Kwa Waziri wa Utalii Tanzania kuhusu Mlima Kilimanjaro na Wakenya

abdulhamis

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
1,436
2,292
Habari wadau,

Leo nimeona nitoe mawazo yangu juu ya ili swala linaloendelea baina yetu na Kenya kuhusu Mlima wetu wa Kilimanjaro.

Kwa miaka mingi wakenya wamekua wakijinad kua Mlima Kilimanjaro ni wa kwao na kuutumia kupata watalii.

Nilikua nashaur kama Wakenya wanatumia Mlima wetu basi na sisi tuwatumie wao kwasababu tukisema tuziwie hata kwa kuziba ukuta haitowezekana ila tufanya hivi.

Serikali ya Tanzania inatakiwa imtumie Mkenya katika kutangaza vivutio vyetu vingine vya Tanzania pamoja na Kilimanjaro yenyewe.

Tunatakiwa Tujenge mabango makubwa kama yale ya Hollywood ya Marekani na Tuandike maneno kama:

Karibuni Kilimanjaro Tanzania
Tunayo mengi ya kukuonesha
Tuna Serengeti
Ngorogoro nk

Hii itakua imesaidia kwetu kwa sababu kivyovyote vile wakenya lazima Watutangaze kwa sababu hawawezi kuacha kuonesha watalii Mlima Kilimanjaro na kila mtalii akiungalia mlima lazima asome yale maneno na moja kwa moja atajua Kilimanjaro ipo wapi.

Hii itafanya watalii wengi kutoka Kenya kurudi kwao wakijua kua Mlima Kilimanjaro upo Tanzania na huenda wakiulizwa kuhusu Africa Lazima waelezee ukwel halisi.

Hayo ndiyo mawazo yangu. Maana Kenya kazidi
 
Kumtumia Mkenya siafiki. Wabongo wenyewe tunaweza, ila hapo kwenye bango kubwa ndo pazuri yani liwekwe bango kama lile la Hollywood likitizama upande wa Kenya hapo sasa liandikwe jina la nchi na vivutio vingine nchini naona jamaa watakua wanatupigia promo wenyewe bila hata kutaka.
 
Kumtumia mkenya siafiki, Wabongo wenyewe tunaweza, ila hapo kwenye bango kubwa ndo pazuri yani liwekwe bango kama lile la Hollywood likitizama upande wa Kenya hapo sasa liandikwe jina la nchi na vivutio vingine nchini naona jamaa watakua wanatupigia promo wenyewe bila hata kutaka
Lazima watutangaze yani tukiweza ivi ndani ya Mwaka Wakenya na Kilimanjaro yetu wataisahau
 
Back
Top Bottom