Kwa wenye uzoefu wa kutumia uganga katika biashara

MeruA

JF-Expert Member
Aug 9, 2017
1,391
2,125
Habarini za leo ndugu zangu,

Sitaki kupoteza muda naenda moja kwa moja kwenye lengo,

Humu ndani kuna watu wenye shughuli mbalimbali wapo waliofanikiwa kupitia biashara,kilimo ajira n.k

Napenda kupata msaada wa mawazo kwa wale ambayo wamefanikiwa biashara zao kupitia kwa waganga wa jadi,japo tuna imani tofauti tofauti lkn hatuwezi kukataa uwepo wa jadi ambayo ni asili yetu.Waliofanikisha mambo yao kupitia waganga wa kienyeji watupe udhoefu na kwa namna gani walifanikisha mambo yao,maana sote tu watafutaji na katika utafutaji kuna njia mbalimbali za kupita ili kufikia malengo.Karibuni
 
Mkuu usijaribu kulamizimisha kuvuta rizki kwa nguvu hizo ni pesa za giza mkuu utajuta na utakuwa na simanzi daima utaangamiza familia yako yote kwa pesa za giza wanaanzia na damu ya samaki,watakwambia ya kuku au panya au ya sungura,watakuja ya mbuzi na ng'ombe kulinda mali mwishowe ya familia yako eidha watoto,mkeo au wazazi wako mkuu faida yake iko wapi ikiwa watu wa kula nao pesa yako utawapoteza.
 
Hapo sasa
 
kiukweli utajiri hausitawi bila ndumba, namaanisha huwezi miliki utajiri bila kuwa muumini wa kiza. matajiri wote unaowaona wanasili nzito na hutokaa kuijua juu ya Mali wanavyomiliki. sisi waoga tukubalini na hali zetu tu tukipata hela ya kula tulidhike tu lakini maisha ya utajiri huku yesu yesu..sahau hilo
 
Habarini za leo ndugu zangu,

Sitaki kupoteza muda naenda moja kwa moja kwenye lengo,

Humu ndani kuna watu wenye shughuli mbalimbali wapo waliofanikiwa kupitia biashara,kilimo ajira n.k

Napenda kupata msaada wa mawazo kwa wale ambayo wamefanikiwa biashara zao kupitia kwa waganga wa jadi,japo tuna imani tofauti tofauti lkn hatuwezi kukataa uwepo wa jadi ambayo ni asili yetu.Waliofanikisha mambo yao kupitia waganga wa kienyeji watupe udhoefu na kwa namna gani walifanikisha mambo yao,maana sote tu watafutaji na katika utafutaji kuna njia mbalimbali za kupita ili kufikia malengo.Karibuni
wala usitumie dawa. Dawa zipo sema hatuzijui ila nakupa moja kama unaishi karibu na ziwa au bahari bas kachote yale maji kwenye kidumu kisha chota na mchanga wake kiasi dumbukiza ndani baada ya hapo rudi nayo home unapokua unataka kwenda kwenye biashara oga vizuri badae jisuuze na hayo maji yako kama una biashara utashangaa inaenda vizuri tu
 
Aisee usijaribu utajiri wa ndumba una masharti magumu balaa.
Fikiria una utajiri wa Bilioni mbili lakini huruhusiwi kulala kitandani au huruhusiwi kupanda gari.
Una utajiri mkubwa lakini hutakiwi kuvaa viatu vya kufunika au unataka wa kuvaa malapa.
Kuna tajiri mmoja alikua na sharti la kutovaa viatu, ikatokea akapata emergency ya kwenda Dar es Salaam haraka ikabidi apande ndege. Alipofika kwenye ndege wakamzuia coz amevaa malapa wakamwambia avae angalau sandals.
Akavaa sandals akasafiri, kufika Dar es Salaam anapewa taarifa magari yake yamepata ajali na mali zimeungua moto.
Bado alikua ametoa kafara ndugu Zake wengi lakini mwisho wa siku akapoteza mali zake na ndugu Zake pia aliowatoa kafara.
Katika maisha chagua vitu viwili pesa au amani(furaha). Kama kipaumbele chako ni pesa sio amani unaweza kutafuta utajiri kwa waganga utaupata lakini utakua na maisha yasiyo ya furaha.
Kama Amani kwako ni muhimu fanya kazi kwa jasho lako usitegemee waganga.
Usisahau kujihusisha na waganga ni kutengeneza maagano ambayo kuyavunja ni ngumu.
Baki na imani yako.
 
mambo yanazidi kuwa magumu mtaani na kifuku kinakuja watu watatafutana wakazi wengi wa dar wanaishi kwa imani hizi ila ni ngumu kusema
 
Mkuu usijaribu kulamizimisha kuvuta rizki kwa nguvu hizo ni pesa za giza mkuu utajuta na utakuwa na simanzi daima utaangamiza familia yako yote kwa pesa za giza wanaanzia na damu ya samaki,watakwambia ya kuku au panya au ya sungura,watakuja ya mbuzi na ng'ombe kulinda mali mwishowe ya familia yako eidha watoto,mkeo au wazazi wako mkuu faida yake iko wapi ikiwa watu wa kula nao pesa yako utawapoteza.
Umenena mkuu mungu ndo mpaji tuu.
 
Back
Top Bottom