Kwa wazazi na walezi: Mada maalum ya watoto

Wengi wetu humu tunalea ama watoto wetu ama watoto wa ndugu jamaa na marafiki.

Tumekuwa na mada maalum nyingi za mambo tofauti kama urembo magari simu n.k. lakini hatujawahi kuwa na mada hii maalum ya watoto.

Kumlea mtoto tangu kutungwa kwa mimba mpaka kuzaliwa na hatimaye kulelewa mpaka kuvuka kile kipindi cha hatari si jambo dogo.

Changamoto ni nyingi hasa na zingine hatujui jinsi ya kuzitatua lakini tukiwa na hii mada hapa jukwaani tutashirikishana na kujuzana mengi kwa haraka na uhakika zaidi.

Kuna vitu vidogo vidogo ambavyo havihitaji daktari au ufumbuzi wake ni kama huduma ya kwanza kabla hujapata usaidizi mwingine. HII NI TOFAUTI NA JF DOCTOR.

Kwa mfano, ufanyeje;

-Mtoto anapolialia
-Mtoto anapopata gesi tumboni
-Mtoto anapopaliwa kila akila chochote
-Mtoto anaposhtuka shtuka usiku na kulia sana nk k

Hatari zimnyemeleazo mtoto;
-Umeme
-Maji
-Moto
-Mwanga wa Tv
-Simu, mawimbi yake
-Vyombo na vitu mbalimbali
-Madawa na vipodozi nk nk

Hii ni mada pana yenye mambo mengi mno.

Kwa mfano kitunguu saumu ni tiba kwa mtoto anayelia na kushtuka usiku, Kijiko cha asali ni tiba kwa mtoto anayekohoa mfululizo (ukiacha kifua na mafua), Vitu kama mahirizi ya kiunoni na mkononi havimsaidii mtoto, Muda mwingi kumvalisha mtoto nguo nyingi humsababishia nimonia n.k.

Mambo ni mengi...

IKIWAPENDEZA ITAKUWA NI MADA MAALUMU YA WATOTO..

Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha..!
Itakuwa darasa maridhawa kabisa
 
Jamani naimba mnisaidie kujua, kwann baadhi ya wanawake wakiwa wajawazito wanawachukia waume zao? Na ni nini maana yake?
 
Habari za jukwaa hili..
Tatizo ambalo linamsumbua mwanangu ni kila baada ya kula anatapika na tatizo hili limeanza leo asubuhi
Naomba ushauri na mawazo yenu kwa wazoefu wa tatizo linalo msumbua mwanangu. Ana umri wa mwaka mmoja na nusu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashauri mpeleke hospital lakini pia unaweza kumpa dawa ya minyoo kwanza
Habari za jukwaa hili..
Tatizo ambalo linamsumbua mwanangu ni kila baada ya kula anatapika na tatizo hili limeanza leo asubuhi
Naomba ushauri na mawazo yenu kwa wazoefu wa tatizo linalo msumbua mwanangu. Ana umri wa mwaka mmoja na nusu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Jr
 
Japo tunadhani kuwa changamoto za malezi ya mimba ni nyingi lakini kiuhalisia changamoto kubwa na za muda mrefu ni baada ya mtoto kuzaliwa mpaka atoke kwenye kile kipindi cha 'danger zone'
Sana asee.nawaza mimi mpaka hichi kipindi kiishe na dogo ni mtunduu balaaa
 
Maalum kwa watoto wa kiume
Si vema kumuwahisha tohara mtoto. ..hii ni kwa faida yake ukubwani, tohara inayowahi husababisha vibamia
Nagombana na baba ake kila siku alitaka nimpeleke hata 7hajamaliza ila nilijitahidi kumpotezea..natamani hata afike mwaka
 
Alimvalisha pampas?, zina madhara pia, kuna mama mmoja alikumbwa na hilo la mwanae kuumwa sana ngiri, aliposhauriwa aache kumvalisha pampas tatizo likakoma
Mungu Wangu baby wangu anatumia pampas, isije ikampata.japo huwa namuomba anayebaki nae mchana amshindishe na kptula tu.ila sidhani.mimi kama mzazi nakerwa sana nikisikia mda wote alimvalisha pampers
 
Pampas (diaper) ni kwa matumizi ya muda mfupi tuu ama dharura Ila wengi huchukulia ndio nepi.. Sio vizuri hata kidogo
Mungu Wangu baby wangu anatumia pampas, isije ikampata.japo huwa namuomba anayebaki nae mchana amshindishe na kptula tu.ila sidhani.mimi kama mzazi nakerwa sana nikisikia mda wote alimvalisha pampers

Jr
 
Ni kweli. Wa kwangu alikuwa hivi hivo hadi kitovu kinakuja juu. Dr akaniambia nimcheki hadi miezi mitatu.

Sikumpa dawa, zaidi nilikuwa namfanyia masaji kdg kdg kwa mafuta ya nazi.

Na kweli alipoingia tu miezi mitatu akawa yupo fresh na kitovu chake kimerudi vizuri.
Hata wakwangu kiliisha japo mwanzo niliogopa na sijampeleka hospitali.kiliisha tu.ila alikuwa anasumbuliwa na tumbo sana
 
Back
Top Bottom