Kwa wazazi na walezi: Mada maalum ya watoto

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Messages
4,019
Points
2,000

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined May 23, 2017
4,019 2,000
Uzi ni productive..
kwa watoto wanaosumbua kula kuna dawa inaitwa pharmactin
hii dawa huwa inasaidia sana kumuongezea mtoto hamu ya kula ila kwa experiency nilo nayo ukiandikiwa dozi ukaanza kumpa akianza kuchanganya kula usiendelee na dozi maana atakuwa msumbufu wa kuhitaji kula


Ushauri wa pili kama unasimu na unamuachia mtoto kuangalia video iweke kwenye flight mode

muwekee mtoto wako education videos za shule za chekechea kuliko kumuwekea nyimbo za bongofleva au video za ajabu ajabu. hili ninaushuda nalo kwa mwanangu niliye naye kwa sasa ana miaka miwili lkn anajua namba hadi 20 na anafahamu ABC...Z kutamka akiziona na kuziandika

mkaririshe mwanao namba moja wapo ya mzazi hii itakusaidia sana
mlishe mwanao samaki kwa wingi hasa sato au sangara inasaidia ukuaji wa ubongo na akili kwa mtoto

tenga muda wa kucheza na watoto wako hii inasaidia kumjengea mtoto mapenzi ya wazazi na kujiamini na kutokuwa na nidhamu ya woga

mjengee mwanao mazoea ya kuhoji na kuweza kutoa sababu ya anachohoji

hata kama uwe busy vipi jitahidi kuwatoa wanao out mkiwa wazazi wote wawili baba na mama. Jitahidi walau kula pamoja na watoto wako hata chakula cha jioni.

usigombane na mkeo au mumeo huku watoto wanashuhudia.
usimuongelee mabaya mkeo au mumeo mbele ya watoto.
Jitahidini kila mara watoto wawaone wazazi mna furaha.
Salini pamoja na watoto wenu kwa wakristo waweza teua mtoto aongoze sala
kwa waislamu kama wasalia nyumbani baba ongoza sala ila ukimaliza mwambie mtoto aombe dua.

mpongeze mpe zawadi mtoto pindi afanyapo jambo lolote zuri.
Afya ya mwanao ni muhimu fuatilia afya ya mwanao na tabia za mwanao mueleze wajibu wake ni nini kama mtoto na wewe kama mzazi wajibu wako nini
Mueleze mali ulizonazo ni zenu ninyi wazazi anatakiwa yeye baadae atafute mali zake atapokuwa mkubwa.

unapofikiria kuchepuka au kumfanyia vitimbi mwenzio kwenye ndoa ujue mwisho wa siku mtaachana na hakika nakiri Hakuna Mama kama mama na hakuna baba kama baba. hivyo mwanao hatopata malezi bora kama kutoka kwa baba halisi au kwa mama halisi, kwakuwa hakuna mzazi halisi apendae mwanae kuwa na mwisho mbaya.

Usimueleze mwanao matatizo ya baba yake au mamaake akiwa bado mdogo badala yake tatue matatizo na tofauti zenu kabla hamjapanda kitandani kulala. maana penye maudhi shetani hutawala mwaweza fanya tendo la ndoa mkazaa shetani badala ya binadamu Mshana Jr anaweza tolea ufafanuzi hili.

Ikumbukwe mtoto ni wako anapokuwa mdogo lkn akikua huwa ni wa jamii inayomzunguko lea mwanao kwa maadili mazuri ili tuwe na jamii Bora

Kumbuka hakuna mtu yeyote atayekulelea mwanao kama wewe mwenyewe mzazi.

Kumbukeni kuna maisha baada ya watoto wasisitize wanao kuheshimu kila binadamu duniani


Kama hakuna ulizima usimpeleke mwanao boarding school akiwa vidudu na shule ya msingi, hii inaweza sababisha mtoto akakosa mapenzi na mzazi.
msikilize mwanao usipende kumkatisha anapokuambia jambo hata kama nila kitoto au kipuuzi msikilize then shauri au onya au pongeza kutegemeana na jambo lenyewe. usipofanya hivyo utasababisha asijekukuambia lolote na akajenga nidhamu ya woga kwako.

