Kenya 2022 Kwa yanayoendelea Kenya, Nyerere apongezwe kuondoa ukabila

Kenya 2022 General Election

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,026
Kiukweli Nyerere si wa kumbeza licha ya yeye kuwa mwanadamu aliekosea mambo machache likiwemo hili la muungano mithiri ya tembo kuungana na sungura wawe wanakula sawa.

Kiukweli siasa za Africa ikiwemo Kenya tumeshuhudia zikiwa zinabebwa sana na ukabila ambapo kabila likiwa na idadi ya watu wengi basi hawa ndio wanakuwa na sehemu kubwa ya uongozi wa nchi unaowawezesha kupeana vyeo, kujiletea miradi ya maendeleo , n.k.

Nyerere kwa nafasi aliyokuwa nayo angeweza kabisa kuwateua watu wa kabila lake vyeo vikubwa, kupafanya alikotoka kuwe na maendeleo sana, n.k. lakini alijua kabisa angeafanya hivi hii ingezaa mbegu ya ukabila

Kwa hapa Tanzania kwa makabila yenye watu wengi kama wasukuma, wachaga na wanyakyusa, Kwa mfumo wa ukabila leo hii ndio wangekuwa wamweshikilia serikali lakini kwa system iliyokuwepo tunashukuru sana kwamba wamepigwa pini.

Wasukuma wapo wengi sana, sana, sana,,, lakini ukiangalia asilimia ya idadi yao yenye uwakilishi kwenye uongozi ni ndogo, Tunamshukuru mama anafanya kazi ya kuwapunguza wengi walioingizwa na kujaa sana awamu flani, wapungue pungue kwakweli.

Wachaga wapo wengi tu wa kutosha tena hawa wameamka sana kwenye uongozi mpaka wana vyama vyao lakini system imewapiga pini, ila hawa kwa kujiongeza kidogo wakaingia kwenye biashara huku ndiko kulikowafanya wawe kabila lililofanikiwa zaidi.

Wanyakyusa nao wapo wengi sana, Lakini system iliyopo imewabana vizuri sana na wao wasitumie wingi wao kushika vyeo vingi vya serikalini, uzuri wao hawa ni watiifu kwa hio ni rahisi kuwa controll sio kama wachaga na wasukuma, Mambo ya kushikilia power hawana sana,

Halafu uzuri ni kwamba Nyerere alihimiza kwamba Makabila madogo ndio yawe yanapewa vipaumbele kwenye vyeo vikubwa hasa katika uraisi, Tulijaribu kwenda kinyume chake kwa kujaribu kumweka Msukuma, Weee!! Sidhani kama kuna mtu atasahau maana tulishuhudia wasukuma wengi wakilamba nafasi za uongozi, Maraisi kutoka nchi ntingine wakawa wanatua usukumani kuonana na Raisi, Nyumbani kwa raisi ulijengwa uwanja wa ndege mkubwa, N.k.

Matunda ya Nyerer ndio yanayofanya Leo hii Mchaga, Mngoni, Mfipa, Mnyakyusa, Mbena, Msukuma, Mnyakyusa, n.k walingane kwenye level za uongozi.

Asante sana Baba wa Taifa
 
Tanzania ni Taifa kubwa sana huwezi kulifananisha na Kenya. Japo kwenye ukabila na udini ni kweli Nyerere alituweka sawa.

Tukiacha UKABILA na UDINI, Nyerere alikosea sana kutuachia KATIBA mbovu namna hii na tume mbaya kiasi kile.
Tatizo sio katiba, Tatizo ni kwamba katiba haifatwi, hata wakileta katiba mpya unadhani itafatwa ??
 
Hayo unayosema Nyerere aliyasemea wapi ndugu yangu? tupe ata nukuu tukasome!! Hayo makabila uliyotaja jumlisha wahaya ndio watu walioelimika na yaliendelea angalau, sasa kulingana na poverty mentality yetu kuwa makabila madogo sijui ndio nn sasa
 
Tanzania ni Taifa kubwa sana huwezi kulifananisha na Kenya. Japo kwenye ukabila na udini ni kweli Nyerere alituweka sawa.

