Kwa wenyeji wa Mzumbe University: Wale wanaosoma sheria nao wanasoma kwa kupokezana?

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,663
18,036
Kuna baadhi ya kozi pale mzumbe husoma kwa kupokezana. Yaani wengine wakiwa chuoni, wengine wanakuwa likizo, kisha waliokuwa chuoni wakienda likizo, ndipo waliokuwa likizo wanarudi chuoni. Je kwa wanaosoma shahada ya sheria Nao husoma hivyo hivyo kwa kupokezana? Je kuna usumbufu wowote kwa mtindo huo?
 
Ndio! Kuna Jamaa yangu walifunga mwezi wa tatu wakafungua mwezi wa saba huko!
 
Hapo itabidi nimshauri dogo akitose! Hii kusoma kwa mafungu siyo kabisa! Au kuna faida yoyote ya kusoma kwa awamu? Au kuna faida zipi ambazo pamoja na kusoma kwa awamu bado inalipa?
 
Hapo itabidi nimshauri dogo akitose! Hii kusoma kwa mafungu siyo kabisa! Au kuna faida yoyote ya kusoma kwa awamu? Au kuna faida zipi ambazo pamoja na kusoma kwa awamu bado inalipa?
Mwache dogo aende kula kitabu Mzumbe University. Ni bonge moja la chuo lenye kutoa elimu ya uhakika nakwambia hawezi kujutia. Baadhi ya wahitimu pale ni pamoja na Makamu wa Rais, Naibu Waziri wa Fedha, Nape, Marehemu Kombani, Hussein Bashe,
 
Na Funzadume mzee wa makinikia
 
kusoma kwa kupokezana ni mwaka wa kwanza tu tena semista ya 2 baada ya hapo chuo kinaendelea kama kawaida.

huku kupokezana watu wana tafsiri kama vile kila mwaka wa masomo lazima watu wapokezane sio kweli aseeh
 
yah wanapokezana, tunaiita staggered semester... wakifunga mwez wa 3 wanarud mwez wa saba wanapga ktab ad miez miwil tu then wanaingia second year...
Ila All in All Mzumbe chuo makini sana na kinatoa cheti cha maana
 
Nimetumiwa ujumbe wa SMS za kawaida, kuwa nmechaguliwa udom,nitume majina yangu kuconfirm ,vipi nikweli au ! Nisaidien mawazo ,nawasilisha
 
Hii kusoma kwa kupokezana inaashiria kuwa wanafunzi hudahiliwa wengi kuliko uwezo Wa chuo wa kuwahudumia kwa Mara moja. Kwa nini wasingedahili idadi wanayoimudu?
 
Nzumbe hakuna kitu kinachoitwa kusoma kwa kupokezana hizo ni lugha tu. Chuo makini sana duniani kuwahi kutokea. Ila huyo dogo kwa sheria ajipange sababu wakina Mgeta, Leiza, Nkobobo wao kula vichwa sio suala la kuuliza.
 
Back
Top Bottom