Kwa wenye uzoefu na Toyota Belta 1290cc naomba ushauri

muuza ubuyu

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
3,510
3,477
Wakuu, naombeni mwenye uzoefu na hicho kigari.

Nimeangalia beforward nikaona kwa mazingira ya sasa ambayo nahitaji kufanya heavy investments, nahitaji kuwa na gari ndogo yenye gharama ndogo za uendeshaji hivyo chaguo langu limeangukia kwenye gari hii tatizo sina uzoefu nayo kuhusu uimara wake (given utunzanji upo constant).

Kwa sasa nina Toyota Harrier 3.0 L (old model) mwaka wa 5 huu hivyo nahitaji kubadilisha kabla haijaanza kuniletea matatizo, na pia nahitaji tu gharama zangu ziwe chini ili savings zangu ziwe kubwa nifanikishe lengo tajwa hapo juu.

Baada ya kufanikisha investments zangu ndiyo nitarudi kwenye SUV nizipendazo ambazo ni kati ya BMW X5/ Benz M Class au GL Class au Volvo XC 90 (that is five years to come mwenyezi Mungu akibariki).

Wenye uzoefu na Belta naombeni ushauri wenu. Japo kwa kweli moyo unaniuma kuacha comfortability ya Harrier.

1615978066535.png

Toyota Belta
 
Mrithi wa Platz. Kama lengo ni kutoka point A kufika point B bila kutumia wese sana au gharama sana kwenye gereji sawa. Kachukue tu.

Engine yake 2NZ-FE ile ngumu kama jiwe so usiwe na wasiwasi. Sema ni vigari vya zamani tegemea kutu kutu tu.
 
Asante mkuu, nimeviona vi Belta vya miaka ya 2005 kupanda juu, kimuonekano ni vizuri sana. Na imani pia hata masafa marefu ya 1,000km vinafaa japo najua stability ya barabarani haitakuwa nzuri sana compared na gari ninayotumia now.
 
Asante mkuu, nimeviona vi Belta vya miaka ya 2005 kupanda juu ni vizuri sana. Na imani pia hata masafa marefu ya 1,000km vinafaa japo najua stability ya barabarani haitakuwa nzuri sana compared na gari ninayotumia now.
Boxer pikipiki inapiga ata kilometa 1,000 tatizo muda, speed, na comfortability tu barabarani.

Ila kama ndio unanunua kwaajili ya masafa marefu tu (tuseme mara 3-4 kwa mwezi) sikushauri.
 
Boxer pikipiki inapiga ata kilometa 1,000 tatizo muda, speed, na comfortability tu barabarani.

Ila kama ndio unanunua kwaajili ya masafa marefu tu (tuseme mara 3-4 kwa mwezi) sikushauri.
Hapana masafa marefu ni mara chache sana! Hata ikiwa mara 2 kwa mwezi, basi safari za style hiyo hazitazidi 3 au 4 kwa mwaka!

Sema zile za 600km (go and return) zinaweza zikawa mara 1 au 2 kwa mwezi.
 
Hapana masafa marefu ni mara chache sana! Hata ikiwa mara 2 kwa mwezi, basi safari za style hiyo hazitazidi 3 au 4 kwa mwaka!

Sema zile za 600km (go and return) zinaweza zikawa mara 1 au 2 kwa mwezi.
Basi itaweza. Service ukifanya kwa wakati na vizuri.

Ila kwa bei ya JP hazitatofautina na Corolla, Runx, Alex, IST, Raum, etc ambazo me naona zina muonekano mzuri zaidi.
 
Basi itaweza. Service ukifanya kwa wakati na vizuri.

Ila kwa bei ya JP hazitatofautina na Corolla, Runx, Alex, IST, Raum, etc ambazo me naona zina muonekano mzuri zaidi.
Thanks, mbadala wake ninaoweza ku-opt ni Corolla. Nitaendelea kucheki zaidi, ngoja niisukume kwanza hii Harrier!
 
Back
Top Bottom