Kwa yote utakayofanya, wewe ndie muhusika mkuu kwa asilimia mia moja, juu ya maamuzi yako utakayoyatoa

Nov 2, 2020
68
90
Hakuna atakayekuja chumbani au mezani kisha akakulazimisha kuelewa unayojifunza darasani kwa ngazi yeyote uliyopo.

Vema ukajitambua aina ya usomaji ulionao ,Kwa maana ni kwa njia ipi unaitumia ili kuelewa yale unayojisomea.

Kuna mtu uelewa kwa kusikiliza,mwingine kwa kupitia discussion au yupo anayetumia njia ya kujisemesha mwenyewe kile anachojisomea kwa wakati huo.

Yote kwa yote unalo jukumu la kujisomea kwa nguvu na ari zote.

Kabla ya kusoma,Vema ukafanya jambo moja kwa wakati mmoja,Ikiwa umeamua kusoma mezani,Fanya hilo hilo moja na si kuchanganya na vitu au mambo mengine.

Muda wa kusoma uwe ni wa kusoma, Na muda wa kuchat na kuchezea simu uwe ni mwingine.

Tenganisha muda wa kupiga soga na marafiki na muda wa kujisomea,Usiige kila afanyacho rafiki yako nawe ukifanye hicho,Kumbuka kila mtu amekuja hapo kwa sababu zake.

Ili kuhakikisha unafikia malengo ,Vizuri kuwa nayo malengo hayo,mfano kurekebisha GPA,Kupata scholarship ,Au kusaidia jamii unayotoka na mfano wake.

Malengo haya yakuumize kila siku uamkapo na kila unapohisi uvivu wa kutojisomea au kuhudhuria masomo.

Kwa yote utakayofanya,Wewe ndie muhusika mkuu kwa asilimia mia moja, Juu ya maamuzi yako utakayoyatoa.

Anza leo.

Youth Worker

Hardness ,Teaches
 
Kuna msemo mmoja ambao una umuhimu sana katika maisha ya mwanadamu

"Hakuna mtu atakuwa na wajibu na maisha yako ila wewe mwenyewe ndio mwenye wajibu na maisha yako kwaiyo hata unaowategema wawe na wajibu na maisha yako watafika mahali watatoweka"
 
Back
Top Bottom