Kwa Waziri wa Michezo na Viongozi wakubwa Serikalini

GedsellianTz

JF-Expert Member
Jul 5, 2016
1,318
2,000
Moja ya watu wenye laana kubwa sana Tanzania ni viongozi wezi na wenye uchu wa madaraka,wanaopenda rushwa .Bungeni wamejaa watoto wa wabunge na mawaziri wenye uwezo mdogo kwa kila kitu,Bunge halina mashiko wala tija tena sababu ukweli humuweka mtu huru,Umaskini ,ujinga,Elimu mbovu vinaongezeka kwa kasi kuliko kukua kwa uchumi sababu ya udogo wa akili ya baadhi ya viongozi.

Viongozi wanachaguana kwa udhaifu wao kifikra,utendaji,uwajibikaji na uzalendo kwenye Taifa ambalo linahitaji watu wabunifu ,wazalendo,wenye upeo mkubwa na mawazo chanya yenye uwezo wa kudumu miaka 30 inayokuja.Bunge la sasa wamejaa watoto wa viongozi waliokufa na kurithi nafasi za baba zao na mama zao ila linapokuja swala la utashi,uwajibikaji,ubunifu,kujenga hoja na kutetea hoja kule bungeni ni aibu sana.

Viongozi wanachagua watu wenye hobby ya uongozi na sio karama ya uongozi hili tayari ni tatizo kwa taifa,si kila Professor anaweza kuwa Kiongozi na si kila kiongozi anatakiwa kuwa mtoto wa kiongozi ,Kuna watoto wa maskini wenye uwezo mkubwa sana kiuongozi na wana vipaji vya uongozi ila hawajapewa ridhaa ya kulitumikia taifa hili la viongozi wasio na tija na wananchi maskini wenye akili kuliko viongozi wao.

Badala ya kutoa mikopo ya Elimu ya juu nafikili tubadilishe utaratibu wa kutoa mikopo kwa vijana wenye karama ya kufanya biashara na uwekezaji ,sababu haina maana unampa mtu mkopo wa elimu kwa muda wa miaka mitatu harafu unamyima ajira ,na watoto wenu mnawapa uongozi wakati darasani walikuwa hawana uwezo wa taaluma wala kiuongozi.

Ukifuta umisseta jua unaharibu karama za watu wengi sana,soccer ni ajira bora kwa sasa na njia moja wapo ya kuthibitisha karama za watu ni kutengeneza Tournemnt zenye tija kwa wafanyakazi na wanafunzi ili kuweza kuwa na mseto wa kizazi chenye karama tofauti katika ujenzi wa Taifa hili la viongozi wenye udogo utashi na ubunifu.

Nimecheza michuano ya vyuo vikuu vya Africa Mashariki na kati iliyofanyika Uganda mwaka 2006 najua hamu na njaa ya kuonyesha karama yako unapokutana na watu wenye karama kama yako . Hatuwezi kuwa wafanyakazi wasomi wote tuliotoka vyuoni,wala wanavyuo wote hatuwezi kuwa wafanyabiashara ,Waziri wa michezo atizame kwa kina suala la michezo kwa kizazi hiki.Sababu karama ni bora kuliko Elimu.

Wealthy people have not disappeared, they are just not so willing to show off their wealth.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom