Kwa wenye uzoefu na kuagiza mizigo Dubai

KeXMO

Member
Jul 25, 2021
20
0
Naleta kwenu wana JamiiForums

Kwa wale wenye uzoefu wa kuagiza bidhaa mbalimbali kutoka Dubai kuja Tanzania tupeane experience japo kidogo

EXPERIENCE HUSANI KATIKA;
• Masoko: ni masoko yapi maarufu kwa kuuza nguo,mikoba, electronics devices,simu used nk
• Platform: ni online platform gani zinatumika dubai kuuza bidhaa kama ilivo kwa amazon, eBay,Alibaba, AliExpress,na zingine nyingi.
• Changamoto: Ni changamoto gani /Zipi ambazo wafanya biashara wanapitia katika kuagiza mizigo yao kutoka Dubai kuja Tanzania?
 
Nafikiri asilim8a kubwa kwa mara ya kwanza wanakwenda wenyewe.

Sidhani kama kuna website/app moja yakuagiza vitu vyite hivyo kutoka DBx ???

Japo sijajuwa njia wanazotumia kuship mizigo ni maji au anga!!!
 
Kusanya pesa upande pipa wende Dubai mkuu, Kwa uzoefu wangu ni vizuri ukienda mwenyewe hapo ndio utaweza kutengeneza mazingira mazuri ya kuagiza mizigo ikiwa tayari ushakuwa na connection nzuri na wenye maduka na ma clearing agents.

Dubai ipo very easy mazingira yake tofauti na china,Biashara nyingi zinapatikanwa kwenye center ya mji wake wanaita Deira, hii ni kama vile Kariakoo kwa hapa Dar. Biashara nyingi unamalizana nazo hapa, ni chache tu ambazo zitakulazimu utoka nje ya huu mtaa.
 
Back
Top Bottom