Kwa yeyote mwenye kibarua mimi nipo tayari kufanya naombeni msaada wenu

Maji Chai

JF-Expert Member
Dec 8, 2018
243
319
Maisha ni fumbo,fumbo ambalo linahitaji kufumbuliwa, wachache wameweza kulifumbua fumbo hili sasahivi wanakula kuku kwa mrija kama wengine wasemavvyo. Mimi ni miungoni mwa wale ambao tumeshindwa kulifumbua fumbo la maisha na kuishia kusindikiza wengine kama dunia hii iliyojaa shida.

Kiukweli natamani maisha yangu yote yangekuwa kama ndoto tu ili nikishtuka nijiandae niende shule maana maana nshaona nkicheza na elimu nkitoka bila hata cheti cha darasa la 7 kazi za ulinzi pia ntakosa.

Miaka sita bila kazi ya maana ilinichosha ikabidi nikaombe mtaji kwa ndugu yangu mmoja tunaye heshimiana sana ili nianze biashara nisogeze maisha mbele ila mpka sasa huo mtaji sina na biashara ishakufa.

Ulimwengu wa biashara unahitaji mengi nakumbuka siku ya kwanza nmeanza ile kazi nliambiwa 'be carefull' sikutilia maanani nmejua alikuwa anamaanisha nini sasa.

Wapendwa sina mengi ya kusema nkipata muda nitakuja kuelezea safari yangu kwenye hiui biashara niliyoifanya kwa miezi mitatu nkakumbana na misukosuko nkapoteza mtaji.

Kwasasa napambana kutafuta kazi yoyote ile hapa Dar ili niweze kupata pesa ya kulipa deni langu.Kwa yeyote mwenye kibarua mimi nipo tayari kufanya naombeni msaada wenu
 
Be patience ur time is come keep prayers to the Almighty God to him nothing Imposssible ✍️🙏
 
Back
Top Bottom