Kwa wenye uzoefu na mikopo ya benki/sheria za mikataba

m2me

Member
Jul 23, 2012
63
15
Habari zenu wadau,
Kwanza niwapongeze waliobuni na kuanzisha jukwaahili ambalo siyo tu ni chanzo cha habari mpya, burudani bali pia kisima chamaarifa. Hapana shaka kuwa kila anayetembelea jukwaa hili huondoka na fikra namtazamo tofauti juu ya maisha yake binafsi, taifa na mahusiano yetu kimataifa.
Kwa kutambua hilo, nimeona nitake msaada wakisheria hasa sheria za mikataba na fedha. Nilichukua mkopo kutoka benki mojahapa nchini tawi la Mwanza kwa dhamana ya mwajiri wangu kwa makubaliano yakukatwa kiasi fulani cha fedha kutoka kwenye mshahara wangu kwa kipindi chamiaka 3 ambapo natarajia kumalizana nao ifikapo October 2015.
Pamoja na makubaliano hayo, na kama mnavyojua hiziasasi zinazotegemea wafadhiri kwa asilimia 100, hatuna mishahara kwa zaidi yamiezi 6 sasa japo kuna matumaini kuwa hali inaweza kutengamaa kuanzia mweziujao (Octoba).
Kutokana na hali hiyo, nimeshindwa kabisakurejesha kiasi chochote kwa zaidi ya miezi 6 kutokana na ukweli kuwa mkopo huonilijaribu kuingiza kwenye biashara nikakutana na changamoto kadhaa ikiwemoajali na wizi.
Baada ya kuona kimya “hakuna marejesho kwa miezikadhaa” zikaanza simu zinazojitambulisha kuwa ni kutoka makao makuu ya Bankhusika, zikifuatilia mkopo huo ambapo nilijaribu kuwaeleza hali halisi yamishahara kwani ndo iliyokuwa nyenzo pekee ya ulipaji wa deni hilo.
Simu hazikukoma lakini pia afisa mfuatiliaji wamikopo kutoka tawi la benk hiyo alifika ofisini kwetu na kuzungumza na mwajiriambaye alimweleza hali halisi kuwa tupo (hatujaacha kazi) ila mishahara ndo hakuna kutokana na sababunilizozieleza hapo juu.
Pamoja na majibu hayo kutoka kwa mwajiri na ukwelikuwa tulishapewa barua zinazoeleza hali ya uchumi wa ofisi yetu na kuruhusiwakutafuta kazi kwingine au kuendelea kuvumilia hadi hali itakapotengamaa, badosimu zimeendelea kupigwa na safari hii deni langu likizidishwa kwa zaidi yamara tatu ya deni halisi!
Hali hiyo ilinishtua na hata kulazimika kutembeleatawi la benki hiyo ambapo afisa mikopo alinieleza kuwa wanaopiga simu nimadalali waliopewa jukumu la kufuatilia deni hilo na kuwa hawataacha kunipigiasimu kwani wanatimiza kipengele chao kabla ya hatua itakayofuata ya kukabidhiwakwa mfilisi ambaye atakapo ingia kazini atakamata hadi simu ya mchinaninayotumia!
Pia alinieleza kuwa kiasi ninachotajiwa na dalalisiyo cha kweli ila kinaweza kufika hapo baadae kama sitolipa deni hilo mapemakutokana na adhabu “fine/penalty”. Dalali anasema deni langu ni milioni 7,Benki wanasema million 3.6 na mimi natambua deni la milioni 2.2
Msaada:

  1. Nikwanini kuwe na adhabu wakati benk inafahamu kuwa kwa sasa sina mshahara nadhamana yangu ni mshahara?
  2. Kwanini adhabu hiyo isianze kutumika baada ya tarehe ya mwisho ya urejeshaji mkopo(Oct, 2015)? Kwani katika kipindi hiki harakati ninazofanya zinaweza kuzaamatunda na hata nikaweza kurejesha kiasi chote (2.2 m) hata kabla ya tarehehiyo.
  3. Mwajirianawajibika vipi na deni hilo? Au nini msaada wake kisheria?
  4. Je,ni sawa kisheria benk kupiga mnada mali za familia kama shamba, nyumba/gariamabavyo nimevipata nje ya mkopo huo?
  5. Je,ni sahihi benk kuendelea kunipiga ‘fine’ hata baada ya kuonesha nia yakurejesha kidogo kidogo kwa kadri ninavyopata?
 
Umeuliza maswali mengi sana ila jibu lake ni moja tu,MKOPO uliokopa mdhamini wako alikua ni mwajiri wako na mshahara wako ndio pekee utukao tumika kurejesha makato,ndo maana kipindi umeanza kukatwa wewe sio uliokua unapeleka makato ni mwajiri wako. Na ktk mambo ya mikopo wewe hata ungekufa leo mwajiri wako ndo anawajibika kuelewana na hiyo benki. Soma vizuri mkataba wako wa mkopo hakuna kipengele kinachokupa nafasi kujidhamini mwenyewe.
Hao benki ni wezi na simama imara kutetea haki yako.
 
Katika mikopo kipengele kinachonikera ni kimoja tu,eti benk ina uwezo wa kuongeza au kupunguza riba ya makato bila kumjulisha au kumuhusisha mteja.
 
Katika mikopo kipengele kinachonikera ni kimoja tu,eti benk ina uwezo wa kuongeza au kupunguza riba ya makato bila kumjulisha au kumuhusisha mteja.

Huo nao ni aina ya wizi,wataongezaje riba wakati mimi na wao tulishafunga mkataba wa kunikopesha kiasi fulani kwa makato ya riba kiasi fulani,kwahi kama wameamua kuniongezea au kunipunguzia wanatakiwa waje tena tufanye makubaliano mapya kuhusu huko kunipunguzia au kuniongezea riba.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom