Kwa wenye ndugu aliye na ulemavu wa akili. Natafuta Kazi

Barn

JF-Expert Member
Feb 28, 2017
2,734
4,024
Habarini ndugu zangu..

Kama kichwa kinavojieleza Mimi ni kijana niliemaliza shahada ya elimu maalumu kwa watu wenye ulemavu wa akili (cognitive disabilities), nimeona tujaribu kusaidiana kama una ndugu mwenye ulemavu wa akili jinsi ya kumsaidia ili umuhimu wake uonekane kwenye jamii.

NB: ulemavu wa akili ni tofauti na ukichaa.

"Disability is not inability"
 
Aiseeee!
sikutegemea kukutana na reply ya aina hii.
Mambo iko tight mkuu!
Jengo la TRA linajengwa porini kusiko na walipa kodi, traffic lights kuongozea vinguchiro, uwanja wa ndege wa maonyesho!

Muhimbili mzazi analipia kujifungua lakini mume wa grace analipia meli ya wachina kufanya utalii wa kitabibu!

Huyu jamaa tunampigia magoti aende tafadhali!

Hatuna hela za kumpata General Chiwanga!
 
Hahahahahaha
 
Hahahahahaha
All in all Nakuona kwa jicho linalotafsiri kuwa unaupeo mkubwa katika kupenda kazi unayoifahamu na upo tayari kufanya kazi na kuutumia ujuzi wako kwa manufaa ya jamii.

Mungu akupe na upako wa kufanikisha matibabu kwa ndugu zetu wenye matatizo ya mfumo wa akili.

We are all the subject to the matter.
 
grace mugabebashite kadandia issue ya Mali shenzy type anapenda kiki kujifanya yeye ndo kaorganise kumbe chakubanga tu iyo meli inakuja everyyear tokea kipindi cha JK na inatembelea nchi nyingi c Tz na wanapokelewaga na Jeshi na mayor
chakubanga bashite kaweka utaratibu mpya aonekane yeye ndo kawaleta
 
Hivi hilo jengo la TRA unalolisema ushawahi liona kweli?
Jengo lenyewe ki ghorofa cha ngazi moja tu ndo ushakuwa maneno.
Ata kama ni porini ni muhimu wananchi wa huko nao kupata huduma kwa ukaribi zaidi.
Tupia kapicha ka hako kagorofa mkuu uniongezee ufahamu
 
All in all Nakuona kwa jicho linalotafsiri kuwa unaupeo mkubwa katika kupenda kazi unayoifahamu na upo tayari kufanya kazi na kuutumia ujuzi wako kwa manufaa ya jamii.

Mungu akupe na upako wa kufanikisha matibabu kwa ndugu zetu wenye matatizo ya mfumo wa akili.

We are all the subject to the matter.
Asante sana mkuu kwa maombi yako
 
Tutofautishie hizo aina za ulemavu wa akili na viwango (degree) vya ulemavu kwa kila aina utakazo zitaja (hapo juu)
 
Tutofautishie hizo aina za ulemavu wa akili na viwango (degree) vya ulemavu kwa kila aina utakazo zitaja (hapo juu)
Ulemavu wa akili unajumuisha matatizo mbali mbali yanayoweza athiri mfumo wa ubongo na imegawanyika katika aina nyingi kama; asperger's syndrome, rett's syndrome,down's syndrome,autism, mental retardation, schizophrenia, panic and mood disorders, depression and anxiety disorders na zingine zipo nyingi.
Degree (kiwango) cha ulemavu wa akili inafuatana na Huyo mtu ameathirika kwa kiasi gani ambapo imewekwa katika madaraja kama; mild cognitive disabilities, moderate cognitive disabilities, severe cognitive disabilities and profound cognitive disabilities, kwa hiyo katika kila ulemavu mahususi kuna kiwango chake kwa mfano usonji (autism) wapo ambao ni mild,moderate,severe na profound,hivyo hivyo na kwenye aina zingine za ulemavu wa akili.

Asante kama nitakua nmeeleweka karibu kwa mchango wako na maoni pia
 
Upo vizuri mkuu, nakushauri fungua "kitengo" wazo la kuajiriwa ni wazo "mfu". changamoto kubwa utakayo kutana nayo wengi wao (hao wanafunzi) watarajiwa hasa (weusi) ni masikini hivyo ili kuavoid hasara changanya na wahindi ukiwa (serious) utatoboa. Ushauri:-si lazima uwe na madarasa anza kuwasaidia majumbani mwao.
 
Asante kwa ushauri mkuu
 
Back
Top Bottom