Kwacha ya Zambia ilikuwa dhaifu dhidi ya shilingi ya Tanzania. Imekuwaje kwa sasa Kwacha ipo juu sana zaidi ya shilingi yetu?

Msukuma Original

JF-Expert Member
Oct 2, 2018
928
3,330
Miaka ya 2004 hadi 2006 nilikuwa nikipita mara kwa mara Zambia kuelekea South Africa. Nilikuwa nikibadilisha shilingi yetu kwa kwacha ya Zambia napata hela nyingi sana za Kizambia.

Infact enzi hizo ukiwa na TZS unakuwa don kwa maisha ya Zambia. Nimeshangaa leo hapa mitaa ya Posta nakuta exchange rate ya Kwacha ni TZS100 - TZS170.

Yaani Kwacha 1 inanunuliwa kwa TZS100 na kuuzwa kwa TZS 170. Nimebaki kujiuliza sana imekuwaje Kwacha ilikuwa weak hivyo lakini imeipita TZS zaidi ya asilimia 1000?

Tanzania tunakwama wapi jamani? Dar es salaam huwezi hata kuilinganisha na Lusaka. Jiji la Dar lipo juu sana ukililinganisha na Lusaka.

Miji Kama Mwanza, Arusha iko juu sana ukilinganisha na miji ya Zambia. How come currency ya Zambia ipo juu kuizidi TZS?

Wachumi naomba mtufafanulie.

By the way mimi pia ni mchumi japo sio certified hivyo basic principles za economics nazijua, ila kwa hili nimeshindwa kulielewa.

Karibu tujadili.


 
Muda mwingine thamani ya pesa ni purchasing power take, hapa namaanisha kitu sh 170 ya Bongo inaweza kununua vitu sawa na yule mwenye Kwacha 100 huko Zambia. Kwa mfano sh 170 unapata chumvi robo kilo, je Kwacha 100 unapata chumvi robo huko Zambia?
Tuanzie hapo kwanza kwa simple logic za uchumi

Hit direct to the Ntonku
Iko ivi ukiwa na Zambian kwacha moja (1) ni sawa na kuwa na tanzanian shilings mia moja na sabini (170) kwa upande wa dola ya marekani ukiwa na US dolar moja (1) ni sawa na kuwa na tanzania shilings elfu mbili mia tatu na kumi na tano (2315) kwa upande wa majirani zetu wa kenya ukiwa na kenyan shiling moja (1) ni sawa na kuwa na tanzania shiling ishirini na tatu (23) natumaini unaweza kuona nguvu ya kwacha ya zambia.
 
Mkuu nashindwa hata niongeaje yaani. Kwa ufupi kwacha 1 ina thamani ya shilingi 170. Hizo story za kupunguza masifuri ni irrelevant.

Sasa kwa kutoelewa kwako ndo tatizo lile jina uliloniita mimi. Na pengine haya mambo yako nje ya uwezo wako. Ungekua unaelewa hicho nilichokuwekea kuwa wanapunguza sifuri ila thamani ni ile ile ungeelwwa kuwa hio 170/180 tunayonunulia pale Kazungula ina thamani gani
 
Sasa kwa kutoelewa kwako ndo tatizo lile jina uliloniita mimi. Na pengine haya mambo yako nje ya uwezo wako. Ungekua unaelewa hicho nilichokuwekea kuwa wanapunguza sifuri ila thamani ni ile ile ungeelwwa kuwa hio 170/180 tunayonunulia pale Kazungula ina thamani gani
Mkuu miaka ya nyuma shilingi ilikuwa na nguvu kuzidi kwacha lakini kwa sasa imekuwa kinyume. Hiki ndio msingi wa hili bandiko. So unachoongea wewe kipo nje ya bandiko. Au wewe hujui kuwa kwacha ilikuwa dhaifu dhidi ya shilingi lakini sasa kwacha ina nguvu zaidi ya shilingi?
 
Tuko katika raiti traki
Screenshot_2019-12-21-17-45-45.jpeg
Screenshot_2019-12-21-17-45-03.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom