namba huwa hazidanganyi aisee huu uchumi unaokua kila siku huku Tz shilling ikizama siuelewi!.Mi sio mtaalamu wa uchumi sana ila itakuwa 'imbalance of trade' sisi tuna 'import' sanaa alafu tuna 'export' kidogo,hiki ni kigezo mojawapo cha kufanya fedha yetu isikue,nashangaa na Uganda wanakuja kwa kasi zamani tuliwazidi sana, 1Tzsh ilikuwa ni 2UGsh mfano, 500Tshs ilikuwa 1000UGshs ila kwa sasa hiyo 500 ya Tz ni saw na 700 hivi ya Uganda wanatupigia indicator wanaomba site uenda nao watatupita siku za usoni tusipo nyiimarisha.
 
Shilingi ishuke tu ili tukuja na pesa zetu kutoka nchi za wenzetu tukienda kuchenchi tuinjoi wallah maan shilling ikipanda tunakuwa hatuna amani huku ishuke hivyo hivyo mipango yetu ikamilike ndukiii
 
Kuimarika au kuwa na sarafu kimara inaweza kuwa either ni matokeo ya intervention yaani vyombo vya fedha hasa benki juu inaamua tu kuhakikisha pesa inakuwa hivyo au ni kuwa wanaingiza fedha za kigeni na uwekezaji wa nje mwingi.
Lakini wakati fulani exchange rates hizi huwa hazipo Sawa. Itakumbukwa Tanzania takribani mwaka na nusu uliopita sarafu iliporomoka kwa sababu the exchange rate was unreal. Benki juu ilikuwa inasaidia exchange rate iwe vile. Nigeria pia mwaka huu hadi wakahamia toka kwenye mfumo wa kucontrol exchange rate na kuruhusu soko kuamua exchange rate. Matokeo yake nchi ikatoka nafasi ya kwanza kuwa uchumi mkubwa ikarudi namba mbili. China pia.
Lakini tuseme wazi, exchange rates si kipimo peke cha uchumi kufanya vizuri.
 
Mwaka 2012 nilikuwa Zambia .Shilingi 1 ya Tanzania ilikuwa sawa na Kwacha za Zambia 3.Sasa nipo Zambia Kwacha Moja ni Sawa na Shilingi 217.Kwa Muda wa miaka 4 Kumetokea mabadiliko makubwa kabisa dhidi ya Kwacha kuipita pesa yetu.Kuna Mtu Wa BOT humu atuelezee nini kinaendelea?
Kwacha iko juu kuliko ZAR?
Wamefanyaje kufika hapo pa kumpita kaburu?
 
Haya mambo ya thamani ya pesa kiulinganisho na uchumi wake mimi huwa yananishanda kabisa kuyahukumu,kwa mfano hapa nimetoka kuangalia pesa ya Mexico,Mexico peso dhidi ya $ 1 = peso 20
$ 1 = Rand 14
$ 1 = Zambian kwacha 9.8

Sasa hapo swali linakuja, inamaana Zambia uchumi wao huko juu sana au nini .......??
 
Mwaka 2012 nilikuwa Zambia .Shilingi 1 ya Tanzania ilikuwa sawa na Kwacha za Zambia 3.Sasa nipo Zambia Kwacha Moja ni Sawa na Shilingi 217.Kwa Muda wa miaka 4 Kumetokea mabadiliko makubwa kabisa dhidi ya Kwacha kuipita pesa yetu.Kuna Mtu Wa BOT humu atuelezee nini kinaendelea?
Ni kweli kabisa pesa yetu shs imekuwa pesa ya ovyo kabisa Imekuwa kama takataka kabisa Kwacha 1 ya malawi = Tshs 3.4 , Kwacha 1 ya Zambia = Tshs220, Rwanda Franc 1 = Tshs 2.7, Burundi currency 1 = Tshs 1.3.

kwa maana nyingine zambia kwacha 1,000,0000 ni sawa na Tanzania shs 220,000,000 jamani hata Burundi? ama kweli?

HAPA KAZI TU : ETI NA UCHUMI WETU UNAPANDA ZAIDI YA 7.5% KULIKO NCHI ZA EAST AFRICA.
 
Haya mambo ya thamani ya pesa kiulinganisho na uchumi wake mimi huwa yananishanda kabisa kuyahukumu,kwa mfano hapa nimetoka kuangalia pesa ya Mexico,Mexico peso dhidi ya $ 1 = peso 20
$ 1 = Rand 14
$ 1 = Zambian kwacha 9.8

Sasa hapo swali linakuja, inamaana Zambia uchumi wao huko juu sana au nini .......??

Wewe unaelewa lakini?. Thamani ya pesa ina maana sana katika uchumi wa nchi husika maana yake ni kwamba katika masoko ya kimataifa Nchi yenye pesa dhaifu inahitaji pesa nyingi sana za kigeni ili kuweza kununua bidhaa kama matawa, mafuta nk. Na thamani ya pesa zote zinawekwa na masoko na mabenki ya kimataifa kulingana na Import and export of goods ukilinganishwa na dhamani ya $ na pesa ya nchi kwa mfano $1=Tsh 2180 na $1=kwacha 9.8 kwa maana hii 2180tshs gawanya kwa kwacha 9.8 = na thamani ya Tshs to Kwacha ambayo ni shs 222.44 kwa Kwacha 1.(hii ni hatari sana kwa biashara baina ya nchi na nchi kwa maana hii wale wa Tunduma watahitaji malundo ya manoti ili kununu bidhaa kiduchu kutoka Zambia).

Kwa mfano: kama zambia na Tanzania tutakwenda kununua dawa marekani ya US $ 100,000 zambia watalipa na exchange rate $ 1 = 9.8 na US $ 1= Tshs 2,180. Maana yake sisi tutahitaji kutafuta $ nyingi zaidi kuliko Zambia.
 
Mwaka 2012 nilikuwa Zambia. Shilingi 1 ya Tanzania ilikuwa sawa na Kwacha za Zambia 3.Sasa nipo Zambia Kwacha Moja ni sawa na shilingi 217. Kwa muda wa miaka 4 kumetokea mabadiliko makubwa kabisa dhidi ya Kwacha kuipita pesa yetu. Kuna mtu wa BOT humu atuelezee nini kinaendelea?
Mkuu huo ni uongo kabisa utakua umeibiwa
 
Ni kweli kabisa pesa yetu shs imekuwa pesa ya ovyo kabisa Imekuwa kama takataka kabisa Kwacha 1 ya malawi = Tshs 3.4 , Kwacha 1 ya Zambia = Tshs220, Rwanda Franc 1 = Tshs 2.7, Burundi currency 1 = Tshs 1.3.

kwa maana nyingine zambia kwacha 1,000,0000 ni sawa na Tanzania shs 220,000,000 jamani hata Burundi? ama kweli?

HAPA KAZI TU : ETI NA UCHUMI WETU UNAPANDA ZAIDI YA 7.5% KULIKO NCHI ZA EAST AFRICA.
Hebu acheni kutudanganya wenye akili msikurupuke
 
Inawezekana kwa sababu bila kusahau sata alipoingia madarakani niliskia kuwa amepunguza tarakimu za noti zake yaani walikua na hadi 50,000 kwacha ambayo sasa imekua 5000 nadhani inaweza kuwa sababu.
 
Mwaka 2012 nilikuwa Zambia. Shilingi 1 ya Tanzania ilikuwa sawa na Kwacha za Zambia 3.Sasa nipo Zambia Kwacha Moja ni sawa na shilingi 217. Kwa muda wa miaka 4 kumetokea mabadiliko makubwa kabisa dhidi ya Kwacha kuipita pesa yetu. Kuna mtu wa BOT humu atuelezee nini kinaendelea?
We upo mbalizi usitudanganye au chunya unachunga mbuzi usitudanganye!
 
Back
Top Bottom