Kwa yeyote anaejua kutafsiri ndoto anisaidie tafadhali.

duuh, kumbe shehe yahaya hakuacha pengo.....yale maneno ya kuwa eti pengo lake halitazibika ilikuwa ni uongo.....


Kuota uko na ex wako maana yake utarudi nyuma kimaendeleo, angalia sana assets zako.
Kuota uko porini maana yake utapotea, angalia sana mienendo yako.



Simba ni alama ya vita na nguvu, angalia sana kuna kishindo cha nguvu cha upinzani kitakufuata.



Hata hivyo, haya matatizo yatakayokuja yatakuwa ni "blessing in disguise" kwani yatakutoa katika matatizo yako mengine ya kurudi nyuma kimaendeleo.



Matatizo yako ya kurudi nyuma kimaendeleo yatashindwa nguvu na hii nguvu mpya itakayojitokeza.



Matatizo yako yatakushawishi lakini hutaweza hata kuyarudia tena.



Ukija kupita experience hii naomba urudi hapa kueleza usahihi wa tafsiri yangu.
 
Du!Bonge la tafsri.Halafu hizi ndoto wakati mwingine zinakera sana.Nakumbuka siku moja niliota niko uchi mtaani.Nilipozinduka usingizini kwanza nilishukuru kwamba kumbe ni ndoto tu,lakini pia nilikasirika sana!
hii iliasiriaa kupata aibu kubwaaa mtaani,yani ukashushaa heshima yako hakunaa jambo lililotokea tuweke wazi
 
nadhani ww utakuja kumsaliti mpenzi wako, afu yeye atampata mwingine atakaemtesa na kumwachia maradhi atakuwa akikulaumu sana kwa kumsababishia yote hayo. shutka sasa ulie nae mpende na mjali
 
hii iliasiriaa kupata aibu kubwaaa mtaani,yani ukashushaa heshima yako hakunaa jambo lililotokea tuweke wazi

Aisee nimekumbuka.Inawezekana kuwa kweli mkuu.Wakati huohuo kuna jambo la aibu kidogo lililnitokea.Haikuwa mtaani ila ilikuwa kazini.Nakumbuka kuna issue nilicheza bosi akashtukia.Itakuwa ni hiyohiyo!Aisee umenifumbua macho.
 
Ndoto ni moja tafsiri kibao! Aamini ipi? Mnamchanganya tu. Kwanza ajitazame ana historia ya kuotaota na ikatokea kweli? Manake nachojua ndoto za ukweli zina wenyewe, wengine tukila tukishiba sana ndipo ndoto zinatokea kwa mbaali, kama jamaa hana historia na ndoto, piga chini, dont waste ur time man.
 
Daa Mambo ya Ndoto acheni kuna siku niliota mwisho wa Dunia umefika palapanda inalia malaika wanashuka toka mbinguni nkaanguka kilio nakuanza kusali na kulia yesu gafla nikastuka yan nilishukuru ilikuwa ndoto ila nlipata somo langu.
 
Kweli maisha yanatofaytiana, hivi na hali hii ngumu aliyotusababishia kikwete bado mnalala mpk mnaota! Mi nikilala tu kesho yake sili
 
Kweli maisha yanatofaytiana, hivi na hali hii ngumu aliyotusababishia kikwete bado mnalala mpk mnaota! Mi nikilala tu kesho yake sili

sasa mkuu,kulala ndo starehe pekee ilyobaki,maana ukisema ukalewe bar,pesa huna,so ni bora mtu ujilalie zako tu ili kuconcerve energy.
 
Wakati mwingine ndoto hutokana na kile unachowaza kila mara kwa muda wa mchana.Kwa ndoto yako take care bro UKO VITANI, jaribu kuwa mwanamaombi Mungu atakuwa anakupa majibu ya ndoto zako.
 
Ndoto ni bayana. Ukiota ndoto yoyote uiandike siku moja itatokea hivyohivyo. Ndoto hii ina maana nzuri sana kama mtaalam alivyoitafsiri lakini atapitia kwenye shida kidogo na mwisho wake utakuwa mzuri. Nakushauri ufanye maombi sana.
 
Mtu ye yote akuleteaye tafsiri anafanya guesswork tu, maana tafsiri za ndoto hazina msingi wa kisayansi, huwezi kamwe kuwa na uhakiki tafsiri fulani ni sahihi. Lakini, guesswork yaweza kuwa accurate kama yule mtu anakufahamu vizuri, kwani kinachoonekana ndotoni maana yake ni subjective (yaani yaweza kuwa na maana mbali mbali kulingana na watu). Wewe ndiye mwenye kujijua vizuri kushinda mtu yeyote (si ndio?), basi wewe ni mwenye uwezo wa kutafsiri ndoto zako vizuri kuliko mtu yeyote pia. Kwa hiyo nafikiri kwamba, badala ya kungoja tu "mtaalamu" akuletee tafsiri, ni bora wewe wenyewe utafakari juu ya hili. Ni sababu gani inayoweza kukufanya uwe na ndoto hii? Bado unampenda ex wako? Unaogopa kufiwa na mtu upendao sana? Unajisikia hatia maana mtu alijeruhiwa kwa sababu yako? Kuna maswali mengi yatakayokusaidia kuona mambo kwa uwazi zaidi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom