kwa WIZI/HUJUMA kwa wenye MAGARI---TRA na FAKE FIRE EXTINGUISHER---CCM kukosa kura nyingi 2015! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kwa WIZI/HUJUMA kwa wenye MAGARI---TRA na FAKE FIRE EXTINGUISHER---CCM kukosa kura nyingi 2015!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mr. Clean, Aug 9, 2012.

 1. M

  Mr. Clean Senior Member

  #1
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 195
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Jamani napata tabu kutambua uelewa wa wabunge wetu! kwa kupitisha maamuzi kuwa kila mwaka ukienda kulipia vehicle licence ulipie pia gharama ya fire extinguisher takriban 40,000/= pasipo kupewa hicho chombo chenyewe si dhuluma kwa wananchi huku?

  Mazingira nliyoyakuta TRA Kinondoni leo yamenisikitisha sana, kuona jinsi TZ nanavyoishi ktk zama za kale za mawe chini ya serikali hii ya CCM hadi karne hii ya sayansi na teknolojia!

  Ndo kusema ingekuwa basi wanatoa hizo tanki basi kila mwaka wangetoa mpya?

  Kwa dhuluma hii, naona SERIKALI ya CCM inateketea bado kuzimika tuu!

  Wabunge wa CCM nchemba, lisinde and the like mnaopiga makofi ya ndioooooooo! kila hoja mpoooooooo!

   
 2. Mtanzania1

  Mtanzania1 JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 1,169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  mkuu kazi kubwa ya serikali ni kukusanya kodi.......wanasiasa(mie naita wote) ndiyo kitu hasa kinachowafanya wapambane majukwaani....lakini inauma sana mnaposhtukizwa kwamba kama unataka kulipa kodi fulani basi unaongezewa na malipo mengine....huu ni wizi na hakuna maana ya kuwa na bunge la bajeti.....wameshindwa hata kutoa maelezo kwamba hiyo 50,000/- ni ya nini hasa...ya kukaguliwa kifaa??? kununua??? kupewa mafunzo jinsi ya kutumia?? ...inauma sana...si kwa kiasi cha pesa unacholipa bali kwa staili wanavyokichukua...........Mungu yupo......
   
 3. v

  vutakamba Senior Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 199
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  TRA ni wababe na wanyang'anyi. Wakishaamua wameamua hasa kwa wananchi wa kawaida wa chini ambao uwezo wao ni mdogo. Hebu fikiria mwananchi kastaafu na imemchukua si chini ya miaka 2 kusubiri mafao yake na inabidi hata akope ili apate angalau nauli ya kufuatilia. Hatimaye anapokea mafao na anaamua kujinunulia Toyota Hiace ili imsaidie kufanya dala dala ili kujikimu kwa maisha yake yaliyobaki duniani.
  Alipoagiza gari hiyo sheria ya wakati huo haikuwa na dumping fee yaani kodi ya uchakavu. Na kama ingekuwepo asingeagiza gari hiyo maana asingemudu gharama hivyo angeacha na kuangalia biashara ingine.
  Sasa gari imeshaagizwa na imeshaingia mpakani kwa sheria ya zamani, mara TRA baada tu ya kusomwa general budget wanatangaza kuanza kwa sheria mpya kuanzia 1/7/2012 bila kujali kuwa tayari kuna wananchi tayari walishaagiza magari kwa sheria ya zamani na mengine tayari yalishafika nchini na utaratibu wa malipo ulishaanza kufanyika.
  Ghafla unaambiwa ulipe tena 20% kodi ya uchakavu. Huyu mwananchi ambaye amepata pesa kwa kuokoteza atapata wapi pesa za ziada za kulipia?. Kama siyo ujambazi na unyang'anyi wa hata kidogo walichonacho wananchi ni nini?.
  Kwa kuwa si rahisi kwa malipo hayo kufanyika kutokana na ukosefu wa pesa na hali ngumu ya maisha ina maana itabidi gari hiyo ibaki mikononi mwa TRA huku tayari lilishalipiwa malipo yote halali kwa sheria ya zamani. Na matokeo yake ni kupigwa mnada kwa gari hiyo na TRA.
  Ni dhambi iliyoje kwa uonevu wa aina hii kufanywa na binadamu?. TRA wanapaswa kumwogopa Mungu la sivyo iko siku watalipwa kwa ubaya wao wa kinyama.
  Kibinadamu. Kuanza kwa sheria mpya ya kuingiza magari ilipaswa kuwa specific si jumla jumla tu. Kama vile yale magari ambayo yangeagizwa na kuingia nchini baada ya tarehe 1/7/2012, yasingejumlishwa Pamoja na magari ambayo tayari yalishaingia nchini kabla ya tarehe hiyo tajwa.
  Ni wananchi wengi wamekumbwa na kadhia hii. Na kama Serikali kupitia TRA ingekuwa sikivu kama inavyojinasibu mbele ya jamii wangeliangalia hili na kufanya marekebisho ili kuwapunguzia wananchi kadhia na mateso.
  Nawasilisha.
   
 4. Ether

  Ether Senior Member

  #4
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 16, 2008
  Messages: 137
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  hahaha! mtanzania ni mtu mmoja rahisi sana kumburuza kwa sababu hata akionewa hafanyi lolote na ndo maana hawa viongozi wanaweza kuwafanyia lolote wananchi. tutalalamika weee lakini in the end of the day mtalipa tu hizo ada za wizi.at this level the blame rests with us na mpaka tuamke kwenye huu usingizi wa pono hawa jamaa wataendelea na huu wizi. tutaomba mungu mpaka kesho ila mungu hata siku moja hasaidii wajinga wasiotaka kujisaidia wenyewe.
   
 5. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  wenye magari wapo wangapi?? na wangapi watapiga kura??

  mtaji wa ccm ni maskini, walio na umeme, wasio na magari, wasiojua kusoma na kuandika, walionyimwa rights za kujua haki zao
   
 6. m

  malaka JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nadhani hii itawauma sana waliotia tiki kiboksi cha ccm. Tuombe mungu 2015 sio mbali.
   
 7. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  Kaka kwa sasa nadhani wanafika 1 Million na zaidi, Na ukiangalia Upinzani uchaguzi uliopita kura hazikufika hata 1 mil.
  Kwa vyovyote ni wakti sasa kwahao 1 Milion kupiga kura na kuandaa na familia zao kupiga KURA za CHUKI naamini wenyemagari asilimia 70% watakuwa wameoa, so ukichukua wao na wake zao ni kura si chini ya 1 Mil.
   
 8. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  sidhani kama uko sahihi

  umesahau serikali yaweza kuwa na 30% ya magari yote tunayaona barabarani, wafanyabiashara wachache sana wenye magari mengi na watu binafsi wenye magazi zaidi yamoja

  Kumbuka waajiriwa wanaotumika na serikali kwa kiasi fulani ni laki kama nne hivi


  fanya hesabu zako tena, elimu, afya, kilimo na ardhi ndivyo vinatakiwa kuwa target ya chadema kuongoza nchi... madini, ufisadi nk yes, but those are catalysits, chemical reactions zenyewe ziko kwenye social services
   
Loading...