Kwa wauza maduka katika eneo unaloishi, ni bora ukaitika wakati unaendelea na shughuli zako

Cvez

JF-Expert Member
May 19, 2018
4,345
13,078
Wale wote mnaomiliki maduka maeneo katika eneo hilo hilo la nyumbani. Ndio inaeleweka kuWa mnafanya shughuli nyingine za nyumbani na kuuza duka pindi pale mteja anapojitokeza.

Kero ni pale mteja anakuja dukani kupata huduma unamsikia anaita hujibu chochote, mteja anaendelea kuita tu, halafu baada ya muda unajitokeza.

Ni bora ukaitikia na kumjulisha kuwa umemsikia halafu baada ya muda mfupi ujitokeze.
 
Watakwambia na wewe fungua duka lako, ni sawa sawa na ile ukiona mahindi yamepanda huna haja ya kulaumu nenda kalime ya kwako.
 
Binafsi huwa sipendezwi na watu wa namna hiyo,kwasababu nakuwa km napewa bure kumbe natumia pesa.
 
Back
Top Bottom