Tukiacha UKABILA na UDINI, Nyerere alikosea sana kutuachia KATIBA mbovu namna hii na tume mbaya kiasi kile.
Nyerere alisema katiba si msaafu. Inaweza kufanyiwa marekebisho ili kuakisi mahitaji ya wakati husika. Kizazi cha sasa ndo shida. Uwezo wa kufikiri ni mdogo sana
 
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Kenya (IEBC), Juliana Cherera na wenzake watatu wamesema hawayatambui matokeo ya uchaguzi mkuu yatakayotangazwa kutokana na hatua za mwisho kughubikwa na sintofahamu.
 
Wazee wa Pwani hawakumbagua Nyerere kutokana na dini au kabila yake. Wakampokea na kumpa nafasi ya kisiasa ndani ya TAA na baadae TANU.

Akaongoza mapambano,wakamlinda,kumshauri na kuwa pamoja naye. Tukapata uhuru, kidogo akakengeuka! Mapinduzi ya mwaka 1964 yakamkumbusha umuhimu wa umoja. Akahubiri umoja.
 
Hayo unayosema Nyerere aliyasemea wapi ndugu yangu? tupe ata nukuu tukasome!! Hayo makabila uliyotaja jumlisha wahaya ndio watu walioelimika na yaliendelea angalau, sasa kulingana na poverty mentality yetu kuwa makabila madogo sijui ndio nn sasa
Hatuongelei elimu tunaongelea wingi wa watu wa kabila katika kuiongoza nchi na wao kupeanna vyeo kiupendeleo, Tunaongelea wingi wa watu kwenye kabila, nchi kama Nigeria kabila la Hausa lina watu wengi na halijaelimika lakini wao ndio wanaiongoza Nigeria, hata mawaziri wanachaguana wao wenyewe hata kama wana elimu ndogo, makabila yaliyoelimika kama Yoruba na Igbo hayafui dafu hapo,

Kwa Tanzania Tunamshukuru Nyerere kwasababu

Wasukuma wapo wengi sana, sana, sana,,, lakini ukiangalia percent ya population yao yenye uwakilishi kwenye uongozi bado ni ndogo imepigwa pini,,, Hili ni jambo zuri.

Wachaga wapo wengi tu wa kutosha tena hawa wameamka sana kwenye uongozi mpaka wana vyama vyao lakini system imewapiga pini, ila hawa kwa kujiongeza kidogo wakaingia kwenye biashara huku ndiko kulikowafanya wawe kabila lililofanikiwa zaidi.

Wanyakyusa nao wapo wengi sana laiti kungekuwa na ukabila basi wangeikamata mikoa ya nyanda za juu kusini wangeikamata vilivyo, lakini kwa system iliyopo wamepigwa pini nao, uongozi unasambazwa kwa makabila mengi....

Hao wahaya uliowataja washukuru kuna hii system maana sehemu walizopo ni ukanda wa wasukuma, bila hii system hata elimu zao zisingefua dafu kuwangarisha, Licha ya hivyo kabila hili kwa kipinfi cha nyuma walitumia vizuri fursa za elimu lakini kwa sasa hali inavyokuwa elimu inasambaa sana Tanzania inafika sehemu nyingi, Zamani unaweza kukuta chuo kimejaa walimu wa kihaya lakini leo hii hali ni tofauti unaweza kuwakuta wahaya wawili, wengine makabila mengine, Ushauri kwa wahaya wajikite kwenye Biashara, huku kwenye elimu kwa sasa hawako peke yao.
 
Katiba ikiletwa na CCM haitafuatwa, maana wanakubali katiba kwa shingo upande ili watu wanyamaze. Katiba nzuri itakayofuatwa ni ile itakayopatikana baada ya machafuko, au nchi kupinduliwa.

kwan katiba yenu mnaifuata mkuu? mwenyekiti wenu mwisho miaka mingap?
 
Back
Top Bottom