Kwa wazazi,walezi na wazazi watarajiwa hii inakuhusu

mak89

JF-Expert Member
Sep 21, 2012
1,072
914
Nimekuwa na mawazo ya muda kuandika huu uzi ila mambo yalikuwa mengi nikawa nahairisha mara kwa mara leo ndo nimeona ni muda sitahiki sasa twende kwenye mada.
Je unajua kama watoto ni zawadi ya Mungu kwetu? Je unajua kama ipo siku unaweza ukaukumiwa kwa makosa ya wanao? Kwa wale wakristo na wasoma biblia watakuwa wanajua kisa nabii wa Mungu ELLI, kwa kifupi ni kuwa kifo cha Elli ni kushindwa kulea watoto wake vizuri. Haya sasa tuendelee, vifuatavyo ni vitu vya kumfanyia mwanao na vyakutomfanyia.
Vifuatavyo ni vitu ambavyo hupaswi kumfanyia mwanao.

1.Zawadi, wazazi wengi huwa wana tabia ya kuwa nunulia watoto wao zawadi na kuwapelekea nyumbani pale watokapo kazi, zawadi siyo kitu kibaya kwa mtoto ila inategemea hiyo zawadi anakula na nani kwa mfano nyumbani una watoto watatu na ndugu wengine na unapokuja na zawadi anapewa mtoto mmoja tu hapo unamtengenezea uchoyo tangu akiwa mdogo kwasababu alishazoea kupewa kitu na wengine hawapati na hii itamfanya kujiona yeye ni bora kuliko wengine. Chakufanya unapokuja na zawadi hakikisha inaweza gawanyika na wengine wapate hii itamfanya ajione yeye na wengine ni sawa.
2.Kukoa au kumpiga kibao kwenye mashavu, mtoto anapofanya kosa kuna njia nyingi za kumhadhibu kama kumchapa au kufanya kazi pekee yake kutokana na kosa alilofanya ila siyo kumpiga kibao au kumkuoa hii inamjengea uoga muda wote, ndo maana kuna nyumba nyingine baba akiingia tu watoto wanakuwa kama mazezeta hivi au wanakimbilia chumbani.
3.Usiwe materialist parent/husimfanye materialist child, kama mzazi unatakiwa upendo wako kwa wanao husiwe taken over na vitu. Hapa nitakuja kupaongelea kwa undani zaidi.
4.Hasifanyiwe vitu vinavyo muhusu na mtu, kuna wazazi wengene sijui ndo wanamapenzi sana na watoto wao hapo sina jibu ila kuna umri mwanao anatakiwa afanye kazi kama kufua na kunyoosha nguo zake pi na kufanya vikazi vidogo vya nyumbani, wazazi huwa tunapenda kupeleka watoto wetu kwenye shule nzuri ni jambo jema je huku huwa wana extra activities? Au ndo kusoma tu bila hata kufanya kazi ndogondogo ili kujenga mwili wake? Mfana unakuta mtoto amesoma primary english medium ambako ambako watoto wanatandikiwa hadi vitanda hata akija nyumbani anajua kuna mtu maalumu kwa ajili ya kumtandikia kitanda au kumfulia nguo. Penda kumshughulisha mwanao na hii itamjenga na ataweza kuishi na watu wengine bila kuona anaonewa
Sasa embu tuangalie ni mambo gani kama mzazi au mlezi unatakiwa kumfanyia mwanao, haya tufuatane.
1.Jenga urafiki na mwanao/wanao, kwa kujenga urafiki na mwanao utaweza kujua mambo mengi sana yanayo muhusu na yeye atakuwa willing kukueleza wewe, ujue ulimwengu umebadilika sana usidhani ulimwengu uliopitia wewe enzi hizo ni sawa na sasa tengeneza urafiki ambao utamfanya kuwa muwazi mapema kwako kuliko kwa mtu mwingine hata ushauri.
mengine nitamalizia, kama kuna mtu ana mengine aongezee
 
Back
Top Bottom