Kwacha ya Zambia ilikuwa dhaifu dhidi ya shilingi ya Tanzania. Imekuwaje kwa sasa Kwacha ipo juu sana zaidi ya shilingi yetu?

Wewe nawe acha ujinga. Ni kweli 1 Kwacha ni TZS 170....sasa 170 Tanzania inanunua andazi si ndio?....hiyo kwacha moja kule Zambia haina issue huwezi pata chochote.

Yaani iko hivi....chupa ya bia ni Kwacha 100. Badili iwe Shiliningi. Ina maana ni 100*170 sawa na Sh. 17,000.....je? Bei ya bia Tanzania ni sh 17,000?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa Mzambia mwanauchumi!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nashindwa hata niongeaje yaani. Kwa ufupi kwacha 1 ina thamani ya shilingi 170. Hizo story za kupunguza masifuri ni irrelevant.
mkuu siyo irrelevant ukweki ni kwamba hiyo figure ya kwacha unayoiongelea izidishe mara1000 ndio thamani halisi ya kwacha. Waliibadilsha kuepuka kubeba mafurushi ya noti ili kununua hata mkate tu
 
Muda mwingine thamani ya pesa ni purchasing power take, hapa namaanisha kitu sh 170 ya Bongo inaweza kununua vitu sawa na yule mwenye Kwacha 100 huko Zambia. Kwa mfano sh 170 unapata chumvi robo kilo, je Kwacha 100 unapata chumvi robo huko Zambia?
Tuanzie hapo kwanza kwa simple logic za uchumi

Hit direct to the Ntonku
Kwacha 180 unanunua kilo 25 ya unga wa ugali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka ya 2004 hadi 2006 nilikuwa nikipita mara kwa mara Zambia kuelekea South Africa. Nilikuwa nikibadilisha shilingi yetu kwa kwacha ya Zambia napata hela nyingi sana za Kizambia.

Infact enzi hizo ukiwa na TZS unakuwa don kwa maisha ya Zambia. Nimeshangaa leo hapa mitaa ya Posta nakuta exchange rate ya Kwacha ni TZS100 - TZS170.

Yaani Kwacha 1 inanunuliwa kwa TZS100 na kuuzwa kwa TZS 170. Nimebaki kujiuliza sana imekuwaje Kwacha ilikuwa weak hivyo lakini imeipita TZS zaidi ya asilimia 1000?

Tanzania tunakwama wapi jamani? Dar es salaam huwezi hata kuilinganisha na Lusaka. Jiji la Dar lipo juu sana ukililinganisha na Lusaka.

Miji Kama Mwanza, Arusha iko juu sana ukilinganisha na miji ya Zambia. How come currency ya Zambia ipo juu kuizidi TZS?

Wachumi naomba mtufafanulie.

By the way mimi pia ni mchumi japo sio certified hivyo basic principles za economics nazijua, ila kwa hili nimeshindwa kulielewa.

Karibu tujadili.


Pesa yetu itapungua thamani endapo bidhaa zinazotumika humu nchini tunaagiza zaidi nje ya nchi zaidi ya tunavyozalisha.

Zaidi fanya rejeo la bandiko langu Depreciation of tanzania shilling, are policy makers still asleep?
 
Mkuu swali ni kwamba "Kwa nini kwacha ipo juu zaidi ya TZS?" Hili swali linajibika kiuchumi zaidi na sio kiuhasibu. Kuhusu kuingiza issue za international finance ni kuwaonyesha tu wale wanaong'ang'ania kusema kwacha ina nguvu kuliko TZS wakati hata dakika hii ukienda kuinunua kwacha utakuta inauzwa kwa sh.170. So issue sio kwamba ipi ni strong against the other but the question is why kwacha is stronger than TZS while a few years back TZS was stronger than Kwacha.
Jibu ni rahisi tu currency ya Zambia, Kwacha imeipita thamani Tsh acheni kupiga ramli sisi korosho mauzo kwishney, Tumbaku tulishaharibu kitambo, mbaazi ndio usiseme halafu hyo akiba ya fedha za kigeni itatoka wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muda mwingine thamani ya pesa ni purchasing power take, hapa namaanisha kitu sh 170 ya Bongo inaweza kununua vitu sawa na yule mwenye Kwacha 100 huko Zambia. Kwa mfano sh 170 unapata chumvi robo kilo, je Kwacha 100 unapata chumvi robo huko Zambia?
Tuanzie hapo kwanza kwa simple logic za uchumi