Mwambie mwanao akuheshimu ila asikuogope
Ok noted boss lakini pia dagaa na migebuka hope inafaa maana laina wa pande hiyo wana akili na vipaji sema wabishi kisa dagaa
 

DsmicSound

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2015
Messages
1,430
Points
2,000

DsmicSound

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2015
1,430 2,000
Jamani naomba nijuzwe na wataalam na wazoefu...MIMI NAONA KUNA ILE TABIA MTOTO AKIANZISHIWA CHAKULA TU BAADA YA KUNYONYA MIEZI 6...BASI NI MTOTO NI MIUJI TUUUUU YA UNGA WA SEMBE...

KITU AMBACHO MIMI NAONA SIO SAWA...

HIVYO BASI NAOMBA UFAFANUZI WA KITAALAM NA KIZOEFU...NI CHAKULA GANI CHA KUMUANZISHIA...

VIPI KUHUSU ASUBUHI...MCHANA NA JIONI...
 

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
132,212
Points
2,000

Mshana Jr

Platinum Member
Joined Aug 19, 2012
132,212 2,000
Jamani naomba nijuzwe na wataalam na wazoefu...MIMI NAONA KUNA ILE TABIA MTOTO AKIANZISHIWA CHAKULA TU BAADA YA KUNYONYA MIEZI 6...BASI NI MTOTO NI MIUJI TUUUUU YA UNGA WA SEMBE...

KITU AMBACHO MIMI NAONA SIO SAWA...

HIVYO BASI NAOMBA UFAFANUZI WA KITAALAM NA KIZOEFU...NI CHAKULA GANI CHA KUMUANZISHIA...

VIPI KUHUSU ASUBUHI...MCHANA NA JIONI...
Si jambo jema kabisa.... Inapaswa kuchanganyiwa vyakula vya aina zote ili mtoto apate balanced diet
 

frem zero

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Messages
583
Points
1,000

frem zero

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2016
583 1,000
JAMANI MSAADA
Nina mtoto wa kike ana mwaka na miezi mitatu na nusu lakini hawezi kuita hata neno dada. Yaani hawezi kabisa ila akiona chakula anasema amu amu, pia anasema pipii pipiii . Sasa nikiwa kama mzazi naumia mno, maana watoto waliozaliwa chini yake wanatamka maneno mbalimbali ila yy hawezi. Kuna muda anatamani kuongea ila anaishia kupiga kelele. Nimemuangalia udata hana kabisa. Kinachonipa wasiwasi kuna shemeji yangu ni mlokole, kasema kaonyeshwa kuwa mwanangu kafungwa kuongea na wachawi eti wamemtupia kitu kifuani ndo kinachomzuia kuongea. Nisaidieni tafadhali wazazi wenzangu, mnajua kuwa mtoto asipokuwa sawa kiafya mzazi huwa anajisikiaje.
NB: MWANANGU ANATEMBEA VIZURI KABISA, ANACHEZA VIZURI , ANASIKIA VIZURI HATAA UKIMUITA KWA SAUTI YA KUNONG'ONA ANASIKIA NA KUBWA ZAIDI ANAELEWA VITU VINGI UKIMUONGELESHA TATIZO NI MOJA HAONGEI.
 

