Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 515
- 2,874
Viongozi walioko madarakani na kwa sisi vijana pia kuna la kujifunza.Kuna kitu kinaitwa misingi (values) au principles ,sheria na taratibu.Katika maisha yako unapopata nafasi yeyote ya kutumikia usijiaribu kumfurahisha aliyekuteuwa ukasahau kushikamana na misingi,taratibu na sheria.
Ukishikilia misingi , taratibu,kanuni na Sheria utaishi kwa kujiamini na kwa amani mara zote ,utapendwa na kila mtu sababu una simamia misingi kama ya haki ,usawa,upendo, uwajibikaji, heshima n.k. Misingi na taratibu hizi huishi milele .
Hata aliyekuteuwa akikuona unasimamia misingi , principles,Sheria ,na taratibu atakuogopa na kukuheshimu sana.Utapendwa sana na jamii hata siku akikuondoa katika nafasi yako utakuwa na amani moyoni na jamii itaendelea kukuheshimu mfano mkubwa ni CAG aliyeondolewa Prof.Mussa Assad anaheshimika hata na waliomteuwa katika mioyo yao wanamuheshimu , wananchi na jamii nzima tunamuheshimu sababu alisimamia misingi,Sheria,kanuni na taratibu wala hakufanya kazi zake kumfurahisha mtu.
Ila ukiacha misingi ,ukataka kumfurahisha aliyekuteuwa ukadhani ndio muarubani ,basi umepotea .Misingi huwa haibadiliki Ila viongozi unaowasifu na kuwafurahisha wanabadilika na hawatabiriki sababu wote wewe na yeye ni wanasiasa kila mtu mbele ya macho yake hutazamia kupata fursa ya sifa za kisiasa kwa maslahi binafsi hivyo anaweza kukugeuka muda wowote .
Ukajikuta upo pekeako ,uliitenga misingi na Sheria na taratibu ,ukatenga wananchi na watu ukatumia muda kumfurahisha aliyekuteuwa.Hatimaye aliyekuteuwa amekugeuka kwa kudharau na kuvunja misingi.Wewe ulidhani kuvunja misingi ndio mbadala wa kumfurahisha aliyekuteuwa.Sasa misingi imekutenga , wananchi wamekutenga na uliyekuwa ukimsifia amekutenga.
Huu ni ugonjwa ambao unatafuna viongozi wengi wa serikali ya awamu ya tano kwa kudhani ndio usalama wao ,mtu akisima jina Mh.Rais Magufuli linatajwa kwa marudio yasio hesabika,sifa hujaa pipa ,akidhani ndio njia yeye kupendwa badala ya kuishi na misingi ,kanuni , taratibu na Sheria .
Mjirekebishe ,heshimuni misingi ,kanuni , taratibu na sheria zitawaheshimu na kuwalinda pia .Mh Kangi alikwama hapo tuu alijisahau akidhani kumsifia na kumtukuza aliyemteuwa ndio mbadala wa kufuata misingi ya kazi na cheo chake leo hii anataka kufunguliwa mashtaka ya uhujumu uchumi.
Huu ugonjwa upo pia kwa Mh. Makonda ,@baba_keagan na viongozi wengine pia,kama hawatojitathimin na kubadilika watakumbuka maneno yangu.
Abdul Nondo.
0683494398
Sent using Jamii Forums mobile app