Kwa yanayoendelea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Watanzania tumelala sana

Kifurukutu

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
4,525
6,472
Habari wakuu,

Kwa yanayoendelea sasa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni ishara tosha kuwa Watanzania bado tuko usingizini na hakuna dalili yoyote ile inayoashiria kutoka usingizini.

Upinzani wa nchi hii ndio bure kabisa, yaani haiwezekani majina ya wagombea wawakilishi wa vyama vya upinzani wanakatwa hivihivi pasipo kuchukua hatua kali dhidi ya ubakaji huu wa sheria.

Ni muda rasmi sasa, Watanzania na wapinzani wote tuamke na tupinge wazi wazi vitendo vinavyofanywa na serikali kupitisha wagombea wa CCM tu.

Tuungane, na tuandamane pamoja barabara zote, kila mkoa kupinga ubinywaji huu wa demokrasia nchini.

Daniel Agger
 
Hatuhitaji kuandamana tena! Sasa hivi ni tunakimbiza mwizi kimya kimya!!//tukimkamata ni halali yetu
 
Wapinzani walikuwa wanahamasisha watu wasijiandikishe kwenye daftari la wapiga kura
Leo hii wanachukua fomu za kugombea uongozi

Wapinzani msitufanye sisi mandondocha
 
Hawa ni viumbe wa ajabu sana

Sasa wanategemea nani atawachagua wakati wao walizuia wanachama wao kujiandikisha?

Hapo wasingesimamisha hata wagombea, wagomee kila kitu
 
Wapinzani walikuwa wanahamasisha watu wasijiandikishe kwenye daftari la wapiga kura
Leo hii wanachukua fomu za kugombea uongozi

Wapinzani msitufanye sisi mandondocha
mpinzani gani alihamasisha watu wasijiandikishe, weka ushahidi hapa.

na je hilo linahusiana vipi na haya yanayoendelea; ?
 
Habari wakuu,

Kwa yanayoendelea sasa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni ishara tosha kuwa Watanzania bado tuko usingizini na hakuna dalili yoyote ile inayoashiria kutoka usingizini.

Upinzani wa nchi hii ndio bure kabisa, yaani haiwezekani majina ya wagombea wawakilishi wa vyama vya upinzani wanakatwa hivihivi pasipo kuchukua hatua kali dhidi ya ubakaji huu wa sheria.

Ni muda rasmi sasa, Watanzania na wapinzani wote tuamke na tupinge wazi wazi vitendo vinavyofanywa na serikali kupitisha wagombea wa CCM tu.

Tuungane, na tuandamane pamoja barabara zote, kila mkoa kupinga ubinywaji huu wa demokrasia nchini.

Daniel Agger

Lowasa Oyeee
 
Toba. Jamani mimi natamani hawa jamaa waingie barabarani maana huo ndio uwanja uliobaki pekeyake kujinusuru na sisi tumemisi sana kuona live sinema za mikong'oto. Jamani ingieni fasta na muda ndiyo huu mkichelewa hapo mtakuwa mafara sasa. Nahimiza.
Maana juzi nimeona magari ya washa washa yanazima moto na kusafisha barabara yaani hayana kazi hamsheni dude jamani mmezalilishwa sana imetosha makamanda tuwaone.
 
Back
Top Bottom