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
132,212
Points
2,000

Mshana Jr

Platinum Member
Joined Aug 19, 2012
132,212 2,000
JAMANI MSAADA
Nina mtoto wa kike ana mwaka na miezi mitatu na nusu lakini hawezi kuita hata neno dada. Yaani hawezi kabisa ila akiona chakula anasema amu amu, pia anasema pipii pipiii . Sasa nikiwa kama mzazi naumia mno, maana watoto waliozaliwa chini yake wanatamka maneno mbalimbali ila yy hawezi. Kuna muda anatamani kuongea ila anaishia kupiga kelele. Nimemuangalia udata hana kabisa. Kinachonipa wasiwasi kuna shemeji yangu ni mlokole, kasema kaonyeshwa kuwa mwanangu kafungwa kuongea na wachawi eti wamemtupia kitu kifuani ndo kinachomzuia kuongea. Nisaidieni tafadhali wazazi wenzangu, mnajua kuwa mtoto asipokuwa sawa kiafya mzazi huwa anajisikiaje.
NB: MWANANGU ANATEMBEA VIZURI KABISA, ANACHEZA VIZURI , ANASIKIA VIZURI HATAA UKIMUITA KWA SAUTI YA KUNONG'ONA ANASIKIA NA KUBWA ZAIDI ANAELEWA VITU VINGI UKIMUONGELESHA TATIZO NI MOJA HAONGEI.
Kabla hujamuamini huyo shemeji yako nashauri kapate ushauri wa daktari bingwa wa watoto
Nijuavyo mimi watoto hawafanani
Kuna wanaowahi kutembea kuna wanaochelewa
Kuna wanaowahi kuongea kuna wanaochelewa nknk
 

Caroline Danzi

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2008
Messages
3,619
Points
1,225

Caroline Danzi

JF-Expert Member
Joined Dec 19, 2008
3,619 1,225
Wengi wetu humu tunalea ama watoto wetu ama watoto wa ndugu jamaa na marafiki.

Tumekuwa na mada maalum nyingi za mambo tofauti kama urembo magari simu n.k. lakini hatujawahi kuwa na mada hii maalum ya watoto.

Kumlea mtoto tangu kutungwa kwa mimba mpaka kuzaliwa na hatimaye kulelewa mpaka kuvuka kile kipindi cha hatari si jambo dogo.

Changamoto ni nyingi hasa na zingine hatujui jinsi ya kuzitatua lakini tukiwa na hii mada hapa jukwaani tutashirikishana na kujuzana mengi kwa haraka na uhakika zaidi.

Kuna vitu vidogo vidogo ambavyo havihitaji daktari au ufumbuzi wake ni kama huduma ya kwanza kabla hujapata usaidizi mwingine. HII NI TOFAUTI NA JF DOCTOR.

Kwa mfano, ufanyeje;

-Mtoto anapolialia (mvue nguo zote, mlaze kifuani kwa mama yake wagonganishe matumbo)
-Mtoto anapopata gesi tumboni (tikisa coca cola toa gesi yote, mpe nusu kijiko)
-Mtoto anapopaliwa kila akila chochote (kubadilisha position unavyomshika wakati ananyonya, kunywa, au kula
-Mtoto anaposhtuka shtuka usiku na kulia sana Same as no. 1,

Hatari zimnyemeleazo mtoto;
-Umeme
-Maji
-Moto
-Mwanga wa Tv
-Simu, mawimbi yake
-Vyombo na vitu mbalimbali
-Madawa na vipodozi nk nk

Weka mbali na watoto vitu vyote day aina hiyo...ilinisaidia mimi, sina uhakika kama wengine itawafaa

Hii ni mada pana yenye mambo mengi mno.

Kwa mfano kitunguu saumu ni tiba kwa mtoto anayelia na kushtuka usiku, Kijiko cha asali ni tiba kwa mtoto anayekohoa mfululizo (ukiacha kifua na mafua), Vitu kama mahirizi ya kiunoni na mkononi havimsaidii mtoto, Muda mwingi kumvalisha mtoto nguo nyingi humsababishia nimonia n.k.

Mambo ni mengi...

IKIWAPENDEZA ITAKUWA NI MADA MAALUMU YA WATOTO..

Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha..!
 

Forum statistics

Threads 1,392,167
Members 528,552
Posts 34,100,407
Top