Kwa yanayoendelea nchini bado tunajiuliza wasiojulikana ni akina nani?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Ukiona binadamu wanavyoshuhudia mahakamani kwa kuandika stori zisizo na muunganiko huitaji kuuliza wasiojuikana ni wakina Nani, nadhani ikiwa mtu anaweza kuja adharani akasimama nakusema ulifanya hivi na hukufanya basi mtu huyo ana chuki na ana roho ya kukua. Wapo watu wanarithi laana za wazazi wao maana haiwezekani matendo ya baba yafanywe na mtoto Tena kwenye jamii ambayo ulikuwepo uwezekano wa huyo mtoto kutokufanya.

Ukimsikiliza Sabaya anakiri alikuwa na nguvu yakutembea nchi nzima kufanya kazi alizokuwa anatumwa na wakubwa zake. Lakini nenda kwenye majukumu ya DC huone Kama alichokuwa anafanya anaruhusiwa kukifanya. Means wasiojulikana walikuwa watu wanaojulikana na ambao wanabeba vitabu vitakatifu nakushuhudia wakiwa na roho unaweza kudhani ni roho wa Bwana.

Leo wanajitokeza watoto wetu mahakamani unakiuliza analipwa Nini au alilipwa Nini Hadi awe sehemu ya uhalifu huu? Jibu Ni kwamba tumeamua kutengeneza kundi la watu wasiofuata sheria, matokeo yake hawa tunaowana wanaisaidia Jamhuri ipo siku watatamani kuwa ma IGP, Director wa maeneo nyeti, kuwa DC nk. Kipindi kwa sababu watakuwa wamezaliana na kukuwa kwenye mfumo tusishangae wakawa sehemu ya mapinduzi.

Lakini pia Hawa watoto wenye miaka 35- wanaoweza kufanya kazi popote na Viongozi wao wasiseme chochote kwa kuogopa kutumbuliwa ipo siku watahukosea utawala, watafukuzwa au kufungwa Kama Sabaya. Wakiwa uraiani na kwakuzingatia mambo waliyokwisha kufanya watatengeneza upinzi binafsi au kutafuta pakukimbilia, tuombe wasiangukie Miko mibaya kwenye mataifa jirani.

Leowapo vijna wanatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo Rushwa lakini awapelekwi mahkamani kwa sababu waliwahi kuishi Kama wasiojulikana huko nyuma,tunaogopa wakaenda kutaja waliokuwa wanawatumia Kama Sabaya alivyodiriki kuwataja adharani waliokuwa wanamtuma.

Tulichrkelea walipoitwa wasiojulikana, Sasa hivi mfumo umewaacha wanaangaiaka kuthibitisha matendo yao gizani. Wasiojulikana ndio Hawa hawatunaosikia walikuwa wanaweza kuzunguka nchi nzima kufanya kazi wakati kila eneo watu wapo. Hawa ukiwasikiliza hakuna mahali unaweza kusema wana utaalam wa ziada. Lakini fuatilia ukwasi waliona then jiulize haya mabilioni wanayatoa wapi angali mishahara yao midogo?

Damu za wakiana saanane zinalia na watu na kadri siku zinavyokwenda tutabaini wale wote wenye vinasaba vya wasiojulikana.

Viongozi wa dini mlikaa kimya kipindi wanaumiza watu, leo hii endeleeni kukaa kimya. Mwisho, ukitaka kujua binadamu tumejawa tamaa na roho za kikatili fuatilia sifa alizopewa Maalim Seif Jana then angalia waliokuwa wanamsifia Jana akiwa hayupo Duniani walimfanya Nini alipokuwa hai. Tumemwacha Mungu tumeambatana na uchu wa madaraka na unafiki.
 
Ni ukweli mchungu lakini ndo uhalisia. Usimwamini MTU hata aweje, dunia ishageuka kisanga wa karibu yako na umwaminiye ndiye kaburi lako la baadaye
 
Watu siasa zinawashinda wanaamua kulazimisha kwa kufanya ugaidi

Madhara ya kupenda sana madaraka ndio haya.
 
Watu siasa zinawashinda wanaamua kulazimisha kwa kufanya ugaidi

Madhara ya kupenda sana madaraka ndio haya.
Unamzungumzia Shujaa? Maana yule ndo siasa ilimpitia kushoto kabisa ilikua ni mwendo wa MKONO WA CHUMA tu.
 
Halafu watu kutojukana inapaswa kuwa mwanzoni kwa muda mfupi lakini baada ya muda wanapaswa wawe wamejukana baada ya uchunguzi n.k.

Sasa je, matukio mazito yalofanywa na waloitwa watu wasojukana uchunguzi umefanyika na kuwabaini ni kina nani?

Maana Mhalifu anaweza asijulikane mwanzoni lakini baada ya muda uchunguzi kuanza anapaswa kujulikana.

Kwamba ahaaa kumbe walofanya ule uhalifu fulani walikuwa kina fulani! Wananchi wanapaswa kupewa mrejesho.
 
Serikali na vyombo vya dola vituambie wananchi wale walokuwa wakifanya uhalifu mkubwa na kuitwa wasiojulikana

Je, wameshajukana sasa?

Ni kina nani kwa majina na titles zao?

Kama bado hawajajulikana mpaka leo tatizo litakuwa ni kubwa sana na kuleta mashaka makubwa kiusalama wa raia na kama nchi.

Nilitegemea wabunge wangeihoji serikali kuhusu hili seriously.
 
Ilibaki tuu marehemu walipie pango kodi walipozikwa.
 
Back
Top Bottom