Hit direct to the Ntonku
Acha uongo kwacha 100 ya Zambia sawa na 15000 sh, haishuki hapo Jana tu nimeuza kwacha 600 nimepata sh 99000, japo inapanda na kushuka Kama dollar tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iko ivi ukiwa na Zambian kwacha moja (1) ni sawa na kuwa na tanzanian shilings mia moja na sabini (170) kwa upande wa dola ya marekani ukiwa na US dolar moja (1) ni sawa na kuwa na tanzania shilings elfu mbili mia tatu na kumi na tano (2315) kwa upande wa majirani zetu wa kenya ukiwa na kenyan shiling moja (1) ni sawa na kuwa na tanzania shiling ishirini na tatu (23) natumaini unaweza kuona nguvu ya kwacha ya zambia.
Mimi naishi tunduma kwacha Ina thamani kuliko shilingi tukubari tukatae maana kwacha 1 upata sh 165 kwa bei ya Jana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu anakujibu vizuri unamtolea kashfa ilihali umekuja jukwaani kuomba ufafanuzi. Hii sio sawa. Nikirudi kwenye swali lako ufafanuzi ni kwamba sio kweli kwamba pesa ya Zambia ina thamani kuliko Shilingi yetu.

Kama ambavyo wengi wamekujibu ni kwamba pesa ya Zambia imefanyiwa mabadiliko hasa katika uandishi wa tarakimu.

Walichokifanya wameondoa wingi wa sifuri ili kujaribu angalau kuifanya irudi kwenye thamani. Ukitaka uelewe ninachokimaanisha, nenda na pesa za thamani sawa sokoni, kisha fanya manunuzi ya aina moja kwa pesa zote mbili.

Mfano, chukua elfu 10 ya Tanzania, kanunue mbolea, kisha chukua Kwacha yenye thamani hiyo hiyo nunua mbolea. Ukikabidhiwa mzigo wako, utapata jibu kwamba purchasing power ya Shilingi ya Tanzania ni kubwa kuliko Kwacha ya Zambia..na hivyo ndivyo thamani ya pesa hupimwa.

Ukweli ni kwamba, Ile noti ya Kwacha 1000 ya sasa ina thamani ya Kwacha 100,000. Kilichobadilika ni kuondolewa kwa 000 za mwisho. Tunaokwenda huko kwao kununua bidhaa jamaa wakikuona una Shilingi ya Tanzania wanataka ununue bidhaa zao kwa hiyo pesa. Wao wenyewe hawaithamini kabisa pesa yao.



Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini unakataa kuwa pesa yao imepanda thamani au wameipandisha thamani.ishu ni kwamba Zambia noti yao kubwa ni 100.haina ubishi.na ukiitaka hiyo 100 yao ni lazima zikutoke elfu kumi na saba mpk kumi na nane za Kitanzania,ni lazima tukubali kuwa pesa yao imepanda thamani ata kama tutakuwa na uchumi mkubwa kuliko wao.ni sawa na kwacha ya Malawi nayo pia ipo juu kuliko shilingi yetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Chige msaada wako tafadhali.
Duh! Hii post ni ya kitambo sana!!

Anyway, suala la Kwacha ya Zambia lipo wazi kabisa... linategemeana sana na bei ya Shaba kwenye Soko la Dunia!

Mleta dau amesema back in mid-2000's, ukiwa na shilingi ya Tanzania, alikuwa anapata Kwacha za kumwaga wakati hivi sasa tunalazimika kuachia shilingi za kumwaga kwa Kwacha ile ile!!!

Kimsingi, thamani ya Kwacha ya Zambia (ZMK) inakuwa influenced sana bei ya shaba kwenye soko la dunia! Aidha, tukumbuke pia kabla ya mambo ya Trade Liberation, mataifa mengi yalikuwa yana-set thamani ya pesa yao FIXED.

Sasa tukija upande wa ZMK, miaka ya 80 kulikuwa na oversupply ya shaba duniani na matokeo yake bei ikashuka vibaya mno!! Kwahiyo kipindi hicho, ZMK nayo ikaanza kuyumba.

Miaka ya 90, bei ya shaba ikaimarika lakini ilikuja kuimarika wakati uchumi wa Zambia umeyumba sana, na inflation kuwa juu kutokana na msuko suko wa bei ya shaba miaka ya 80. Kwa maana nyingine, kupanda kwa bei ya shaba hakukuisaidia ZMK; na sana sana ZMK ndo kwanza ikaendelea kuyumba kutokana na high inflation.

Ingawaje bei ya shaba mwanzoni mwa miaka ya 90 iliimarika lakini ukiangalia historical data za global copper price, utaona kati kati ya miaka ya 90 bei ya shaba ikaanza tena kuporomoka na hii ikaanza kupanda hadi mwaka 2005, na ikaanza kupanda tena kuanzia hapo!

Sasa ukiangalia taarifa ya mleta mada, anazungumzia kuvuna ZMK nyingi zaidi per shilingi kipindi ambacho bei ya shaba iliyumba sana! Na kwavile bei ya shaba ilikuwa chini sana, ikaathiri hadi thamani ya ZMK!

Na ukifuatilia historia ya ZMK, utaona ni kipindi hicho pia Zambia walianza kuchapisha manoti makubwa makubwa (denomination) ya ZMK kwa sababu thamani yake ilishuka sana!!

Na ingawaje kuanzia kati kati ya miaka ya 2000 bei ya shaba ilizanza kuimarika tena, lakini bado ilishindwa ku-offset damage ya miaka ya 80 iliyotokana na kuyumba kwa bei ya shaba, na ile ya kati kati ya miaka ya 90 ambayo ilisababishwa na high inflation (iliyotokana na miaka ya 80) na pia kushuka tena kwa bei ya shaba!

Matokeo yake, ndo maana haishangazi kumsikia Mleta Mada kwamba bado aliendelea kuvuna ZMK za kutosha hadi miaka ya 2006 kwa sababu bado ilikuwa haija-stabilize!!

Kinyume ha hayo, ukiangalia historical data za bei ya shaba kwa miaka 10 uliyopita, utaona ni mwanzoni mwa mwaka 2016 ndipo bei ya shaba ilishuka na kufikia takribani $2/lb. Hicho ndo kiwango cha chini kabisa over the past 10 years wakati ile miaka niliyosema shaba ilishuka sana, ilikuwa inacheza kwenye $1/lb.

Kwa maana nyingine, bei ya shaba imeonekana kuwa mzuri zaidi kwa miaka kadhaa sasa, na hivyo haishangazi kuona ZMK nayo imeimarika!

Na tusahau, kadri construction boom inavyoongezeka, demand for copper na yenyewe inaongezeka! Na kwa ujumla, copper ni metaliki ya 3 kwa kutumika zaidi duniani! Soko la uhakika la shaba limeshathibitisha kuimarisha ZMK; na kwahiyo tena, tusishangae kulipa shilingi kadhaa kwa Kwacha moja!
 
Thamani ya pesa ni uwezo wake wa kununua(purchasing power).

Tukitaka kumaliza huu ubishano tujikite kwenye uwezo wa kununua(purchasing power) kati ya kwacha ya zambia na Tsh.

Mfano nikienda lusaka leo nikatumia noti ya elfu kumi ya Tanzania nikanunua vitu bila ya kuibadilisha, hapo hapo nikatoa kwacha 60 ambayo kwa exchange rate ni sawa na Tsh 10,000.

Jee ni ipi itanunua vitu vingi
Kati ya kwacha 60 na Tsh 10,000.

Likijibiwa hili swali basi mjadala utaisha.

Ni hayo tu kwa sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo 60 ongeza sifur 3 ndio upime
 
Kwanza habari yako is pure speculation, unaleta habari za 2011, almost 9 years ago, yani kama ni mtoto alizaliwa kipindi hicho yupo darasa LA 3 au LA 4, moreover, Kwacha INA value and higher purchasing power kuliko hela ya Tanzania au ya Kenya, hilo sitaendelea kukuelimisha zaidi sababu kama wewe ni MTU mzima na bado unashindwa kuelewa hizi basics nikusaidieje? Kama unaamini kwacha wamepunguza zero wakati kwacha moja Leo hii inanunua dola 13, nikusaidiaje with all that information? Sisi kwa ufupu tu hatu export zaidi kama Zambia, pesa yao ina nguvu, suala LA kwamba uchumi wao ni bora kuliko wetu or vice versa hiyo ni discussion nyingine sababu pesa yako kuwa na nguvu sio kipimo pekee una uchumi Mkubwa, ila Kwa ufupi tu Zambia pesa yao INA nguvu kuliko yetu, that's a universal truth sina sababu ya kubishana na facts au MTU anaepingana na facts wakati haya mambo unaweza hata google kuona kwacha na shilling ipi INA nguvu.
Mzee unapata wapi nguvu ya kushindanisha uchumi wa Tanzania na Zambia? Kwa kifupi Zambia ni moja ya nchi ambayo ipo hoi kuichumi, ni bahati nzuri nimeishi sana kitwe miaka ya 2017, Tanzania ni nchi inayofanya vizuri kwenye suala la uchumi.
Screenshot_20210507-192436_Chrome.jpg
Screenshot_20210507-192551_Chrome.jpg

Hapo nimejaribu kuweka comparison in all aspects, so far Tanzania inazalisha idadi ya mamilionea wapya wengi east africa kutokana na shughuri za kiuchumi.
 
Back
Top Bottom