Kwa watu wa dini, hii imekaaje?

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,051
12,949
Sio kwa lengo baya. Nataka tu kujua.

Nina bosi wangu ni mtu wa dini sana na kusali/swali sana, ndie bosi wa mambo ya fedha. Sasa anachonishangaza yeye hataki mambo ya ujanja ujanja ofisini, maana yake hataki kushiriki mambo yote ya dili za ofisini.

Sasa tukitengeneza dili ofisini yeye ndie muidhinishaji wa mwisho, tunaweza kutengeneza dili la kulipa mfano suppliers hewa anajua kabisa hawa ni suppliers hewa lakini bado anatuidhinishia malipo na cha ajabu zaidi tukimpa mgao anachukua.

Ukimpa mchongo boss dili hii hapa piga huu mpunga hataki kwamba dini yake haimruhusu ila tukicheza hilo dili anatuidhinishia malipo na tukimpa mgao anachukua.

Au ndio ile kama ya mabinti wa mkoa mfani kanda ya juu kusini anakwambia wewe fanya tu si dhambi utapata wewe ingawa utamu tutapata wote.

Huyu bosi wangu kwa kweli ananiacha hoi.
 
Back
Top Bottom